Tuesday, March 2, 2021

LIGI YA MPIRA WA MIGUU KWA WANAWAKE- MKOA WA MBEYA


MPAJU FC (a.k.a ATINISU) 

WAANZA KWA KUKUBALI KIPIGO CHA MAGOLI 9 KWA 1 

Tarehe 01 Machi 2021 kulifanyika tukio la kihistoria kwa wanasoka wa Mkoa wa Mbeya. Ligi ya Mkoa kwa Mpira wa Miguu wa Wanawake ilianza rasmi ili kutafuta Bingwa atayeuwakilisha Mkoa katika kusaka tiketi a kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Ikumbukwe sio siku nyingi tokea kituo cha Michezo cha Mpaju yaani Mpaju Sports Centre kifanye tamasha la Mpaju Week 2020 ambalo lilikuwa na lengo la kuhamasisha mpira wa wasichana mkoani Mbeya. (Fuatilia kiungo:  http://mpaju.blogspot.com/2020/12/mpaju-week-2020-yawa-chachu-kwa-soka-la.html). Ligi hii

inatarajiwa kufanyika kwa kipindi chote cha wiki mbili yaani  tarehe 01-15 Machi 2021. Usikubali kukosa. 

Pamoja na kuanza na kichapo, ATINISU walionekana kupambana kwa hali na mali kiasi cha kuwafanya ICON FC ambao walidhamiria kupata ushindi mnono na mkubwa ili waweze kujihakikishia uwingi wa magoli kabla ya kukutana na wapinzani wao wakali wa Tukuyu Queens siku chache zijazo kushindwa kufanikisha dhamira hiyo. Kukosekana kwa Stamina na uzoefu ndio vikwazo vikubwa vilivyosababisha ATINISU washindwe kuzitumia Mbinu nyingi na kali kutoka kwa mwalimu wao Ali Mkumbukwa. Mpaju SC inapenda kuwashukuru viongozi wa mpira Wilaya na Mkoa kwa kuwa wenye kusikiliza na kuweza kutuletea ligi hii. Bila kusahau, shukurani nyingi sana ziwaende wadau woote ambao wamekuwa bega kwa bega katika kuhakikisha Mpaju SC inafanikisha jitihada mbalimbali kama kuendesha matamasha na mashindano muhimu katika kuendeleza mpira wetu Mbeya. Hongera sana ICON FC kwa ushindi, na ni matumaini yetu kuwa mtaongeza jitihada ili kuweza kufika mbali zaidi katika malengo yenu na Hongera sana ATINISU pia kwa hatua kubwa mliyofikia. Picha zinaeleza zaidi juu ya mtanange huu.

Viongozi wakikagua Timu Kabla ya Kuanza Mchezo (Orange-Mpaju FC na ICON FC)


Makepteni wakiwa na waamuzi Binti Hatari Mnooo kutoka Mpaju FC (Maria Steven Kakwale)

Walimu wakifurahia mchezo kuisha salama kutoka Kushoto ni Denis Songela (ICON), Ali Mkumbukwa (Mpaju FC) na Mussa Noah Ujinu (ICON)

Mpaju FC wakiwa na Mmoja wa viongozi wa Soka la Wasichana (a.k.a Dada Rose)


Kama Picha inavyojieleza, Thabita Mbali,Golikipa machachari sana na aliyekuwa kivutio kikubwa.

 

0 comments:

Post a Comment