KIKOSI CHA MPAJU ATINISU KILICHOLETA USHINDI NA KUSHIKA NAFASI YA TATU

Hawa ndo vijana walio tung'arisha na bado wanahamu ya kufanya zaidi ya hapa...

Kikosi toto cha Mpaju SC

Hiki ndicho kikosi cha Mpaju SC upande wa watoto kikiwa kwenye ziara katika shule ya msingi Mpolo.

Mpaju FC wakiwa kwenye Picha ya Pamoja

Mpaju FC wakiwa kwenye Picha ya Pamoja wakati wa Tamasha la Mpaju Week 2019 Uwanja vya Magereza Mbeya.

Tuesday, December 31, 2013

Mungu wetu sio pepe.



1
Nataka kata Utepe, Kwanza radhi mnipe.
Mchana kuko kweupe, Machoni nisiwakwepe.
Uone nina Pelepe, Rohoni kwangu mweupe.
Si Madenge si Kipepe,Viongozi msisepe.

Saturday, December 28, 2013

UTANDAWAZI na BIM, havitaki ubinafsi!!!!!



                       DUNIA ni kweli kijiji, "UBINAFSI" UTATUUA, TUUBORESHE haraka.
KUNA hisia kuwa WATANZANIA wengi, hatuna TABIA YA KUFANYA KAZI NJE YA NCHI. Sidhani kama ni JAMBO BAYA, pengine TUMEJITOSHELEZA. Lakini HOFU yangu, ni kuwa Hatuna UTAMADUNI wa kufanya KAZI zetu katika KIWANGO cha KIMATAIFA. Na kama

Friday, December 20, 2013

Kiswahili ama Kiingereza? KISWAKINGE chatumeza.



 1
Sauti juu napaza, Ajibu mwenye uweza.
Nataka andika meza,Karibuni mboga Pweza
Wapishi wamekoloza, Tule bila ya kusaza.
Chumvi yetu kuongeza, Hilo hatutokataza.
Kachumbari tengeneza, Utamu usochukiza.

SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA



1
Hao hasa ndio yanga, Kwao ndio kujipanga.
Okwi sifa sitapinga, Tano wakumbuka Yanga.
Wakongo waende yanga, Nonda alivyowapanga.
Wageni Yanga mapanga, Kuwamaliza wachanga.
Lengo kubwa lao Yanga, Eti Simba kuwatwanga.

Monday, December 16, 2013

Kama "Mapera",Fikra hizi nazo Feki!

Zamani, Tukuyu-MBEYA kulikuwa na vyakula na matunda mbalimbali pengine kuliko leo. Kulikuwa na aina ya “MAPERA” iliyofahamika kwa jina la “KALUNGA-MUNYU”. Mtu alikuwa hanunui MAPERA, zaidi

Friday, December 13, 2013

WAJENZI WA "BONGO" NA MASLAHI YAO


NANI ALIPWE NINI? KWA NINI?
BWANA MIHELA UNAJUA UNACHOKILIPIA?

 ",,,,,,,,,,KIBONGOBONGO,unaweza kujibu unavyoona, lakini ni vema sana kujua hasa Uthamani ama VALUE, yenyewe ndio nini kwa huyu MNUNUZI au CLIENT? Ili

Saturday, December 7, 2013

MSHAHARA, nani apewe zaidi, MENEJA au MFAGIZI? Kwa nini?



Moja kati ya masomo, ambayo wanafunzi siku kadhaa hapo nyuma tulikuwa tukifeli kwenye KIDATO cha SITA, ni UCHUMI. Ukisoma maswali yake, unaona kama tayari umefaulu, lakini majibu yakitoka unashangaa, alama kubwa ni “C”,pengine hata kitaifa. Sijui mambo yakoje kwa sasa. Lakini, badala ya

Friday, December 6, 2013

NELSON MANDELA-MUNGU AILAZE ROHO YAKE PEMA PEPONI



Ni Nelson Mandela, Muhimu kuliko Hela.
Alipendwa na Masela,Fukara na wenye Hela.
Wasomi wafunga tela, Kawafunza bila hela.
Lala Peponi Madiba,  Upumzike Wetu baba.

