KIKOSI CHA MPAJU ATINISU KILICHOLETA USHINDI NA KUSHIKA NAFASI YA TATU

Hawa ndo vijana walio tung'arisha na bado wanahamu ya kufanya zaidi ya hapa...

Kikosi toto cha Mpaju SC

Hiki ndicho kikosi cha Mpaju SC upande wa watoto kikiwa kwenye ziara katika shule ya msingi Mpolo.

Mpaju FC wakiwa kwenye Picha ya Pamoja

Mpaju FC wakiwa kwenye Picha ya Pamoja wakati wa Tamasha la Mpaju Week 2019 Uwanja vya Magereza Mbeya.

Sunday, August 25, 2013

JE BAGAMOYO STARS ITATUVUSHA HAPA?

Swali kubwa kwa wanabagamoyo, ni nini kifanyike ili waweze kucheka ZAIDI ya walivyocheka siku za Timu za zamani kama Mwenge, Chai na Kurugenzi, ama zaidi TUKUYU STARS maarufu kama
Banyambala walioweza kupanda daraja na kutwaa ubingwa wakiwa na wachezaji na Kocha mzawa wa Tanzania. Tanki lina hili la kuchangia.


Mi  si wa enzi za mwenge, Ila namjua Mwenge.
Alipenda atupange, Kwa pamoja tujijenge.
Mbiu yetu tuitunge, Tuijue  tuichunge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.

Msondo ngoma, wanaweza sana!!!!!

 "Baadhi ya wasanii wa bendi ya msondo ngoma wakitumbuiza kwa mara ya kwanza baada ya mwanamziki mkongwe wa bendi hiyo muhidini Gurumo kustaafu kutoka kushoto ni Shabani Lendi,Hamisi Mnyupe,Saidi Mabera,Juma Katundu na Mustafa Pishuu." Chanzo:- burudani.blog

"SHETANI ANATUTINGA"

Kabila langu Mkinga, Si Mkinga kwa kupinga
Machache mimi napinga, Hata kwa wangu Ujinga.
Mkono mimi napunga, Si Mafinga hata Mbinga
 MUUMBA TUNAMPINGA, SHETANI ANATUTINGA

Saturday, August 24, 2013

TIMU YA MBEYA CITY



KILA LA KHERI MBEYA CITY
Tanki linawatakia Mpira Mzuri na Ushindi Mnono!!!!!!
(PICHA NA BASAHAMA BLOG)

Sunday, August 18, 2013

KIPAJI NI ASILI HAKITUPWI!!!!!!!!!!!!

Watanzania wengi wa leo wanaongelea vipaji, pengine kuliko kitu chochote. Wengine huongea pengine bila kufahamu hasa kuwa wanachoongela ni VIPAJI. Kipaji ni UWEZO wa ASILI wa KIPEKEE alionao MWANADAMU,kutoka kwa MUNGU.Ukiangalia KIPAJI kama TALENT (Kiingereza) unaweza

Saturday, August 17, 2013

ZAMANI KUNA MBELENI

1

Enyi wetu wa zamani,Radhi yenu niwieni.
Wekeni yenu pembeni,Someni yangu hewani.
Mimi sio wa zamani,Napenda jua zamani.
Yangu haki naamini,Yangu kuweka hewani.
Kwa wote mlo makini,Yawekeni  akilini.
Yeyote mwenye imani, Msingi wake zamani.
TUMEITUPA ZAMANI, TUTAJUAJE MBELENI.

BAGAMOYO STARS-TUKUYU (MBEYA)


Kutoka http://www.basahama.blogspot.com. Tanki, linapenda kutoa pongezi za dhati kwa wahusika wote walioweza kufanikisha suala la KUANZISHWA kwa TIMU ya MPIRA wa MIGUU-BAGAMOYO STARS. Washabiki wa soka wa kitongoji cha bagamoyo,Tukuyu na TANZANIA kwa namna au nyingine watakuwa wamefarijika sana kwa taarifa hii pia.

Friday, August 9, 2013

SALAMU ZA IDDI - 2013!!!!!!



Thelatha kumi timia, Wetu mfungo sawia.
Mwana IDI katujia, Kheri katuletea.
Kesho tunafungulia, Ya kheri kutoachia
Salamu zangu pokea,Za  IDD nawatumia