Sunday, December 11, 2016

Building Information Modeling (BIM) Tanzania

NANI ANAIHITAJI ZAIDI?

Mjadala wa Building Information Modeling ni miongoni mwa mijadala mikubwa kwa wakati huu kwenye sekta zinazohusu Majenzi Duniani kote.
Unaweza kuona mfululizo wa makongamano ya BIM Uingereza, ikiwemo lijalo la tarehe 21 Septemba 2017, (http://www.bimconference.co.uk/why-attend.php). Mwaka huu 2016 swala kuu lilikuwa kuongelea nadharia ya BIM, na hii ya mwaka kesho inaendeleza kuanzia hapo kwa kuonyesha jinsi utekelezaji na utumiaji wake katika uhalisia wa Majenzi. Ujerumani nao hawako nyuma. Wao wana juhudi mbalimbali na makongamano kama inavyoonyeshwa kwenye  kiungo hiki (https://www.bim-world.de/), ambapo Miaka miwili mfululizo sasa kongamano kubwa la BIM linafanywa,yaani kwa mwaka 2016 na 2017. Umuhimu wa BIM kwenye kuweka wazi taswira ya kazi za majenzi, ushirikiano baina ya wadau wa ujenzi na kuboresha utendaji wa kazi za majenzi umejadiliwa ikiwa ni pamoja na kujadili miongozo iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha utekelzaji wa BIM Ujerumani unafanikiwa.
 
Sio kwamba Tanzania haina habari kabisa kuhusu BIM, la hasha. Bali juhudi Zaidi zinahitajika ili kuifanya iwe kitu cha kawaida katika utendaji wa kila siku katika majenzi. Makongamano ya Bodi ya Wasanifu na Wakadiriaji majenzi yameshudia baadhi ya wataalamu wakisisitza umuhimu kuipa nafasi BIM katika seta yetu ya ujenzi nchini. Mfano ni mtaalamu kutoka nchi za kiscandinavia, ( Broberg, 2014), aliyetoa mtazamo wake katika kongamano la Uboreshaji Endelevu wa Utaalamu Continous Professional Development (CPD) lililofanyika mnamo tarehe 21-23 march Mbeya Tanzania. Mtaalamu huyo, alieleza kuwa matumizi ya BIM yamewanufaisha sana wao katika miradi yao ya ujenzi, kuanzia kupunguza gharama, ufanisi kwenye kudhibiti muda, kuongeza ubora na kuongeza ufanisi wao kama wataalamu wa usanifu wa ujenzi. 

Kwa mara ya kwanza unapoisikia BIM, unaweza kusema sio kitu cha kuweza kufanyika leo wala kesho kwa nchi kama Tanzania. Inakuwa kama ni dude Fulani kubwa sana linalohitaji mabilioni ya pesa na maandalizi ya kimasomo kwa hali ya juu. Wengi wa wataalamu wamesikika wakisema hiyo ni ya Ulaya, huku baaado sana. Hawa ni wale ambao hata kufanya kazi vizuri, pia huwa wanasema hiyo si kwa Tanzania, labda nchi za watu huko (Yaani Ulaya na kwingineko). Wapo pia ambao huwa wanajiuliza kuwa “Hii BIM hasa ni nini? Inaongeza nini kwenye mfumo wetu? Isijekuwa ni makompyuta tu.” Mimi napenda kuwa kwenye hili kundi. Lakini pia wapo wale ambao wanasema BIM ni kwa ajili ya Architects tu. Na Zaidi wapo ambao wanahisi BIM itaondoa umuhimu wa baadhi ya taalamu kama Quantity Surveying, ama ukadiriaji wa ujenzi. Mara kadhaa kumezuka fununu kuwa Utaalamu wa ukadiriaji utapungua umuhimu kwa kuwa kumeongezeka teknolojia ambayo inaonekana kuwa na uwezo wa kupiga hesabu automatiki. Hilo limekuwa pia gumzo kwa ujio wa BIM. Lakini kuna misemo mingi sana inaonyesha kuwa akili ya mwanadamu bado inastahili heshima Zaidi ya teknolojia. Mmojawapo wa misemo hiyo ni  “Computers are useless. They can only give you answers” Wa ― Pablo Picasso.Lakini kama haitoshi katika kitabu cha (Moran, 2015) imesisitizwa kuwa 

“Process plant design is an art, whose practitioners use science and mathematics, models and simulations, drawings and spreadsheets, but only to support their professional judgment. This judgment cannot be supplanted by these things, since people are smarter than computers (and probably always will be). Our imagination, mental imagery, intuition, analogies and metaphors, ability to negotiate and communicate with others, knowledge of custom and practice and of past disasters, personalities, and experience are what designers bring to the table.
If more people understood the total nature of design they would see the futility of attempts to replace skilled professional designers with technicians who punch numbers into computers. Any problem a computer can solve isn’t really a problem at all—the nontrivial problems of real-world design lie elsewhere.”

Kifupi ni kuwa Utaalamu wa mwanadamu una thamani kubwa kulinganisha na msaada wa teknolojia katika utatuzi wa matatizo ya kitaalamu kwa sababu mwanadamu  ana nafasi ya kujiuliza,kujifunza,kufikiri na hata kuomba msaada juu ya jambo analotaka kulitatua. Maamuzi yake yananafasi kubwa ya kuwa bora kuliko teknolojia yeyote. Hata BIM iwe na maendeleo ya kiteknolojia kwa kiasi kikubwa sio rahisi kuondoa umuhimu wa wakadiriaji,labda kama haukuwa Utaalamu halisi unaohitaji utashi wa mwanadamu. Hivyo mtaalamu hata uwe na kiasi gani cha teknolojia, tafadhali usidharau kusoma na kusikiliza kutoka kwa binadamu mwenzio. Hebu angalia na hiki kiungo (http://www.goodreads.com/quotes/tag/technology) kwa kuona maneno kama yafuatayo;

“Please, no matter how we advance technologically, please don't abandon the book. There is nothing in our material world more beautiful than the book."(Acceptance speech, National Book Award 2010 (Nonfiction), November 17, 2010)” Patti Smith

Japokuwa natamani kuongelea wadau wote wa majenzi, ila navutiwa Zaidi na kuanza na Architect Technologist, kwa sababu nina uhusiano nao binafsi na hivyo ningependa kushauri kuwa pengine wanapaswa kuipa nafasi ya kwanza BIM kwenye maisha yao ya kitaaluma. Wengine ni Architects, ambao mimi nawaita mabosi zangu kwa sababu kama mkadiriaji wa ujenzi nategemea kupata kazi nzuri kutoka kwao ili niweze kufurahia kazi yangu. Na pengine inaweza kuwa ni kuwapa heshima stahili kwa sababu katika ujenzi hasa wa majengo, Architects au Wasanifu huwa mara nyingi ni wataalamu wa mwanzo sana kuongea na mteja ili kujua hasa anahitaji nini. Na baadae wataalamu wengine huungana ili kukamilisha kile walichoanzisha kukishauri kuwa ndio kinamfaa mshitiri wa mradi huo. Na ukiangalia maandiko kadhaa kama la ((McGraw-Hill, 2010) na (Monko & Roider, 2014)) yanaonyesha kuwa pia Architects wanaonyesha kuwa katika hatua za mbele katika utumiaji wa BIM. Hivyo sio mbaya kuwapendelea na kuanza kuwaongelea kama ambavyo itakuwa sawa pia kuwalaumu pia pale tutakapoona Tanzania haisongi katika BIM wakati wao walianza kuijua mapema.

Architects Technologists (ATs) na Architects kwa Tanzania wakati fulani huniwia vigumu kuwatofautisha  wakati wa utendaji mtaani. Sitazigusa sana taalamu hizi kwa sababu ki ukweli sizijui kihivyo. Lakini Bodi kuwa moja naamini ni uchanga tu wa nchi ama muda bado wa kuzitenganisha,maana hata Wakadiriaji mpaka sasa wako bodi moja na Architects ama wasanifu. Sijui manufaa kama bado yapo ama ni uoga wa kujitegemea wa wakadiriaji (QS). Kwa hapa, ATs ni wale ambao kimsingi wanapaswa kubobea katika KUHAKIKISHA USANIFU UNAJENGEKE KWA UBORA NA UFANISI wa kisayansi na SAHIHI kwa mujibu wa taratibu,sharia na taaluma. Architects ama Wasanifu ni wale ambao wanapaswa kubobea kwenye KUHAKIKISHA UBUNIFU NA SANAA SAHIHI NA ENDELEVU KWA HITAJI LA MAJENZI VINAPATIKANA KULINGANA Mahaitaji ya MSHITIRI NA JAMII.

Ninachomaanisha, ni kuwa kwa nini TUNA SEBULE YA NJE nyumba nyingi za USWAHILINI PWANI, ni swali analojibu Architect. Lakini kama KISEBULE KIMEJENGWA kiasi cha kuleta  kiwango sahihi cha UPEPO MWANANA, ni swali ambalo Architect Technologist anapaswa kulijibu kwa uthabiti zaidi. Lakini pia kuna wale ambao wanapaswa kuona usiadizi wa wote hao katika kuhakikisha uchoraji na vifaa VYA KISEBULE uko TAYARI kama inavyotarajiwa KIUTARATIBU NA HATA KISHERIA, hapa wao ni ARCHITECT TECHNICIANS (ATTs). ATs ni wanasayansi wa Usanifu wakati As ni Wabunifu wa Usanifu. Wasanifu wanapaswa kuiona picha kubwa ya kwa nini Mradi wa Majenzi katika Jamii na uendelevu wa jamii hiyo, wakati ATs wao wanapaswa kuziona hali mbalimbali za uhalisia wa ujengekeji wa vipande vya mradi huo wa majenzi katika taratibu na sharia za jamii na taaluma. Wakati ATTs wao watapaswa kuiona na kuionyesha picha maalumu ya kipande cha mradi huo wa majenzi katika taratibu zake za kitaaluma na kuiwakilisha kama wanavyoelekezwa.

Ukiangalia maandiko mbalimbali, BIM ni uwakilishi wa kidijitali wa taarifa za majenzi na taswira ya majenzi kuanzia mwanzo mpaka mwisho unaowafanya wataalamu wote kuweza kufanya maamuzi sahihi.Kimsingi bado kuna debate kubwa juu ya hasa BIM ni nini. Ila mambo makuu ni pamoja na USHIRIKISHAJI WA WAHUSIKA WOTE WA MRADI,UWASILISHAJI WA TAARIFA NA MAELEZO YA MAJENZI KATI YA WAHUSIKA NA MTAZAMO WA MRADI WA MAJENZI KUANZIA USANIFU MPAKA UBOMOAJI NA PENGINE UJENZI MPYA. Haya ni kati ya mambo makuu ambayo BIM inayafanikisha. Japo ziada ni pamoja na uwepo wa MIFUMO THABITI YA KIDIJITALI ambayo, sio kama ilivyozoeleka. Kwenye BIM uwezo wa kiautomatiki ni mkubwa kwa kuwa vifaa na vipande vya majenzi vimehusishwa na tabia husishi na kuvifanya view tabia za kiakili. Mlango ukiondolewa,ukuta utarudi kuziba peng kwa sababu tayari uhusiano kati ya ukuta na mlango ulikwisha wekwa kuwa penye mlango ukuta haupo. Pia usanifu katika BIM unaanzia kwenye KITU CHENYE MIRABA MITATU (3D Objects). Hivyo Mradi wa majenzi ni muunganisho wa vipande mbalimbali vyenye tabia husianishi kama ilivyoelezwa. 

BIM is an acronym for Building Information Modelling. BIM describes the means by which everyone can understand a building through the use of a digital model which draws on a range of data assembled collaboratively, before during and after construction. Creating a digital Building Information Model enables those who interact with the building to optimize their actions, resulting in a greater whole life value for the asset. (https://www.thenbs.com/knowledge/what-is-building-information-modelling-bim)

Kwangu mimi, BIM NI UBUNIFU, UUNDAJI, UWAKILISHAJI na UONGOZI wa KIASI NA KIWANGO CHA MAELEZO CHA MAJENZI KATIKA MAISHA YA MRADI. Yaani, kwa kutumia mfano wa sebule la pwani ulioelezwa hapo juu BIM kiasi cha MAELEZO YA KISEBULE ambacho wataalamu wataweza kuunda, kuwakilisha na kuongoza kitakachoweza kuwapatia majibu yao KWA MAISHA YOTE YA MRADI.  Kwa kutazama maana zilizotolewa hapo juu za watalaamu BIM itawafaa wataalamu wote, yaani ATs,As na ATTs. BIM itawasadia ATs kujaribu na kuchunguza KIASI CHA UPEPO, IDADI YA WATU WANAOWEZA KUKAA na kadhalika KATIKA KISEBULE. BIM inatoa majibu ya majaribio mbalimbali ya MUUNDO WA SEBULE NA KIASI CHA UPEPO kinachopatikana. Architects wao BIM mbali na kuweza kuona kama Taswira yao iko sawa na anachofanya AT kupitia BIM, pia wanahitaji BIM kuona muunganiko wa UPEPO, SEBULE NA JAMII husika kwa ujumla. ATTs nadhani ndio kabisa BIM inaonekana jinsi inavyoweza kuwapatia vipimo vya SEBULE kwa shepu zote na kwa picha kamili ikiwa ni pamoja na vipimo vya mradi mzima. Lakini kikubwa kabisa katika BIM hapa ni kuwa wote hawa sio tu wataweza KUONGEA NA KUELEWANA WAO; bali sasa WATAWEZA KUWAHUSISHA WATAALAMU WENGINE KIRAHISI NA KIUFANISI MKUBWA KULIKO ZAMANI,kwa sababu KIMSINGI BIM inawafanya WAWEZE KUONGEA LUGHA MOJA (WAHUSIKA WA MRADI WANAPATA MAWASILIANO NA UELEWA SAHIHI WA MAELEZO YA MRADI NA KUWEZA KUCHANGIA KATIKA MAAMUZI KWA UFANISI NA UBORA SAHIHI), huku wakitofautiana hekima na busara YA MATAMSHI TU. Nadhani vitabu vya DINI vinalieleza hili vizuri kwa kusema wajengaji wa mnara wa babeli hawakuendelea kwa sababu walianza kuongea lugha tofauti.

Kwa ufupi kabisa ninachojaribu kukisema, ni kuwa TUNAHITAJI BIM kwa nafasi zetu za kitaalamu na kwa ujumla kama TIMU moja katika  mradi wa Majenzi. Kwa maisha ya SASA usiposhirikiana inawezekana ukawa unamaanisha hutaki kubaki katika soko. In a networked world, collaborate or perish  (Bratton & Tumin, 2012).Utandawazi unataka ushirikiano. Tuungane kuipokea na kuitathmini BIM maana haiondoki leo wala Kesho. Njia bora ya kupambana nayo ni kuamini IPO na ITAKUWEPO, hivyo kuifahamu na kujiandaa nayo kutatunusuru na madhara yake kuliko kuikwepa halafu ikatulazimu kuikubali kwa kulazimishwa na mazingira magumu wakati ukifika. Hili sio swala la mtaani tu, bali hata vyuoni, wataalamu waanze kuandaliwa kuifanya BIM kama sehemu ya maisha yao ya kila siku. Kama ambavyo tunashauriana kuifundisha Katiba mashuleni, tuifundishe BIM mavyuoni pia.
Taaluma kuweza kufanya vizuri kitaifa na kimataifa inahitaji utafiti na mazoezi. Taratibu na sera pia muhimu, lakini kuna ni vitu vinavyoweza kufuata kulingana na matumizi ya taaluma hiyo yanavyopanda chati. Bila kufundisha, kujadili na kutafiti hatuwezi kujua kama BIM ni nzuri kwetu ama mbaya na kibaya Zaidi hatutaweza kufahamu kuwa tufanye nini kunufaika ama kuikwepa. Kwa sasa BIM imeshaanza kufundishwa elimu za juu, maana yake si muda mrefu itafundishwa elimu ngazi za chini. Ushauri wangu ni wewe na mimi tuwe waalimu wa kwanza kwa kuijadili na kuifikiria pindi tunapofanya shughuli zetu za ujenzi. Ikumbukwe ujenzi ni sekta muhimu kwa taifa, hivyo inapobaki nyuma kiufanisi, maana yake taifa linasonga polepole kwa sababu sekta zingine pia zinadorora kwa kuwa nyingi zina uhusiano Fulani na Ujenzi.Sisemi maendeleo ni kujenga nyumba ama lah, bali nasema miundo mbinu ikikosa ubora endelevu, basi uchumi, afya,kazi, kuishi na kadhalika vinapungua ufanisi na hivyo kuathiri maendelo ya nchi kwa ujumla. Kwa utaratibu wetu tunaweza kujenga majumba, mabarabara na kila kitu, ila kwa kutumia BIM tunaweza kujenga JAMII ENDELEVU.

Architects Technologists, kama wanapaswa kuyabadili mawazo ya Architects ili yaweze kujengeka  kiufasaha,kisheria na “kisayansi”, basi BIM kama teknolojia inawahusu sana. Lakini kama ni ujumla wa taarifa inayotakiwa kuyabadili maelezo ya majenzi ili kutoa sio tu taswira ya wataalamu bali pia kuiboresha ili kuendana mahitaji endelevu ya jamii, Architects, Architects Technologists  na Architects Technicians hawana jinsi ya kuikwepa BIM. Lakini Zaidi kama BIM inamaanisha kuongeza UWEZEKANO WA KILA MSHIRIKI WA MAJENZI KUELEWA TAARIFA ZA MAJENZI NA KUSHIRIKI KWA UFASAHA KWENYE kutoa maamuzi juu ya MRADI, basi CLIENTS (WASHITIRI) wanapaswa KUIKIMBILIA BIM. Kama ilivyo kwa Architects, ni hivyo pia kwa designers wengine na hivyo pia wataalamu wengine. Swali la nani anaihitaji zaidi naomba kukuachia msomaji.


0 comments:

Post a Comment