WAZO LA KIZALENDO!
CHEKECHEA NA MSINGI: UNG'ENGE TU, NAOMBA TUSILIJADILI KWA SASA.
TUJADILI HILI KWANZA
CHEKECHEA NA MSINGI: UNG'ENGE TU, NAOMBA TUSILIJADILI KWA SASA.
TUJADILI HILI KWANZA
" KISWAHILI ( KWANZA) & KIINGEREZA (PILI)
na
MAOFISINI
na
MAOFISINI
KISWAHILI KIWE LAZIMA".
LUGHA ZA KIGENI
RUKSA
LUGHA ZA KIGENI
RUKSA
Katika Kitabu hiki
'ARABIC
LANGUAGE: ITS ROLE IN HISTORY, Kilichoandikwa na Anwar C Chejne, cha mwaka 1969.' (AU
search- http://books.google.de/books/about/The_Arabic_Language.html'), unaweza
kukutana na mambo mengi yanayohusiana na umuhimu wa Lugha yako (japo kitabu kinaelezea lugha ya Kiarabu), iwe Kikinga,
Kichaga, Kihaya, Kinyakyusa, Kimakonde, Kinyiha, Kinyamwezi, Kiha, Kigogo, Kidigo,
Kipemba, Lugha
yeyote unayoifahamu, ama KISWAHILI. Ila TANKI limevutiwa na mambo machache kuhusiana na suala la lugha
yeyote unayoifahamu, ama KISWAHILI. Ila TANKI limevutiwa na mambo machache kuhusiana na suala la lugha
Language
is a means of thought and instrumental to
communication, a means of transmitting thoughts from ancestors to their offspring.
A person who abandons his own language is an outsider to his social group, and alien to its thoughts. Language is the link between the world of bodies and the world
of mind!
Kwanza, lugha ni nguzo ya mawasiliano na zaidi ni nguzo ya kuwezesha FIKRA
NA MAWAZO KUTOKA kwa MABABU kuwafikia mpaka WAJUKUU NA VITUKUU.
Yaani, lugha inaweza kutusaidia hata kufanya Upangaji wa mambo kwa muda mrefu kuwa mwepesi kwa sababu ni rahisi kuelewa fikra za waliokutangulia ambao tunaamini hata kama unajua zaidi yao, utahitaji mawazo yao kutokana na UZOEFU wao. HAKUNA MWALIMU MZURI KAMA UZOEFU.
Yaani, lugha inaweza kutusaidia hata kufanya Upangaji wa mambo kwa muda mrefu kuwa mwepesi kwa sababu ni rahisi kuelewa fikra za waliokutangulia ambao tunaamini hata kama unajua zaidi yao, utahitaji mawazo yao kutokana na UZOEFU wao. HAKUNA MWALIMU MZURI KAMA UZOEFU.
Pili, MTU ANAYE IKANA/ASIYEIJUA LUGHA
yake SI tu anakuwa MGENI KIMWILI bali hata KIFIKRA /KIMAWAZO katika JAMII yake.
Hebu fikiria unaporudi nyumbani, halafu Bibi na Babu yako wanchoongea
huwaelewi, utakuwa na tofauti gani na mgeni yeyote kutoka popote duniani? Na kwa
mazingira hayo ya kutokuelewa lugha, unafikiri ni vipi Babu na Bibi wataweza kukupatia
mtiririko wa Kifikra uliowafanya wafike hapo walipo, nawe ukaweza kuupata hasa?
Ni vigumu.
Na tatu, MIILI YA WANAJAMII NA AKILI ZAO
HUUNGASHWA NA LUGHA. Kama vile NAFSI/ROHO NA MWILI ni vitu ambavyo vikiachana
tu, tunasema binadamu kafariki dunia, vivyo hivyo, WANAJAMII WANAHITAJI LUGHA
ILI WAWE PAMOJA. Kama tunavyoambiwa na vitabu vya Dini kuwa Mungu aliwatawanya watu
walioungana kutaka kwenda kumuona kwa kujenga mnara mrefu, kwa kuwapa lugha
tofaouti. (Kipengere nimekisahau). HEBU FIKIRIA KUWA WABUNGE WETU WAWE
WANAONGEA LUGHA TOFAUTI, UNAFIKIRI KUTAKUWA NA KINACHOENDELEA BUNGENI,KAMA
JAMII? SIDHANI! LABDA!!PENGINE KWA UWEZO WA MUNGU!
Maana halisi ya Lugha
sidhani kama ni muhimu sana, kikubwa kinachoongelwa hapa ni umuhimu wa kuwa na
UELEWANO BAINA YA WATU WANAOWASILIANA,maana mbongo,kawaida yake ni kutafuta kubishana ili muda
mwingi asifanye kazi! Mwalimu alitutaka
tukimbie wakati wenzetu wanatembea,
cha ajabu wakati wenzetu wanakimbia,
sisi tunabishana nani awe mbele na kwa nini aanze yeye, ana nini, atalinga,………….!