Nelson Mandela (18 Julai 1918 -  05 Disemba 2013)-Na  KEVIN BLOOM

"Fifty years ago Martin Luther King called out in hope, “Let freedom ring”. “Freedom” answered his call by walking out of Victor Verster Prison 27 years later - and the world embraced the human embodiment of that elusive concept in Nelson Mandela. The body that nurtured the concept is no more, and now the world again

Monday, December 2, 2013

SAYANSI YA NINI BONGO ?



Sayansi ni neno ambalo pengine watanzania tunalitamka sana. Kati yao wapo ambao tunalitamka na kulitumia vizuri, na pia ambao hatulitumii vizuri ama na hata kutolifahamu kabisa kama sio hata kulitamka na kulisikia.Ukianza kuzungumzia maana, unaweza kuzua UBISHI badala ya MJADALA, kitu ambacho ndio JADI yetu WABONGO. Lakini,  KIBONGOBONGO,potelea mbali acha tubishane tu mpaka tufe na NJAA. 

Kimsingi,

Sunday, November 10, 2013

Architectural Technology (ATy), Kibongobongo ni nini?



Kuongelea Taaluma usiyoijua na hasa kama hii, kidogo mtu unapaswa kuwa jasiri, ama chizi kabisa kama alivyoasa mwalimu Nyerere juu ya kugusa mambo ambayo wengi wamekwisha yafanyia kazi na kuamua tofauti na unavyodhani. Na watanzania ni wepesi wa kumchukia mtu anapoonekana kuwa muongo,Tanki linaomba watanzania wasilichukie kama huu pia ni uongo kwa sababu katika maisha, mara nyingi kuelewa ni kugumu kuliko kutafsiri, hivyo maana inaweza kueleweka kitaalamu na kikawaida na ama vinginevyo. Tanki, linawakilisha uelewo wa vinginevyo kama mbongo, na hivyo kutoa nafasi kwa wataalamu kutoa mwanga zaidi na sahihi katika mjadala huu muhimu kwa taifa letu. Architecture (A) ni Taaluma ya usanifu wa ujenzi, kimsingi kwa Tanzania

Friday, November 1, 2013

MATOKEO MAKUBWA SASA-BIG RESULTS NOW (BRN)

UFAULU USIORIDHISHA ni BORA kuliko UFELI USIOKUBALIKA.

Tamko la kubadilisha mfumo wa Alama wa matokeo a kidato cha nne na cha sita, umepokelewa kwa hisia tofauti na Watanzania ambao wana hamu ya kuona MATOKEO MAKUBWA SASA. Kufuatia matokeo ya

Saturday, October 26, 2013

TQM APPLICATION IN TANZANIAN SPORTS

"Football in Tanzania"

The World of today has witnessed the rise of sports as one of the palatable business. Tanzanians’ mentality has changed abruptly following the benefits accruing to the few sportsmen in the country epecially footballers. However, sports sector in today Tanzania is performing as poorly  as many other sectors. Scholars and media are unsuccessfully playing their best to alert the Government and stakeholders. This is the case to many countries of not only Africa but also the World at large.

Sunday, October 13, 2013

Uzee siyo miaka

Uzee bado Kufika, Ujana unanicheka
1
Tokea  nimeamka, Mwenzenu nasononeka.
Jikoni kutosomeka, Heshima inatoweka.

Saturday, October 5, 2013

"ELIMU BORA MUHIMU"

1
Tunaipenda elimu, Na mimi ninayo hamu.
Si  hii Bora Elimu, Elimu ya usanamu.
Elimu Bora timamu, Bora Elimu Kuzimu.
Itufaayo Elimu,Si lazima ya kalamu.
Fikra Bora muhimu, Kuboresha Ufahamu
Makuu sio muhimu, Muhimu ndio Muhimu.
ELIMU BORA TIMAMU, HUYAMUDU MAJUKUMU.

Thursday, September 26, 2013

USAFIRI - DAR-ES-SALAAM- Reli ni ukombozi wa MTANZANIA

 HONGERA JAKAYA NA MWAKYEMBE 
KWA KUITHAMINI ZAMANI

Rasilimali tulizonazo ni NYINGI na zinatosha SANA kututoa katika umasikini, kama tu tukiikumbuka ZAMANI yetu na KUITHAMINI.Tuache ubinafsi na tusiogope maumivu ya MUDA mfupi, ni kawaida mafanikio huja kwa JASHO.Reli ni zaidi ya mabasi yaendayo kasi, na pengine zingeboreshwa kwanza kabla, tena Tanzania nzima na sio DAR tu.

