Friday, September 6, 2024

MPAJU FC ATINISU BINGWA-KAKAYE NDONDO CUP 2024

 MPAJU QUEENS 

YAVURUGA SHEREHE YA ICON QUEENS

YAWACHAPA WATANI WAO 2-1.

Mchezaji wa Mpaju FC (Kukaye Ndondo Cup) Halima Moses(Kushoto) , ndiye aliyekuwa Mwiba Mchungu kwa ICON Queens, baada ya kuwabugiza goli zote mbili.  Ana kasi na ni makini sana katika ufungaji. Hakika alistahili zawadi.


Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake Mkoa wa Mbeya Dada Mwaipopo, akiongea na kuwaasa mambo kadhaa wachezaji wa Mpira wa Miguu kwa wanawake Mbeya. Hakika Kukaye Ndondo Cup imefanya kazi kubwa sana.

ICON QUEENS BAADA YA KUKUBALI KICHAPO CHA 2-1, WAMEELEWA MAANA YA MSEMO "UHOLO SAGUMALIHA LAKINI UBAYA UBWELA"

KUNA MAMBO YA KUFURAHI KUKAYE NDONDO CUP
1. Inahusisha wachezaji Mbalimbali kutoka  timu za mikoa yote Tanzania. Pia wachezaji wakubwa wanaoshiriki ligi mbalimbali Duniani. Hii ilipelekea watu kuibatiza jina UEFA ALLSTARS  timu ya Mpaju FC ATINISU. Wachezaji toka timu kama Mapinduzi Queens na Kyela Queens walikuwepo na kuayfanya mashindano kuwa ya kuvitia sana.
2. Kuna UTANI MKALI SANA baina ya timu mbili (Mpaju Queens vs ICON Queens). Hizi ni timu mbili zinazotokana na Vituo vy akulelea wachezaji wa U23 had U9. Vituo hivi vimekuwa pia chachu kubwa kwa soka hili la wanawake hapa Mbeya. Utani huu ulikuwa hamasa nzuri na ya kuvutia.
3. Sio kwa uzito, ni Uwepo wa timu ya Prisons Queens. Prisons Queens, ni timu itokanayo na Taasisi kongwe katika mambo ya Mpirs wa miguu nchini Tanzania, na Mbeya. Lakini pia, kwa sasa Prisons Queens pengine ndio wakawa wawakilishi wa Mkoa wa Mbeya katika jitihada za kupata Timu ya Wanawake ya Premier League. Kukaye Ndondo Cup, kwao ilikuwa sehemu ya kuangalia wachezaji na kujipima juu ya maandalizi hayo. Kitu kizuri, ilikuwa ni ushiriki wa Prisons Queens wa hali ya juu ikiwa ni pamoja kuhakikisha vifaa vya matibabu na watabibu wanaongezeka na kuhakikisha usalama wa mabinti zetu uwanjani. Hii iliyapa mashindaano hadhi ya juu na ya tofauti sana. Tunatamani kuwaona Mbeya City na Ken Gold  Mwakani wakifanya hivi pia.
4. Mazuri ni Mengi kwa kweli, Wasimamizi wa sheria na ushirikishwaji katika maamuzi mbalimbali. Oia Mgawanyo wa zawadi ulikuwa mkubwa,ikiwa ni nzuri kwa kukuza mpira. 

CHANGAMOTO NA MAPUNGUFU HAYAKOSI
1. Ni kubadilika badilika kwa ratiba. Hili ni tatizo kwa kweli. Tunatamani kuona Uongozi wa Kukaye Ndondo Cup wakilifanyia kazi. Ratiba ni muhimu, ili kwenda na muda na kupunguza gharama za uendeshaji
2.  Udhamini, kutowafikia timu shiriki kwa kiasi kukubwa. Tumeona timu moja tu ikiwa na jezi yenye nembo ya Kukaye Ndondo Cup. Tunaamini inawezekana timu zote zikapata jezi siku za usoni. 
3. Timu kukosa nidhamu. Kuna umuhimu wa kuhakikisha timu shiriki ziwe na uongozi unaoweza kuwajibika, ili kupunguza utovu wa nidhamu.
4. Takwimu na Matokeo kutotolewa kwa wakati. Ulimwengu wa sasa ni wa taarifa. Taarifa za matokeo na picha ni muhimu sana, kuchelewesha kunapelekea kupunguza ufanisis katika taasisi shiriki. kutokana na hili, hata baadhi ya zawadi zinakosa weledi sahihi, mfano mfungaji bora alitajwa bila idadi ya magoli aliyofunga.



0 comments:

Post a Comment