Sunday, January 6, 2013

KISWAHILI MUHIMU SANA KWA UBORA WA ELIMU YA TANZANIA


WAZO LA  KIZALENDO!
CHEKECHEA NA MSINGI: UNG'ENGE TU, NAOMBA TUSILIJADILI KWA SASA.

 TUJADILI  HILI  KWANZA
kuanzia SEKONDARI MPAKA SHAHADA tutumie

" KISWAHILI ( KWANZA) & KIINGEREZA (PILI)
na   
MAOFISINI 

 KISWAHILI KIWE LAZIMA". 
LUGHA ZA KIGENI
RUKSA
Katika Kitabu hiki

'ARABIC LANGUAGE: ITS ROLE IN HISTORY, Kilichoandikwa na Anwar C Chejne, cha mwaka 1969.' (AU search- http://books.google.de/books/about/The_Arabic_Language.html'), unaweza kukutana na mambo mengi yanayohusiana na umuhimu wa Lugha yako (japo kitabu kinaelezea lugha ya Kiarabu), iwe Kikinga, Kichaga, Kihaya, Kinyakyusa, Kimakonde, Kinyiha, Kinyamwezi, Kiha, Kigogo, Kidigo, Kipemba, Lugha
yeyote unayoifahamu, ama KISWAHILI. Ila TANKI limevutiwa na mambo machache kuhusiana na suala la lugha

Language is a means of thought and instrumental to communication, a means of transmitting thoughts from ancestors to their offspring. A person who abandons his own language is an outsider to his social group, and alien to its thoughts. Language is the link between the world of bodies and the world of mind!

Kwanza, lugha ni nguzo ya mawasiliano na zaidi ni nguzo ya  kuwezesha FIKRA NA MAWAZO KUTOKA kwa MABABU kuwafikia mpaka WAJUKUU NA VITUKUU.
Yaani, lugha inaweza kutusaidia hata kufanya Upangaji wa mambo kwa muda mrefu kuwa mwepesi kwa sababu ni rahisi kuelewa fikra za waliokutangulia ambao tunaamini hata kama unajua zaidi yao, utahitaji mawazo yao kutokana na UZOEFU wao. HAKUNA MWALIMU MZURI KAMA UZOEFU.
 

Pili, MTU ANAYE IKANA/ASIYEIJUA LUGHA yake SI tu anakuwa MGENI KIMWILI bali hata KIFIKRA /KIMAWAZO katika JAMII yake. Hebu fikiria unaporudi nyumbani, halafu Bibi na Babu yako wanchoongea huwaelewi, utakuwa na tofauti gani na mgeni yeyote kutoka popote duniani? Na kwa mazingira hayo ya kutokuelewa lugha, unafikiri ni vipi Babu na Bibi wataweza kukupatia mtiririko wa Kifikra uliowafanya wafike hapo walipo, nawe ukaweza kuupata hasa? Ni vigumu.


Na tatu, MIILI YA WANAJAMII NA AKILI ZAO HUUNGASHWA NA LUGHA. Kama vile NAFSI/ROHO NA MWILI ni vitu ambavyo vikiachana tu, tunasema binadamu kafariki dunia, vivyo hivyo, WANAJAMII WANAHITAJI LUGHA ILI WAWE PAMOJA. Kama tunavyoambiwa na vitabu vya Dini kuwa Mungu aliwatawanya watu walioungana kutaka kwenda kumuona kwa kujenga mnara mrefu, kwa kuwapa lugha tofaouti. (Kipengere nimekisahau). HEBU FIKIRIA KUWA WABUNGE WETU WAWE WANAONGEA LUGHA TOFAUTI, UNAFIKIRI KUTAKUWA NA KINACHOENDELEA BUNGENI,KAMA JAMII? SIDHANI! LABDA!!PENGINE KWA UWEZO WA MUNGU!


Maana halisi ya Lugha sidhani kama ni muhimu sana, kikubwa kinachoongelwa hapa ni umuhimu wa kuwa na UELEWANO BAINA YA WATU WANAOWASILIANA,maana mbongo,kawaida yake ni kutafuta kubishana ili muda mwingi asifanye kazi! Mwalimu alitutaka tukimbie wakati wenzetu wanatembea, cha ajabu wakati wenzetu wanakimbia, sisi tunabishana nani awe mbele na kwa nini aanze yeye, ana nini, atalinga,………….!