Mipango mingi Bungeni, Kumi asilimiani.
Wakuu wengi nchini, Masilahiyo mbonini.
Reli zetu za zamani, Anayeziua nani?

Wednesday, September 25, 2013

"Chancellor Of Germany" ni yuleyule Angela Dorothea Merkel

 Kashinda tena, kweli wanawake wanaweza!
Angela Dorothea Merkel



 Angela Dorothea Merkel (pronounced [aŋˈɡeːla doʁoˈteːa ˈmɛʁkl̩] ( listen);[1] née Kasner; born 17

Monday, September 23, 2013

WESTGATE CENTRE: YAVAMIWA! NA CHANZO BADO NI KIZUNGUMKUTI

Vyombo vya habari Afrika mashariki na kwingine Duniani,vinasikitishwa na kuripoti kwa mtindo tofauti kuhusu uvamizi ama utekaji nyara wa "SHOPPING MALL",kule KENYA. Cha ajabu, ukweli wa chanzo,

Sunday, September 22, 2013

MISS WORLD TANZANIA-Baadhi walalamikia Maandalizi

Newly crowned Miss World Tanzania 2014 Happiness Watimanya
Happiness Watimanya Miss World Tanzania 2014 (C) and her runners-up
 http://beautypageantnews.com/happiness-watimanya-crowned-miss-world-tanzania-2014/
 
BEAUTY PAGEANT NEWS Covering local, national and international beauty contests Photos of Miss Universe 2012 Olivia Culpo

Kwenye kurasa kadhaa za facebook, washabiki wamelaumu ZAWADI na BURUDANI kuwa hazikuwa na

Saturday, September 21, 2013

MBEYA CITY AGAIN

Kile kilichokuwa kikisubiriwa na wapenda soka wengi Tanzania leo kimetimia. Matokeo ya mchezo kati ya mabingwa kutandaza Soka nchini Tanzania, Simba Sports Club na Vijana machachari kutoka Mbeya, yamedhihirisha kuwa Mabingwa watetezi Dar Young Africans hawana haki ya kuidharau timu ya Mbeya City

Sunday, September 15, 2013

Mbeya City Yadhihirisha kuwa Inastahili kuwa Ligi KUU



 Mechi baina ya MBEYA CITY ya jijini Mbeya na YANGA yenye makao yake jijini Dar Es Salaam, zimetoka uwanjani na kukubali kuambulia pointi moja kila moja baada matokeo halali ya 1-1. 

Wednesday, September 11, 2013

MIGOMO YA WALIMU WA "CHEKECHEA" UJERUMANI

CHANZO NI NINI? TUJIFUNZE NINI SISI WABONGO?
 
Ni Kawaida kwa wafanyakazi wa kitanzania kuona MISHAHARA ndio suluhisho la matatizo yao! Pengine ni hivyo duniani kote kwa sababu ndio hasa chanzo cha kipato tegemewa.Lakini, chanzo kikubwa cha mtu kuichukia kazi mara nyingi sio, MSHAHARA, bali zaidi ni mazingira yaendanayo na kazi na hasa thamani apewayo mfanyakazi, kuanzia vitendea kazi mpaka heshima, maarufu kama MARUPURUPU. Hili

MADAWA YA KULEVYA-KULIKONI TANZANIA?

Madawa yenye kulevya, Nahisi Yametulevya.
Juma Sala na Kaluvya, Hakuna yasomlevya.
Tulilamba tukachovya, Tunajidunga  kilevya.

Monday, September 9, 2013

REALITY QUEEN OF SAFARI- Ina maana gani kwa Watanzania?

MALKIA WA SAFARI KUTOKA UJERUMANI, APATIKANA TANZANIA  

JULIA!!!!!!!!!!!!!!!!REALITY QUEEN OF SAFARI, ni kitu cha kihistoria kwa Tanzania. Fuatilia zaidi

Tuesday, September 3, 2013

Building Information Modelling (BIM) in Tanzania

 "A chance to win the global battle, in Construction Industry"

OVERVIEW

It is common for the Tanzanian government to take long to act on issues raised by the scholars or writers, although it may not be the case in political stories. Total Quality Management philosophy has been as far back 1990s ((Hellard, 1993), Rutaguza, (1997), (Mosha,2007), (World Bank, 2000))  been proposed to build quality culture education and construction industry, but only until  today only few sectors has recognized (Ministry of Health and Social Welfare, 2009), never the less with support from abroad. Today, BIM rise as

Sunday, August 25, 2013

JE BAGAMOYO STARS ITATUVUSHA HAPA?

