Sunday, September 28, 2014

MZUMBE SECONDARY SCHOOL ALUMNI

"WAZUMBE"
WAUNGANA KATIKA HARAKATI ZA KUJENGA TAIFA. 

Naomba kutumia andiko la
Rahim Mzee Kachwamba (Mzumbe Sec PCB 1996-1998)
Mjumbe wa Sekretarieti ya kuanzisha Mzumbe Sec Alumni)

kuwafikishia  taarifa WAZUMBE na WATANZANIA wenzangu TUKIO hili la MUHIMU.


AMEANDIKA;
SAFARI YA KWENDA MZUMBE SEKONDARI ILIFANA SANA..
Nachukua fursa hii kuwajulisha kwamba safari yetu ya kutembelea shule yetu ya Mzumbe ilifanyika kwa mafanikio makubwa sana. Kwa ufupi yafuatayo yalijiri katika safari hiyo (SIO TAARIFA RASMI):

KWA UJUMLA

1. Safari ilijumuisha Wazumbe kuanzia mwaka 1966 mpaka mwaka 2014
2. Alumni wa Dar tuliondoka kwa usafiri wa pamoja (Coaster)
3. Tuliungana na Wazumbe wanaoishi Morogoro, Tanga na Dodoma pale Morogoro Mjini na kuongozana nao mpaka shuleni Mzumbe

Kutoka Kushoto Rahim Mzee, akiwa na mwakilishi mwenzie wa MZUMBE ALUMNI Eddy Talawa baada ya kukabidhi  nyaraka kwa Wajumbe wa Bodi ya Shule
 KWA KWELI

4. Tulipokelewa kwa vifijo na nderemo na kiukweli kuna matarajio makubwa sana toka kwetu kuisaidia shule hii
5. Tulikutana na uongozi wa shule, walimu na wafanyakazi wasio walimu, diwani wa eneo la Mzumbe pamoja wa wajumbe wa Bodi ya Shule. Wadau wote hawa wana matumaini makubwa sana kwamba tutawasaidia katika kutatua changamoto zinazoikabili shule yetu.




PIA

6. Tulitembelea maeneo ya shule ikiwemo mabweni, madarasa, maabara, ofisi za walimu, vyoo na maliwato, maktaba, mfumo wa maji safi na maji taka. Kwa ufupi hali ya miundo-mbinu ya shule ni sio nzuri. Kwa mfano mfumo wa maji safi wa shule (toka chanzo milimani Mongwe) haufanyi tena kazi tangu mwaka 2006 baada ya mabomba kuzolewa na mafuriko ya mvua. Kwa sasa shule imeomba msaada na imeunganishwa ktk mfumo wa maji safi wa chuo kikuu Mzumbe kwa muda. Hata hivyo maji haya si ya uhakika na pindi chuo kikifunguliwa kunakuwa na uhaba mkubwa sana wa maji. Samani (viti. meza nk) za shule zimechakaa sana. Maktaba ina vitabu vya zamani sana na vimechakaa. Sehemu kubwa ya mfumo wa maji-taka haufanyi kazi mfano ktk kijiji cha Karume kuna tundu moja tu la choo linalofanya kazi. Maabara zimechakaa, mabweni yamechakaa nk nk
7. Tulifanya kikao cha pamoja na walimu pamoja na bodi ya shule hasa kusikiliza matatizo yanayoikabili shule yetu. Shule imeandaa mpango-mkakati wa namna ya kukabili matatizo haya kuna harambee (fund-raising event mwezi Novemba kuchangia utatuzi wa matatizo yanayoikabili shule yetu)




 HALAFU
8. Tulikutana na kuongea na wanafunzi wote na hasa tukiwapa moyo wasome kwa bidii hata kama mazingira sio rafiki sana, na wana-alumni wakaeleza wasifu wao na mafanikio yao kimaisha kwamba yalitokana na kupita Mzumbe Sekondari. Wanafunzi walihamasika sana na walikuwa wakishangilia na kupiga makofi muda wote tulioongea nao
9. Tulizindua jumuia yetu (MZUMBE SECONDARY SCHOOL ALUMNI LTD) kwa kukabidhi nyaraka za usajili kwa mwenyekiti wa bodi mbele ya wanafunzi, walimu, diwani na wajumbe wa bodi ya shule.



 KISHA

10. Tulipata mlo wa mchana pamoja na wanafunzi (Pilao na soda) na wanafunzi walifurahi sana. Wakati wa mlo na baada tulipata kuongea kwa undani na kirafiki na wanafunzi bila kuwepo walimu wao ili kujua changamoto hasa zinzowakabili katika masomo na mazingira yao.
11. Tuliagana na wanafunzi pamoja na walimu na bodi ya shule na tulirejea salama salimini (Tunamshukuru Mungu kwa hili).

Sisi kama wawakilishi wenu hatukuweza kutoa ahadi yoyote ya kutatua matatizo ya shule zaidi ya kuwaeleza kwamba nia yetu ni thabiti kusaidiana na serikali na wadau wengine kutatua matatizo yanayoikabili shule. Na tukawambia kuwa jumuia ni changa kwani imesajiliwa wiki iliyopita tarehe 23 Sept, 2014. Na sisi ni viongozi wa muda na tunatarajia kufanya mkutano mkuu wa wanachama wote (mzumbe sec alumni) ambao pamoja na mambo mengine utachagua uongozi wa kwanza wa jumuia kulingana na katiba yetu (MEMARTS).

TUKAWAMBIA KWAMBA BAADA YA HAPO NDI TUTAWAELEZA NI MATATIZO YAPI TUTAWEZA KUSAIDIA KUYAKABILI.
Kwa hiyo tunawaomba pale tutakapopanga kufanya mkutano mkuu wa kwanza (AGM) tafadhali tuhudhurie wote tutakaoweza ili tuijenge Mzumbe yetu.
''DETERMINATION IS OUR MOTTO''
''NYAYO-NYAYO''
''MZUMBE MPYA, INAWEZEKANA''
nachukua pia fursa hii kuwashukuru nyote mlioshiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha tukio hili la kihistoria. (Tafadhali angalia taarifa ya habari ya ITV saa 2 usiku na Abood TV- wameahidi kuonyesha tukio hili, tulikuwa nao muda wote).

MWISHO WA KURIPOTI


TANKI LINAONGEZEA KIDOGO TU

PONGEZI KWA "WAZUMBE"
Watanzania tusijadili, kama swala hili ni la KUPITA, kama MENGINE KAMA haya. Bali tujiulize kama ni JAMBO JEMA na SAHIHI. Kama SIO JEMA, basi TULIKOSOE, ili kuliweka SAWA. Ili NIA kuu yaani KUBORESHA  ELIMU na MAISHA YETU, iweze KUFANIKIWA. Kama ni JAMBO JEMA, basi VEMA liigwe, liendelezwe na liboreshwe DAIMA.

WAKATI, umefika  sasa wa kuthamini MASWALI, MAWAZO NA MITAZAMO SAHIHI kwa jamii yetu bila KUJALI ITIKADI,IMANI,MILA, NA HULKA ZETU.

"Utamaduni wa FIKRA ZENYE UBORA ndio MAMA wa MAWAZO endelevu na KIINI CHA MAFANIKIO YA KUDUMU "

"CHUNGUZA JANA YETU,TUOKOE LEO NA KESHO YETU"

2 comments: