Friday, September 5, 2014

Tatizo lako ndio ubinadamu wako,likubali,tatua na usonge?



Ukimchukulia mtoto mdogo kabisa anayezaliwa! Unaweza kusema hajui kitu na pengine ni sawa kusema hana Tatizo! Lakini ukijaribu kufikiria unaweza kuona kuwa tayari mtoto ana shida kama vile Njaa,baridi
ama joto na kadhalika! Haya ni yale ya kawaida, lakini yako pia ya Muumba ya kibaiolojia Zaidi. 

Kwangu mimi, Tatizo, ni hali ama jambo, mtu anahitaji kuishughulikia ili asonge mbele kimaisha kwa namna aonavyo atapata ubora Zaidi wa kimaisha, kwa kutumia rasimali asizoweza kuzipata kirahisi.Tatizo mara nyingi ni hali  tunayoiambatanisha na ugumu wa kutatua kinachotutatiza ama shida. Kwa msingi huo, mtoto pia ana shida za msingi, ambazo ndio ubinadamu wake, na mara nyingi huwa kuna suluhu kadhaa rahisi zisizotatiza, ama kutoka kwa mwenyezi mungu ama kutokana na asili, ukiongeza na utashi kiasi wa binadamu, hakuna tatizo kuzimudu shida/matatizo hayo. 

Sasa kwa nini tunayatafuta matatizo? Kwanza, ili kuweza kusonga mbele kama nilivyogusia kwenye maana. Pili huwa ni kwa ajili ya udhaifu tu wa kibanadamu, pengine kutojua kama shida aliyonayo ni ya msingi na muhimu kwake,matokeo yake anaboronga kuishughulikia na kuifanya ni tatizo, na nafikiri hapa ndio kwenye tatizo letu. Lakini, pia hulka, kama vile ubinafsi na ulafi. Hivi pia hupelekea mtu  kutaka apate kupindukia, pengine mpaka akaiba na kadhalika. Kwa hii sababu ya kwanza, kila mtu inabidi ama anaifanya kwa kukamilisha ubinadamu, maana nafikiri ni agizo la muumba. 

Yaani, unapaswa kuyasaka matatizo yako, kuyatatua, hata kama ni kwa kuomba msaada wa muumba, huko ndio kuishi. Inasemekana tulikwisha muuzi Muumba, hivyo akatoa kama adhabu, hivyo kama hatuna hizo shida hatupo duniani, na kuzilalamikia si sahihi, bali tunapaswa kuzifurahia, kwa sababmu Mungu anatupenda hawezi kutupatia sumu hata kama ni adhabu, ina lengo zuri. Shida ama Matatizo ya msingi ni Rasilimali kwa mtu makini.

Sasa, utakuta, hatushughuliki na matatizo ya msingi (hayo ya sababu ya kwanza), ambayo rasilimali kwa kiasi kikubwa tunazo, na tunaweza kuyatatua,na kwa kufanya hivyo tunakuwa tunasonga mbele, bila kupata tatizo. Badala yake huwa tunajikita kutaka mambo yawe makubwa kuliko rasilimali tulizonazo (hayo mengine, na yale ujuayo wewe). Hapo ndio kuyatafuta matatizo sasa niongeleako.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Itaendelea,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

0 comments:

Post a Comment