Lugha inatakiwa afikishe ujumbe unaokusudiwa, IELEWEKE KUWA,KWA
MUJIBU WA TANKI, HII NI ZAIDI YA MATAMSHI. NI PAMOJA NA HISIA NA SABABU
ZINZOPATIKANA KUTOKANA NA KUONGEA LUGHA NA KUPELEKEA UELEWO BORA. Mfano, Baba
na mtoto wanapoongea
Familia ya kwanza
Baba : Mwanangu Hujambo?
Mtoto: Shwari Dingi Niaje?
Baba: Unasemaje? Toka Toka? Sitaki kukuona tena hapa?
Familia ya Pili
Baba : Mwanangu Hujambo?
Mtoto: Shwari Dingi! Niaje?
Baba: Ehe! Shwari, Vipi?Eh bwana nipe salamu yangu,hizo
salamu zenu mi sizijui bado, hivyo usizitumie
kwangu mpaka zitakapotambulika,Sawa?
Mtoto: Mia Mzazi
wangu! Shikamoo Baba! Samahani,nimejisahau! Unajua mtaani kunatuharibu!
Baba: Na Kweli! Ukiruhusu, kweli kabisa utaharibikiwa? Hata
hivyo, mimi pia huwa najifunza kidogo kidogo,
maana Mabadiliko hayakwepeki ila
yawe na manufaa tu, sasa nyie ndio mnakitupa
kabisa Kiswahili fasaha, haya
tuachane na hayo……………!
Lugha
inayoweza kutupeleka tunakotaka kwenda ni hiyo ya mzazi wa pili, Maana ina lengo
la kutupatia mambo zaidi ya matatu ambayo yamegusiwa leo! Hebu kumbuka unapoulizwa swali kwa lugha ya
kigeni, halafu unaambiwa jibu hata kwa kutumia lugha yako! Furaha yake ilikuwaje?Kwa
nini? Kwa
hiyo lugha inaweza kukupa hata mori ya kusoma sana, kama vile ambavyo pengine
wengine hawajapata elimu za juu tu kwa sababu walishindwa masomo kutokana na lugha
ya kigeni.
Jaribu kufikiria kuwa una mdeni
wako, anakusumbua sana, halafu unatakiwa kumdai kwa lugha ya kigeni,unafikiri
ni rahisi kuonyesha hisia zako kuliko unapotumia lugha yako? Pengine ukosefu wa
lugha moja ulisumbua kuharakisha harakati za uhuru na kumfanya mwalimu kuona
umuhimu wa kuwa na lugha moja ili kuharakisha maendeleo. Hivyo lugha inaweza
hata kuongeza hamasa ya utaifa na maendeleo!
Fikiria kuwa unaingia ofisi ambayo
wanatumia lugha ya kigeni na ile wanayotumia lugha yako,wapi utakuwa huru
kuhoji, na kugundua mwenendo wa utendaji?Mashule yataongeza juhudi juu ya Kiswahili,
na watanzania watapata ajira zaidi ndani ya nchi yao,na hivyo kuweza kutafsiri
elimu yao katika mazingira yao, badala ya kuanza kuelezeana lugha kwanza halafu
utekelezaji!Unajisikiaje kuongea na hakimu anayetumia Lugha Tofauti na
wewe?Zimwi likujualo halikuli likakwisha, hata lugha ya mwenzio haiwezi
kukubakisha! Unafikiri Mwe! Au Kaa! Kwa lugha ya kigeni ina uzito gani?
Kumbuka Wimbo kama wa MAAZENGO! SHULE
YETU TWAIPENDA SAANA, TWAITAKIA BAARAKA……..au ule wa shule yako! Fikiria ukiimbwa
kwa lugha ya kigeni! Na pia mfikirie mtu anayekuja kukupa pole wakati wa
majonzi, akitumia lugha ya kigeni na ile iliyo yako, unafikiri unapata hisia
sawa? Ipi unajisikia vizuri zaidi? Lugha yako, KWA SABABU LUGHA INAGUSA MPAKA
MIZIZI YA FIKRA, MOYO NA ROHO YAKO!
Na pengine ndio maana wengi
tumesahau masomo tuliyosoma kwa lugha ya kigeni miaka mitano tu iliyopita,maana
kukalili kulikuwa kwingi kuliko kuelewa hata kama ni historia inayonihusu mimi
mwenyewe! Hakuna hisia ndani yake!
NAAMINI LUGHA YETU (KISWAHILI) PIA INA
HIZI SIFA! SINA UHAKIKA KAMA TUNAKIPA UZITO! HASA KWENYE SHUGHULI ZOTE ZENYE
UTAIFA KAMA ULINZI, MIKATABA MBALIMBALI, SERA, MITAZAMO, MIPANGO,……..! ZIANDIKWE
KWA LUGHA YETU!
