Monday, December 15, 2025

KABLA YA MATOKEO, HESHIMA: SHUKRANI KWA JUHUDI ZA MPAJU FC QUEENS (ATINISU) – WRCL 2025

 


Ujumbe huu haujaandikwa kwa sababu Mpaju FC Queens (Atinisu) wamefuzu robo fainali za WRCL 2025, bali kwa sababu ya juhudi kubwa, nidhamu, na uvumilivu waliouonesha katika mazingira magumu kupita kawaida.

Kufuatia changamoto za kifedha na zuio la usafiri tarehe 9–10 Desemba 2025, timu ilifika Mwanza asubuhi ya tarehe 12 Desemba na kucheza siku hiyo hiyo, ikipoteza 3–2 dhidi ya Mandozi Academy Queens, vinara wa kundi. Kufunga mabao mawili siku ya kufika ni ushahidi wa moyo wa ushindani na heshima ya kitaasisi.

Mpaju FC Queens na Victoria Queens walimaliza kundi wakiwa na pointi sawa, tofauti ya mabao sawa, na sare ya ana kwa ana. Kwa mujibu wa kanuni, idadi ya mabao yaliyofungwa ilitumika, ambapo Mpaju FC Queens walifunga mabao 5 dhidi ya 4 ya Victoria.

Kabla ya robo fainali dhidi ya Dhujau Queens (Katavi), uongozi wa klabu unasema AHSANTENI kwa wachezaji, benchi la ufundi, na wadau wote. Msaada WENU unaonyesha wazi kuwa Mpaju FC tayari ina mtaji mkubwa wa kijamii (social capital) unaostahili kuheshimiwa na kuendelezwa.

HAKIKA .....BURUHANI INA MAMLAKA.........!

0 comments:

Post a Comment