Swali kubwa kwa wanabagamoyo, ni nini kifanyike ili waweze kucheka ZAIDI ya walivyocheka siku za Timu za zamani kama Mwenge, Chai na Kurugenzi, ama zaidi TUKUYU STARS maarufu kama
Banyambala walioweza kupanda daraja na kutwaa ubingwa wakiwa na wachezaji na Kocha mzawa wa Tanzania. Tanki lina hili la kuchangia.


Mi  si wa enzi za mwenge, Ila namjua Mwenge.
Alipenda atupange, Kwa pamoja tujijenge.
Mbiu yetu tuitunge, Tuijue  tuichunge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.

Msondo ngoma, wanaweza sana!!!!!

 "Baadhi ya wasanii wa bendi ya msondo ngoma wakitumbuiza kwa mara ya kwanza baada ya mwanamziki mkongwe wa bendi hiyo muhidini Gurumo kustaafu kutoka kushoto ni Shabani Lendi,Hamisi Mnyupe,Saidi Mabera,Juma Katundu na Mustafa Pishuu." Chanzo:- burudani.blog

"SHETANI ANATUTINGA"

Kabila langu Mkinga, Si Mkinga kwa kupinga
Machache mimi napinga, Hata kwa wangu Ujinga.
Mkono mimi napunga, Si Mafinga hata Mbinga
 MUUMBA TUNAMPINGA, SHETANI ANATUTINGA

Saturday, August 24, 2013

TIMU YA MBEYA CITY



KILA LA KHERI MBEYA CITY
Tanki linawatakia Mpira Mzuri na Ushindi Mnono!!!!!!
(PICHA NA BASAHAMA BLOG)

Sunday, August 18, 2013

KIPAJI NI ASILI HAKITUPWI!!!!!!!!!!!!

Watanzania wengi wa leo wanaongelea vipaji, pengine kuliko kitu chochote. Wengine huongea pengine bila kufahamu hasa kuwa wanachoongela ni VIPAJI. Kipaji ni UWEZO wa ASILI wa KIPEKEE alionao MWANADAMU,kutoka kwa MUNGU.Ukiangalia KIPAJI kama TALENT (Kiingereza) unaweza

Saturday, August 17, 2013

ZAMANI KUNA MBELENI

1

Enyi wetu wa zamani,Radhi yenu niwieni.
Wekeni yenu pembeni,Someni yangu hewani.
Mimi sio wa zamani,Napenda jua zamani.
Yangu haki naamini,Yangu kuweka hewani.
Kwa wote mlo makini,Yawekeni  akilini.
Yeyote mwenye imani, Msingi wake zamani.
TUMEITUPA ZAMANI, TUTAJUAJE MBELENI.

BAGAMOYO STARS-TUKUYU (MBEYA)


Kutoka http://www.basahama.blogspot.com. Tanki, linapenda kutoa pongezi za dhati kwa wahusika wote walioweza kufanikisha suala la KUANZISHWA kwa TIMU ya MPIRA wa MIGUU-BAGAMOYO STARS. Washabiki wa soka wa kitongoji cha bagamoyo,Tukuyu na TANZANIA kwa namna au nyingine watakuwa wamefarijika sana kwa taarifa hii pia.

Friday, August 9, 2013

SALAMU ZA IDDI - 2013!!!!!!



Thelatha kumi timia, Wetu mfungo sawia.
Mwana IDI katujia, Kheri katuletea.
Kesho tunafungulia, Ya kheri kutoachia
Salamu zangu pokea,Za  IDD nawatumia

Monday, July 22, 2013

SONGEA

Inauma kusikia, Songea imeumia.
SONGEA: Mwaka 1991, Yusuph Mayanga, Juma Ahmed Mpangule na Hamidu Abdalah

Nimekumbuka Songea, nimeshindwa vumilia.
Mfaranyaki tokea, majimaji tembelea.
Bombambili pandishia, Matarawe potelea
Inauma kusikia, Songea imeumia.

Sunday, July 21, 2013

SWAIBA KAMATA NJIA


“Swaiba kamata njia, Mimi nakusubiria”
Kama ndoto nakwambia, Siku hii kuwadia
Nauli imetimia, Sasa tuache kulia.
Hebu tiketi chukua, Nini wasubiria
Swaiba kamata njia, Mimi nakusubiria.

