Sunday, September 24, 2023

MPAJU FC QUEENS (ATINISU) WACHEZA NA KUSHINDA KAMA MABINGWA HALISI WA MKOA WA MBEYA

WAWAFUNGA WATANI WAO ICON FC KWA MABAO 2 BILA MAJIBU
(JANET NA MARIAM WAINYANYASA ICON KAYA MAGOLI SAAAAFI YA HARAKA) 
Mpaju FC Atinisu Washika nafasi ya Pili huku WAZAWA a.k.a Wakulungwa wakiwa MABINGWA Mashindano ya kihistoria ya KUKAYE MOTO WOMEN NDONDO CUP MBEYA 2023.

Mpaju Atinisu wakiwa na Mwalimu wao David Saimon uwanja wa Mwenge Mbeya. 

Kabla ya Mchezo mmoja wa Wakurugenzi wa S-and-C Technology Ltd (Eng Mashalla Masha) ,Vijana wanaotamba na APP ya LEOLEO kwa habari zote za KILIMO nchini, alikabidhi Maji ya Kunywa kama sehemu ya msaada kwa Mpaju FC. Mpaju FC inashukuru uongozi kwa moyo huu.

Merry a.k.a Luís Jose Miquissone akikabidhiwa Jezi Kama sehemu ya zawadi ya uwakilishi kwa wachezaji wakongwe kama Maria na Thabitha kwa utumishi wao katika timu ya Mpaju FC Queens. Hakika Mpaju FC daima itatambua mchango wenu katika mafanikio ya taasisi hii. Tujikumbushe kupitia kiungo hiki  LIGI YA MPIRA WA MIGUU KWA WANAWAKE- MKOA WA MBEYA ~ Mpaju Sport Centre  

Msisitizo , 'Kushinda Mechi yetu dhidi ya ICON kwa wasichana huwa ni zaidi ya Ubingwa, ICON ni Vinara wa Mchezo huu hapa Mbeya Jijini na hivyo sisi Mpaju FC Atinisu ni lazima tufanye jitihada ya kuwafikia ICON kwanza kabla ya kufikia ubora wa kitaifa, na kama kweli tunahitaji kuonyesha kuwa ni mabingwa halisi wa Mkoa 2022-23 na wawakilishi wa Mkoa katika Mashindano yajayo ya DARAJA LA KWANZA 2023-24, inabidi tusiruhusu hizi goli mbili zirudi'. 

Mashabiki wakiburudika wakati wa mapumziko. Vijana wadogo kabisa walionyesha uwezo wa hali ya juu wa kuimba na kucheza. Hakika BURAHANI INA MAMLAKA

Kocha wa Mpaju FC Queens akinywa Maji kwa Utulivu Baada ya kumaliza mashindano salama na kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Kukaye Ndondo Cup.

0 comments:

Post a Comment