Friday, January 3, 2020

WADAU WA SOKA JIJINI MBEYA WAFURAHIA MPAJU WEEK 2019

Washuhudia Mambo Mengi:

Vipaji vikali, Uongozi Madhubuti wa Mpira Mbeya Mjini,  Ushirikiano wa wadau wa Mpaju SC na bila kusahau, Timu ya wasichana ya shule ya msingi ya Mpolo-Mbalali, Uso kwa Uso na Mdau mkubwa wa Michezo nchini-Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Dr. Tulia Ackson.


Ile Kauli ya Hatua ni hatua, hatimaye imejidhihirisha kwenye tamasha la Mpaju Week 2019. Pamoja na Changamoto ya viwanja, kama vile uwanja wa Sokoine na FFU kufanyiwa Mabadiliko, kufuatiwa ratiba za ligi na mikutano ya shughuli za kitaifa, bado tamasha limefanyika kwa mafanikio makubwa katika Uwanja wa Magereza Ruanda Mbeya. Kwetu Mpaju SC, hatua hii tuliyofikia ni muhimu sana kuelekea katika mafanikio tarajiwa.

Uongozi wa Mpaju Sc, unapenda kutoa shukurani za dhati, kwa Uongozi wote wa Mpira wa Wilaya na Mkoa Mbeya kwa ushirikiano na msaada waliotoa ikiwa ni pamoja na mameneja na viongozi wote wa viwanja ambavyo tamasha hili lilikubalika kufanyika. Yaani Sokoine, FFU na Magereza. Bila wao taamsha hili lisingeweza kufanikiwa kwa kiasi hiki.

Uongozi wa Mpaju SC,umefarijika sana kupewa nafasi ya kuongea kwa karibu na Mh. Dr. Tulia Ackson juu ya chimbuko na maendeleo ya Mpaju SC, lakini pia kuweza kumkutanisha mheshimiwa na timu ya wasichana ya shule ya msingi ya Mpolo. Tunaamini ni hatua kuelekea mafanikio ya wachezaji,shule ya msingi Mpolo na hata Mpaju SC pia.

Zaidi, Uongozi wa Mpaju, unatoa shukurani kwa wadau woote (Akiwemo Mh Bashiru Madodi), kwa kusimamisha shughuli zake na sio tu ili kuwa katika kundi la wazazi walioleta watoto wao kwenye tamasha hili, bali alibaki mstari wa mbele kabisa kuhakikisha changamoto ya mabadiliko ya uwanja inapatiwa ufumbuzi wa kudumu, alisaidia sana kupatikana kwa uwanja wa Magereza ambao ndio tamasha hili limemalizikia kwa siku zote nne.

Sio mwisho umuhimu, uongozi unatoa shukurani kwa wadau, makocha na wanamichezo wote wanaoendelea kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha tamasha linaendelea kuwa bora na la kufurahisha leo, kesho na hata milele.Malk Consultants (Eng Mkisi, Lupakisyo,na Architect Kashula), Dr Said Mkungume na wengine wengi tunawashukuru kwa ulezi wao walioounyesha katika tamasha hili. Picha zifuatazo ni sehemu ya maelezo ya siku ya kwanza kwa kifupi.

Bila Kusahau, Uongozi unapenda kuomba msamaha kwa woote, kwa maeneo yote ambayo kwa namna moja au nyingine yaliwakwaza.

Figure 1: Mpolo Shule ya Msingi, wakiwa tayari kuwakabili Mpaju FC U-12 plae uwanja wa FFU-Mbeya
Figure 2: Mpaju FC U-12, wakimsikiliza Mwalimu wao Kocha Ali Mkumbukwa, wakati wa mchezo wao dhidi ya Mpolo Uwanja wa FFU Mbeya
Figure 3: Mpaju FC wakiliandama Lango la Mpolo katika uwanja wa FFU Mbeya

Figure 4: Golikipa wa Mpaju Fc U-12 (Omega) na Mashbiki wakishuhudia, furahia na kuupa nafasi Mchezo umalizike ili Uwanja Utumike kwa Mkutano wa Dharura uliojitokeza na kulazimika kufanyika Asubuhi uwanja wa FFU Mbeya




Figure 5: Washiriki wa Tamasha La Mpaju Week 2019, siku ya kwanza wakihama Kutoka uwanja wa FFU kuelekea Uwanja wa Magereza. Uongozi wa Mpaju SC, kwa kipekee kabisa unamshukuru Mh Bashiru Madodi kwa msaada wake katika kuhakikisha tamasha linaendelea vema siku hii. Bila Kumsahau Kocha wa Ilemi Youth (Ruta Tiba) aliyekuwa bega kwa bega na Mpaju SC katika kuokoa tamasha hili

Figure 6: Vijana wa U-15 wa Ilemi Youth wakiwa katika picha ya Pamoja, kabla ya kuichapa Mpolo goli Tatu bila Majibu (0-3). Ni timu tishio sana.

Figure 7: Vijana wa Mpolo U-15 wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuchuana na Ilemi Youth

Figure 8: Super Eagle U-12, ( Ambao pia ni Mabingwa wa mashindano yaliyopita ya Mpaju Cup 2019) wakiwa katika picha ya Pamoja kabla ya kuwavaa Ferrari FC

Figure 9: Ferrari FC U-12 wakiwa katika Picha ya Pamoja kabla ya kupambana na Super Eagle

Figure 10: Super Eagle U-15 wakiwa katika picha ya Pamoja kabla ya kuwavaa ICON FC

Figure 11: ICON FC U-15,wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kupambana na Super Eagle



Figure 12: Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Mbeya Mjini  Mzee Gondwe akiongea na 
Baadhi ya Walimu na wachezaji waliohudhuria kuhitimisha siku ya ufunguzi

Figure 13: Mh.Bashiru Madodi, Mmoja wa Wadau wa Mpaju SC na Mzazi wa Mchezaji wa
Mpaju FC (Madodi Bashiru) akitoa nasaha kwa wadau waliohudhuria ufunguzi.
                                                                                            
Figure 14:Mpolo Shule Msingi (U15-Wasichana) Kushoto na Mpaju FC U-12 na Marefa wa
 Mchezo wakiwa Tayari kwa Mchezo Uwanja wa Magereza Mbeya


Figure 15: Mh.Naibu Spika, Dr.Tulia Ackson, Madodi Bashiru na Babu Bakhari ambao ni wachezaji wa Mpaju na wadau wa Mpaju Week 2019 (Kulia Kwake), baada ya maongezi ya karibu sana Pale Nyumbani Kwake na vijana wa Timu ya Wasichana ya Mpolo (Kushoto Kwake). Hakika ilikuwa siku nzuri sana kwa Mpaju SC na wadau wake.

                                                                                            


0 comments:

Post a Comment