Wednesday, July 17, 2013

Mchumi wetu Mchumi, Mchumi acha umimi



Mchumi huyu Mchumi, Mchumi wetu mmimi.
Apanga mambo kivumi, Apangavyo si kichumi.
Kupanga huku uchumi, Kupanga gani Mchumi.
Mchumi wetu Mchumi, Mchumi acha umimi

Sunday, July 14, 2013

KANDANDA LA BONGO




Vijana waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.

Fimbo tangia kitambo, Kwao TFF ni wimbo.
Bora wale wa kitambo, Waliweza wetu wimbo.
Wa leo twaona mambo, Na Mengi yao majigambo
Vijana waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.

Monday, July 8, 2013

BAJETI YA TANZANIA 2013-14: Kama kupanga ni matumizi,WAKULIMA TUMO!



"Upenyo Sahihi wa kuboresha Bajeti ni kupitia Kuongeza Makusanyo Yetu".

Kila mtanzania ana haki ya kusema moja au kadhaa kuhusu bajeti ya nchi yetu maana kwa namna moja u nyingine itakuwa inamgusa tu! Wengi wameitazama kwa jinsi wainavyo, na kuitathmini kwa jinsi waonavyo kuwa ndio sawa!

Saturday, July 6, 2013

KISWAHILI



„KISWAHILI Muhimili, Ni Roho mengine mwili“

Kiswahili Kiswahili, Hebu wote tujadili.
Vifimbo Cheza wa hili, Mudahili Umahili.
Daima tunajadili, Madini si Kiswahili.
 KISWAHILI Muhimili, Ni Roho mengine mwili .

Tuesday, June 25, 2013

TULIANZA KUTUKANA, TUMEANZA KUPIGANA

"TULIANZA KUTUKANA, TUMEANZA KUPIGANA"

Imani nawe Amina, kama kesho kama jana.
Ugumba na wengi wana, neema za maulana.
Wote kwake nyie wana, ajua zenu amana.
TULIANZA KUTUKANA, TUMEANZA KUPIGANA.

Monday, June 24, 2013

Prof J! Hii Hapana

 Kwenye Mkasi na Profesor J!!
 http://www.youtube.com/watch?v=-8rXXIpmPa0, Salama Jabri akiendesha vizuri kipindi hiki, mengi mazuri aliyaongea mwanamuziki mkongwe na bora wa muziki wa HIP-HOP, Professor J.

YOTE, Nimeyapenda ila kidoooooooogo, kwenye hili moja! "Kila anachofanya Mwan HIP-HOP hapa TANZANIA kwa sasa, mimi NIMEKWISHA FANYA". Profesor J, hapo tutake radhi mashabiki wako na hasa wa Hip Hop! Hasa nikisikiliza nyimbo kama NJE YA BOX ya NIKKI wa pili http://www.youtube.com/watch?v=djSJz4T6tcU, na DEAR Gambe wa Dogo Young Killer!!!!!!!!!!!!

Tuesday, June 11, 2013

MAONI JUU YA RASIMU YA KATIBA MPYA-1



KWANZA TUNAIPONGEZA HATUA NZURI NA KAZI NZURI ILIYOFANYWA NA TUME YA KATIBA MPYA. 

LAKINI MAONI YA MABORESHO PIA MUHIMU. NA KAMA ADA, NI VEMA KUWEKA WAZI KUWA MAONI HAYA YANAWEZA KUWA NI SABABU TU YA UPEO MDOGO WA KUIELEWA RASIMU, ILA NI VEMA KUTOA KULIKO KUJA KUJILAUMU KWA KUTO KUTOA MAONI. 

WANASHERIA NA WADAU WENGINE WENYE UJUZI ZAIDI TAFADHALINI TUONGOZENI KATIKA HILI


KUTOKA TANKINI

LUGHA YA TAIFA NA LUGHA ZA ALAMA
4.-(1) Lugha ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano ni Kiswahili na itatumika katika mawasiliano rasmi ya kitaifa na kiserikali.