Lugha inatakiwa afikishe ujumbe unaokusudiwa, IELEWEKE KUWA,KWA MUJIBU WA TANKI, HII NI ZAIDI YA MATAMSHI. NI PAMOJA NA HISIA NA SABABU ZINZOPATIKANA KUTOKANA NA KUONGEA LUGHA NA KUPELEKEA UELEWO BORA. Mfano, Baba na mtoto wanapoongea 


Familia ya kwanza

Baba : Mwanangu Hujambo?

Mtoto: Shwari Dingi Niaje?

Baba: Unasemaje? Toka Toka? Sitaki kukuona tena hapa?



Familia ya Pili

Baba : Mwanangu Hujambo?

Mtoto: Shwari Dingi! Niaje?

Baba: Ehe! Shwari, Vipi?Eh bwana nipe salamu yangu,hizo salamu zenu mi sizijui bado, hivyo     usizitumie kwangu mpaka zitakapotambulika,Sawa?

Mtoto: Mia Mzazi wangu! Shikamoo Baba! Samahani,nimejisahau! Unajua mtaani            kunatuharibu!

Baba: Na Kweli! Ukiruhusu, kweli kabisa utaharibikiwa? Hata hivyo, mimi pia huwa najifunza     kidogo kidogo, maana Mabadiliko hayakwepeki ila yawe na manufaa tu, sasa nyie ndio      mnakitupa kabisa Kiswahili fasaha,             haya tuachane na hayo……………!



Lugha inayoweza kutupeleka tunakotaka kwenda ni hiyo ya mzazi wa pili, Maana ina lengo la kutupatia mambo zaidi ya matatu  ambayo yamegusiwa leo! Hebu kumbuka unapoulizwa swali kwa lugha ya kigeni, halafu unaambiwa jibu hata kwa kutumia lugha yako! Furaha yake ilikuwaje?Kwa nini? Kwa hiyo lugha inaweza kukupa hata mori ya kusoma sana, kama vile ambavyo pengine wengine hawajapata elimu za juu tu kwa sababu walishindwa masomo kutokana na lugha ya kigeni. 


Jaribu kufikiria kuwa una mdeni wako, anakusumbua sana, halafu unatakiwa kumdai kwa lugha ya kigeni,unafikiri ni rahisi kuonyesha hisia zako kuliko unapotumia lugha yako? Pengine ukosefu wa lugha moja ulisumbua kuharakisha harakati za uhuru na kumfanya mwalimu kuona umuhimu wa kuwa na lugha moja ili kuharakisha maendeleo. Hivyo lugha inaweza hata kuongeza hamasa ya utaifa na maendeleo!


Fikiria kuwa unaingia ofisi ambayo wanatumia lugha ya kigeni na ile wanayotumia lugha yako,wapi utakuwa huru kuhoji, na kugundua mwenendo wa utendaji?Mashule yataongeza juhudi juu ya Kiswahili, na watanzania watapata ajira zaidi ndani ya nchi yao,na hivyo kuweza kutafsiri elimu yao katika mazingira yao, badala ya kuanza kuelezeana lugha kwanza halafu utekelezaji!Unajisikiaje kuongea na hakimu anayetumia Lugha Tofauti na wewe?Zimwi likujualo halikuli likakwisha, hata lugha ya mwenzio haiwezi kukubakisha! Unafikiri Mwe! Au Kaa! Kwa lugha ya kigeni ina uzito gani?   

Kumbuka Wimbo kama wa MAAZENGO! SHULE YETU TWAIPENDA SAANA, TWAITAKIA BAARAKA……..au ule wa shule yako! Fikiria ukiimbwa kwa lugha ya kigeni! Na pia mfikirie mtu anayekuja kukupa pole wakati wa majonzi, akitumia lugha ya kigeni na ile iliyo yako, unafikiri unapata hisia sawa? Ipi unajisikia vizuri zaidi? Lugha yako, KWA SABABU LUGHA INAGUSA MPAKA MIZIZI YA FIKRA, MOYO NA ROHO YAKO!


Na pengine ndio maana wengi tumesahau masomo tuliyosoma kwa lugha ya kigeni miaka mitano tu iliyopita,maana kukalili kulikuwa kwingi kuliko kuelewa hata kama ni historia inayonihusu mimi mwenyewe! Hakuna hisia ndani yake!

NAAMINI LUGHA YETU (KISWAHILI) PIA INA HIZI SIFA! SINA UHAKIKA KAMA TUNAKIPA UZITO! HASA KWENYE SHUGHULI ZOTE ZENYE UTAIFA KAMA ULINZI, MIKATABA MBALIMBALI, SERA, MITAZAMO, MIPANGO,……..! ZIANDIKWE KWA LUGHA YETU!

