MPAJU ATINISU WATISHA SANA
WAWACHABANGA TUKUYU QUEENS
NA KUSHIKA NAFASI YA TATU
Siku ya Jumapili ya tarehe 07 Machi 2021, historia iliendelea kuandikwa kwa Mkoa wa Mbeya na kituo cha michezo cha Mpaju Sports Centre. Haikuwa siku ya kuhitimisha Ligi ya Mpira wa Miguu ya wanawake hapa Mbeya, bali ilikuwa siku ya furaha sana kwa vijana wa MPAJU ATINISU yaani wasichana na wanawake wapambanaji wa Mpaju FC baada ya kupambana sana na kuhakikisha wanaondoka na ushindi mnono wa goli 2-0 dhidi ya timu ngumu na yenye uzoefu ya Tukuyu Queens
kutoka Wilaya ya Rungwe. magoli muhimu ya Mpaju FC Atinisu yalipachikwa na Jack ambaye aliwatoroka mabeki wa tukuyu kiustadi na kwa mbio kali na kuachia shuti lilimuacha mlinda lango akishangaa tu. La pili lilifungwa na Merry ambaye wengi walimwita MORRISON wakimaanisha amefanya mengi kwenye mashindano haya kama ambavyo mchezaji wa simba Sports Club (Luis Miquissone) alivyofanya michezo ya klabu bingwa Afrika. Picha zinaelezea mengi
|
KIKOSI CHA MPAJU ATINISU KILICHOLETA USHINDI NA KUSHIKA NAFASI YA TATU |
|
KEPTENI MARIA NA WACHEZAJI WA MPAJU ATINSU WAKIWA NA BAADHI YA WACHEZAJI WA MPAJU U-17 KATIKA PICHA BAADA YA USHINDI |
|
MPAJU ATINISU WAKISUBIRI ZAWADI |
|
KOCHA ALI MKUMBUKWA NA WACHEZAJI WA NA BAADHI YA MPAJU ATINSU KATIKA PICHA BAADA YA USHINDI |
|
VIONGOZI MKOA NA MGENI RASMI KATIKA UTARATIBU WA KUFUNGA MASHINDANO |
|
VIONGOZI WAKITOA ZAWADI WA TIMU NA WACHEZAJI MBALIMBALI |
|
MGENI RASMI (MKURUGENZI WA TIMU KEN-GOLD YA CHUNYA) AKIMKABIDHI KEPTENI WA MPAJU ATINISU MARIA STEVEN KAKWALE KITITA CHA PESA KAMA ZAWADI YA KUWA USHINDI WA TATU |
|
MPAJU ATINISU WAKISHANGILIA ZAWADI |
0 comments:
Post a Comment