Wednesday, April 24, 2013

BUNGENI NA WABUNGE



Wakati Kikao cha 11 sijui, kikiwa kibichi kabisa,tayari kumekuwa na mambo kibao kutoka Bungeni, ambayo unaweza kuyatafsiri vyovyote utakavyo. na Watanzania kama kawaida yetu, KILA mmoja anachagua wa kumtetea. Ili mradi mtu utoe HOJA. Tanki linaomba kuchangia kidogo, katika mijadala yetu mbalimbali juu ya mwenendo wa BUNGE letu, NA TANKI NALO NI LA BONGO VILEVILE, hivyo ulisome KI-BONGO BONGO.

Ukiangalia Kifungu cha 63 (2) cha Katiba ya Juamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama sehemu ya pili, Bunge

Tuesday, April 23, 2013

DARASA LA SABA KUJIUNGA CHUO KIKUU

ELIMU YA JUU 

NI HAKI YA KILA MTANZANIA, 

HIVYO 

TUBORESHE WAZO BADALA YA KULIPINGA


Kwa mujibu wa Ibrahim Yamola, Mwananchi katika kiungo  (http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1753450/-/12aid4m/-/index.html), Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.

Monday, April 15, 2013

BUNGENI: HOJA YA BANGI IFANYIWE KAZI NA IISHE

HOJA YA BANGI: Wakisema nchi za Ulaya tutakataa?

Pengine LAWAMA ije kama Mbunge hakutoa Tathmini ya kina JUU ya FAIDA na HASARA za BANGI na SIGARA! Kiasi cha kutufanya tushindwe kuamua kipi bora. SIDHANI kama hoja hii inapaswa kuwa kama Nyongeza,ukiangalia uzito wake katika jamii, endapo itapewa maamuzi chanya!

Friday, April 12, 2013

TANGANYIKA NA ZANZIBARI



“ENYI WANANGU WAWILI, TANGANYIKA ZANZIBARI

Kweli mwanangu Akili, Hebu mwanangu fikiri.
Fiki mwanangu wa pili,Nawe mwanangu subiri.
Nyie wanangu wawili,Msifanye ya Bakiri.

Friday, March 29, 2013

KATIBA YETU MPYA TUIPIMEJE UBORA WAKE?



 " IWE NA UWEZO WA KUTUFANYA 
TUUOGOPE UONGOZI , TUPENDE KUFANYA KAZI NA TULIPENDE TAIFA LETU KULIKO KITU KINGINE CHOCHOTE"

Maana yeyote ambayo mtu atatoa kuhusu katiba inaweza kwa namna moja au nyingine ikaangukia kwenye maana ya kuwa KATIBA ni MAKUBALIONA JUU YA MWONGOZO WA JAMII AU TAIFA FULANI. Huwa ni MSINGI wa MUAFAKA katika UTAWALAJI na UENDESHAJI, wa TAIFA au JAMII husika, na hata kikundi katika kufikia Mafaniko Bora. Pengine kutokana na uzito wake ndio

Saturday, March 23, 2013

"MLALA HAI vs MLALA HOI"



 "MLALA HAI vs MLALA HOI".


Mlala HAI kasema,
Mlala HOI kubali.
Mlala hai kisima,

Sunday, March 17, 2013

JESHI LA KUJENGA TAIFA, LAZIMA?!! KIVIPI?!!



MPANGO WA LAZIMA KUPITIA JKT, HAUNA MASLAHI MAKUBWA KWA TAIFA LETU

NUKUU YA 1.  KUTOKA KWA DEUDATUS BALILE, 04 March 2013 09:45  “http://modans.go.tz/site/index.php/jeshi-la-kujenga-taifa-laagizwa-kuajiri-vijana-wa-kujitolea-“
 
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ameliagiza Jeshi           la Kujenga Taifa (JKT) …………..Hayo aliyasema hivi karibuni alipotembelea  Makao     Makuu  ya  JKT,  jijini Dar es Salaam  ikiwa ni mara yake ya  kwanza  kwa  Makao Makuu             hayo kutembelewa na Rais  aliyeko madarakani tangu JKT ianzishwe mwaka 1963. 

Saturday, March 16, 2013

SALAMA JABRI :TUONGOZE WATANZANIA KUMPATIA TREKTA KING MAJUTO

Watanzania tuyatafute matatizo yetu  na kuyatatua badala ya kuyasubiri na kuyafanya DILI.

Mzee Majuto, sisi wengi tunamfahamu kwa vichekesho vyake vyenye maadili na mafunzo kwa jamii yetu. King Majuto kwenye kipindi cha Mkasi, cha Salama Jabri (SO5E12-with Majuto:http://youtu.be/bmTuxMSmRMY) aliongea vizuri sana, na kilichonivutia zaidi katika maongezi yake, ni PAMOJA NA

Sunday, March 10, 2013

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC): MAISHA NI NYUMBA NA NYUMBA NI PESA!