ANGALIZO: KWENYE MAONI YA KATIBA, TANKI LIMEPELEKA KIPANDE HIKI
 

"Kiswahili kama lugha ya taifa kiwe ndio lugha ya kwanza kisheria kufundishia kuanzia ngazi ya shule ya msingi , Sekondari  mpaka Shahada ya kwanza, ikifuatiwa na Kiengereza. Kiswahili kiwe lazima  katika ofisi zote, Taasisi,Makampuni na Kwenye shughuli za biashara  kitaifa. Kiingereza kiwe lugha ya pili.Hili ndio lengo, lakini kutokana na ukweli kuwa hatuishi peke yetu duniani, tunahitaji kuwa na upeo mzuri wa kuweza kushirikiana na wenzetu. Hivyo tunahitaji lugha zao pia, hivyo basi kwenye marekebisho ya ndani, mfumo wa elimu unaweza kuruhusu, Kiingereza kutumika chekechea na shule za msingi. Kwa sababu, watoto ni wa watanzania wote na ni muhimu wapata msingi wa lugha hizo, na ni vema sana mtoto akifundishwa lugha hiyo wakati nyumbani anaendelea kufahamu kuongea kiswahili,na darasani anafundishwa Kiswahili fasaha.Kifupi ni kuwa lazima tuwe na utaratibu mahususi wa kuhakikisha kiswahili kinapewa uzito na kuelweka kwa kila mtanzania. Sasa, hata kama ndio Dunia inaongozwa na Kiingereza, hata Civics,Historia yetu na Mengine hayawezi kufundishwa Kiswahili? Au basi hata kukifanya kuwa lazima kufundishwa Mpaka Shahada ya kwanza kama vile "Development Study" na "Communication Skills" kwa Mtanzania."SOMA ZAIDI MAONI YA KATIBA NA UBORESHE ZAIDI.

WAZO!
KAMA MSINGI TU

SHULE ZA SEKONDARI NA VYUONI,

LUGHA YA KISWAHILI (YA KWANZA) NA KIINGEREZA (YA PILI)

ZITUMIKE HATA ZOTE BASI

NA

MAOFISINI, KISWAHILI KIWE LAZIMA. LUGHA ZA KIGENI RUKSA PIA



MZALENDO UNASEMAJE?

4 comments:

  1. Kwa watanzania tulio wengi,Suluhisho la tatizo linapoonekana kuwa kubwa, huwa tunachagua kulizoea tatizo.

    Kuna shule ambazo nyimbo zao ziko katika lugha za kigeni, hapahapa tanzania. Kama sio kuzoea tatizo ni nini? Au ni tatizo kutokuwa tatizo tena?

    Labda hili si tatizo kabisa!, ni wasiwasi wako tu ndugu mtoa maada.

    ReplyDelete
  2. Hahahahahaha! Na mimi nimegundua, tumekwisha zoea tatizo,hivyo sio tatizo tena! hahahaha! Nashukuru sana! Lakini, Nafikiri ukweli ni kwamba bado tuna haki na wajibu wa kujaribu kuliondoa hili,japo kwa kutoa maoni yetu! Ukweli daima unadumu!

    ReplyDelete
  3. naomba mnieleweshe,kikwazo kiko wapi!kwanini siasa imekuwa kubwa kuliko vitendo,binafsi suala la lugha sioni tatizo sana kwenye kuwasilisha uelewa nnachokishangaa ni kuwa mfumo mzima wa utawala umeharibika sio LUGHA TU sekta zote,mbona kenya {swahili and english} safi,malawi (chewa and english},nigeria (hausa and english}egypt (english and arabIC}South africa zipo lugha zaidi ya nne na zote{ENGLISH,AFRICAAN,ZULU SAN KHOI ETC. zinatumika kwa makubaliano na mambo yanakwenda NARUDIA TENA MFUMO WETU WA UONGOZI NDIO TATIZO..LILA .RB,.!

    ReplyDelete
    Replies
    1. KWA MTAZAMO WAKO LILA, NI KWELI VIONGOZI NDIO TATIZO, kwa sababu wanajua na wanaambiwa, lakini UBINAFSI unawafanya wawe BUSY na milo zaidi ya UTAIFA wetu! Yaaani weacha tu! na katika hali ya kushangaza, wanapeleka watoto shule za KIINGEREZA, sasa waambie BORESHENI chekechea, zipige UNG'ENG'E basi ili wote TUPATE, ohh kikaenda kikarudi! Kilichobaki ni kukimbilia kuwa BEPARI BORA TU!!!!!!!!!!!!!

      Delete