![]() |
| MPAJU FC QUEENS a.k.a ATINISU. "HATUCHOKI HATA TUKICHOKA" |
Safari ya Mpaju FC Queens (Atinisu) katika WRCL 2025, IMEISHIA NUSU FAIANLI, lakini imekuwa ushuhuda wa ujasiri, nidhamu, na kujitoa kupita matokeo ya kawaida ya soka. Licha ya changamoto kubwa za kifedha, uchovu wa safari, na upungufu wa wachezaji, wasichana hawa wamepigana kwa heshima na kulibeba jina la Mkoa wa Mbeya kwa fahari.
Katika robo fainali, wakiwa na wachezaji 11 pekee, Mpaju FC Queens walipata ushindi wa kihistoria wa 3–2 kwa kushinda wakitokea nyuma (2-1)— ushindi uliothibitisha moyo wa ushindani na mshikamano wa timu. Nusu fainali iliamuliwa na penati ya dakika za mwisho, ambapo Mpaju walipoteza 1–0 dhidi ya Serengeti Queens.
Kabla ya mchezo wa kuwania nafasi ya tatu dhidi ya Mandozi Academy, klabu na jamii ya Mbeya tunasimama kusema AHSANTENI MPAJU FC QUEENS (ATINISU). Hii ni heshima kwa juhudi, si kwa matokeo pekee.
Mwisho wa safari hii unatukumbusha somo muhimukutoka kauli mbiu ya taasisi yetu ya (Mpaju Galaxy): Uwezo ukionyeshwa kwa vitendo, huwa na mamlaka.
...........Buruhani Ina Mamlaka....................







0 comments:
Post a Comment