 "KAMA TUSIPOPATA FAIDA IMEKULA KWA WALALAHOI MARA MBILI"

NANUKUU Taarifa iliyotolewa na Shirika la Nyumba, ya 24/10/2012 kwenye uzinduzi wa uuzwaji wa nyumba mradi wa MINDU,Dar Es Salaam, “Kila nyumba itauzwa kwa bei ya TZ S 272,050,673.08 bila kodi ya ongezeko la thamani (VAT ) na  TZS 321,019,794.24 ikiwa na  kodi ya ongezeko la thamani  ( VAT )

Saturday, March 9, 2013

SIKUKUU YA WANAWAKE DUNIANI



WA-BONGO TUPUNGUZE KUSHABIKIA SHEREHE ZENYE
 TIJA NDOGO KWA TAIFA LETU

"MWANAMKE NA MWANAUME WOTE MUHIMU NA KILA MTU ANA HAKI ZAKE NA WAJIBU WAKE, TUSIDANGANYIKE" 

Badi Abu Al-farouq akijibu kupitia ukurasa wake wa “Facebook” wenye mafunzo mengi sana ya DINI YA KIISLAMU alisema ,“ Juma Mpangule uislamu umemtukuza sana mwanamke Alikuja mtu kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Ewe Mjumbe wa Allah! Ni nani mwenye haki zaidi miongoni mwa watu kwa mimi kusuhubiana naye kwa wema?” Akasema: “Mamako”. Akasema: “Kisha

Wednesday, February 27, 2013

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012-TANZANIA



 "LAWAMA HAZIJENGI, 
TUACHE KUENDEKEZA FIKRA MBOVU"

Ni vema kuanza kwa kujipa pole kama watanzania kwa mlipuko wa matokeo, ya kushangaza kiasi cha kufanya nchi na hata pengine Dunia kupigwa na butwaa! Maji yamekwisha mwagika, na hivyo ingekuwa vema mitandaoni kujae jinsi ya kutatua tatizo na sio maneno ya kashfa kwa viongozi na kunyoosheana vidole

Monday, February 25, 2013

SIMBA SPORTS CLUBS - "Yaani mimi, Simba inapovurunda ndio naipenda sanaaaa!"



TUJENGE UWANJA KWANZA


TAIFA KUBWA 
NI


“MPIRA BORA KWANZA , MAGOLI, UBINGWA BAADAE”

USIYETAKA HILI HAMIA YANGA

Nakumbuka ilikuwa mwaka 1989, wakati naamini,ndio hasa nilipoweka sahihi ya kuwa nitakuwa mshabiki wa WEKUNDU MSIMBAZI MPAKA KUFA KWANGU. Hii ilikuwa ni baada ya kuwaona wachezaji kama Dan Mhoja, kama sikosei pia John Makelele akitokea benchi. Wengine Mtanisaidia mliokuwa

Sunday, February 17, 2013

Kilimo Kwanza: Ni Kauli Mbiu ya Msingi kwa Taifa?



 Watanzania tunahitaji kufahamu Imani na Misingi ya Taifa Letu.
Misingi ya Taifa letu ndio Roho ya Taifa Letu.
Kuilinda na Kuboresha Misingi Yetu,Ndio Kulinda na Kuboresha Taifa Letu


Umuhimu wa misingi sio tu kwa taifa, bali hata mtu binafsi na familia ama ukoo. Lazima kuwa na misingi ambayo ndio dira ya matendo na maamuzi yako au yenu. Mara nyingi tunapokosa kuwa na Misingi Bora huwa tunaishia kuyumba bila kujua chanzo hasa cha kuyumba ni nini. Hatujui mchawi hasa ni nani!