ANGALIZO: KWENYE MAONI YA KATIBA, TANKI LIMEPELEKA KIPANDE HIKI
ANGALIZO: KWENYE MAONI YA KATIBA, TANKI LIMEPELEKA KIPANDE HIKI
"Kiswahili kama lugha ya taifa kiwe ndio lugha ya kwanza kisheria
kufundishia kuanzia ngazi ya shule ya msingi , Sekondari mpaka Shahada ya kwanza, ikifuatiwa na
Kiengereza. Kiswahili kiwe lazima katika
ofisi zote, Taasisi,Makampuni na Kwenye shughuli za biashara kitaifa.
Kiingereza kiwe lugha ya pili.Hili ndio lengo, lakini kutokana na
ukweli kuwa hatuishi peke yetu duniani, tunahitaji kuwa na upeo mzuri wa
kuweza kushirikiana na wenzetu. Hivyo tunahitaji lugha zao pia, hivyo
basi kwenye marekebisho ya ndani, mfumo wa elimu unaweza kuruhusu,
Kiingereza kutumika chekechea na shule za msingi. Kwa sababu, watoto ni
wa watanzania wote na ni muhimu wapata msingi wa lugha hizo, na ni vema
sana mtoto akifundishwa lugha hiyo wakati nyumbani anaendelea kufahamu
kuongea kiswahili,na darasani anafundishwa Kiswahili fasaha.Kifupi ni
kuwa lazima tuwe na utaratibu mahususi wa kuhakikisha kiswahili kinapewa
uzito na kuelweka kwa kila mtanzania. Sasa, hata kama ndio Dunia
inaongozwa na Kiingereza, hata Civics,Historia yetu na Mengine hayawezi
kufundishwa Kiswahili? Au basi hata kukifanya kuwa lazima kufundishwa
Mpaka Shahada ya kwanza kama vile "Development Study" na "Communication
Skills" kwa Mtanzania."SOMA ZAIDI MAONI YA KATIBA NA UBORESHE ZAIDI.
WAZO!
KAMA MSINGI TU
KAMA MSINGI TU
SHULE ZA SEKONDARI NA VYUONI,
LUGHA YA KISWAHILI (YA KWANZA) NA
KIINGEREZA (YA PILI)
ZITUMIKE HATA ZOTE BASI
NA
MAOFISINI, KISWAHILI KIWE LAZIMA.
LUGHA ZA KIGENI RUKSA PIA
MZALENDO UNASEMAJE?
Kwa watanzania tulio wengi,Suluhisho la tatizo linapoonekana kuwa kubwa, huwa tunachagua kulizoea tatizo.
ReplyDeleteKuna shule ambazo nyimbo zao ziko katika lugha za kigeni, hapahapa tanzania. Kama sio kuzoea tatizo ni nini? Au ni tatizo kutokuwa tatizo tena?
Labda hili si tatizo kabisa!, ni wasiwasi wako tu ndugu mtoa maada.
Hahahahahaha! Na mimi nimegundua, tumekwisha zoea tatizo,hivyo sio tatizo tena! hahahaha! Nashukuru sana! Lakini, Nafikiri ukweli ni kwamba bado tuna haki na wajibu wa kujaribu kuliondoa hili,japo kwa kutoa maoni yetu! Ukweli daima unadumu!
ReplyDeletenaomba mnieleweshe,kikwazo kiko wapi!kwanini siasa imekuwa kubwa kuliko vitendo,binafsi suala la lugha sioni tatizo sana kwenye kuwasilisha uelewa nnachokishangaa ni kuwa mfumo mzima wa utawala umeharibika sio LUGHA TU sekta zote,mbona kenya {swahili and english} safi,malawi (chewa and english},nigeria (hausa and english}egypt (english and arabIC}South africa zipo lugha zaidi ya nne na zote{ENGLISH,AFRICAAN,ZULU SAN KHOI ETC. zinatumika kwa makubaliano na mambo yanakwenda NARUDIA TENA MFUMO WETU WA UONGOZI NDIO TATIZO..LILA .RB,.!
ReplyDeleteKWA MTAZAMO WAKO LILA, NI KWELI VIONGOZI NDIO TATIZO, kwa sababu wanajua na wanaambiwa, lakini UBINAFSI unawafanya wawe BUSY na milo zaidi ya UTAIFA wetu! Yaaani weacha tu! na katika hali ya kushangaza, wanapeleka watoto shule za KIINGEREZA, sasa waambie BORESHENI chekechea, zipige UNG'ENG'E basi ili wote TUPATE, ohh kikaenda kikarudi! Kilichobaki ni kukimbilia kuwa BEPARI BORA TU!!!!!!!!!!!!!
Delete