Tuesday, February 12, 2013

Mtanzania Acha Mipango ya Ujanjaujanja

MAFANIKIO  BORA YANAHITAJI MIPANGO BORA KWANZA
Umuhimu wa mipango bora kwanza
Ukiona vinaelea Ujue vimeundwa. Ni kama kusema mambo mengi mazuri hutokana na kuumiza kichwa "Fikra Bora". Au Kupanga Kwanza ndio Msingi wa mafanikio. Kwa kweli Kubahatisha mafanikio katika

Sunday, February 10, 2013

BUILDING INFORMATION MODELLING (BIM - "BULL'S EYE" TO TANZANIA




 ACADEMICIANS AND PROFESSIONALS MUST ALERT THE GOVERNMENT
 Jiang, Xinan (2011) quoted National Institute of Building Sciences (NIBS 2007), that BIM is a computable representation of all the physical and functional characteristics of a building and its related project/life-cycle

Thursday, February 7, 2013

TANZANIA YAWA KENYA KWENYE MAONYESHO YA "AFRICAN DAY IN GERMANY"

"HAPA NI KENYA NA TANSANIA IPO HAPAHAPA"

Unaweza kuwa na kila kitu, ukikosa fikra bora umekwisha, unaishia kunufaisha wengine.
Watanzania Tuamke na Kuingia Duniani Kutafuta Sasa
Mtu kwao bwana, mambo ya kanga, chai,"gahwa" na kadhalika, watu twaonja tu! Ukigundua kanga imeandikwa nini utakubali kuwa watanzania tumelala.
Siku ya tarehe 26 mwezi wa kwanza, hapa Koln, moja kati miji mikubwa ya Ujerumani kwenye moja ya majumba ya makumbusho kulifanyika maonyesho, ambayo kwa mujibu wa hapa na pale ilikuwa ni siku ya

Monday, January 28, 2013

UTUMWA WA KIFIKRA SASA BAAAAAAAAAASI!!!



"Kuogopa Ukweli 
Kunatugharimu Sana Kimaisha"
Mara nyingi tunapoongelea Utumwa tunamaanisha ile hali ya Umiliki wa Binadamu  na kumfanya kama bidhaa. Inawezekana kukawa na kufanana kwa baadhi ya vitu, lakini pia hali ya kuwa huwezi kufanya maamuzi fulani sahihi kwa sababu tu unaogopa kuwa utakuwa unapingana na ukweli au uhalisia, na hivyo unalazimika kuendelea kufanya yasiyo sahihi kuyafanya tunaweza kuiita utumwa wa kifikra.

Monday, January 14, 2013

TQM FOR TANZANIAN EDUCATION QUALITY IMPROVEMENT

(A review paper of  Total Quality Management application at Ardhi University)
Improving the quality of education may give the best solution to many Tanzanian Social, Economical and political problems in the end. Tanzania of today the question is not more of the quantity of educated people (Tanzanians) but rather the people with quality education to productively guide the country through the expected results of the growth and development.  Actually, being a Tanzanian today means unethical, sluggish, extravagant, treacherous and the like (MBONGO MAN). It is not uncommon for a Tanzanian to be late in the meeting and be happy,or likewise to 100% give self interest priority over the nation interest in the purely public undertakings. That is why even the key organ like Parliament is sometimes street joked to be like a movie or comedy episode. All of these gives the signs that our education system may not be serving Tanzanian or doing it at minimal level. We are not too old to learn.

Sunday, January 13, 2013

KATIBA MPYA YA TANZANIA


"chonde chonde, misingi,haki na wajibu vipewe kipaumbele"

 “MAAMUZI YETU NDIO HATIMA YETU”

Maoni kwenye katiba ni muhimu sana, na watanzania wote tulione hili kuwa ni jambo linalotuhusu sisi na vizazi vyetu, tuweke ITIKADI, JAZBA, KASUMBA(UBINAFSI) NA IDEOLOGIES zetu pembeni, na kuchangia kwa dhati ya kujenga taifa la Tanzania, la leo na kesho.Pia Serikali na Wahusika wote wa

Sunday, January 6, 2013

KISWAHILI MUHIMU SANA KWA UBORA WA ELIMU YA TANZANIA


WAZO LA  KIZALENDO!
CHEKECHEA NA MSINGI: UNG'ENGE TU, NAOMBA TUSILIJADILI KWA SASA.

 TUJADILI  HILI  KWANZA
kuanzia SEKONDARI MPAKA SHAHADA tutumie

Saturday, January 5, 2013

KWELI SADIKI JUMA KILOWOKO AMEFARIKI DUNIA

SAJUKI

MWENYEZI MUNGU 
AMEMPENDA ZAIDI, WANADAMU HATUNA BUDI KUKUBALI. 

Tuesday, January 1, 2013

tunawatakia kheri ya mwaka mpya wa 2013


T