“MPAJU SPORTS CENTRE ILIUWASHA MOTO KAMA WOOOTE, NDANI YA UWANJA WA SOKOINE"
Siku hii ya tarehe 31 Disemba 2019, itakumbukwa daima na
wadau wote wa Mpaju Sports Centre. Hakika ilikuwa siku ya furaha na siku ambayo
iliweka msingi mkubwa wa mafanikio ya kituo hiki cha michezo kilichopo Mbeya
eneo la Iganzo.
Siku ilianza kwa timu mbalimbali zenye vijana wa rika
tofauti kuanzia chini ya miaka 9 mpaka juu ya miaka 22, kujikusanya katika
uwanja wa Sokoine.Vijana wa Mpaju FC U-10 walianza siku mnamo mida ya saa mbili asubuhi kwa kupambana na kaka na watani wao wa Mpaju U-12. Hili pambano la uzinduzi lilishuhudia uwezo wa hali ya juu wa kumiliki Mpira wa Mh. Bashiru Madodi ambaye mbali ya Kuwa mchezaji wa Mpaju Veterans, pia ni Mmoja wa wa Wadau wakubwa wa Mpaju Sports Centre, ambaye alifanya jitihada kuhakikisha walau tamasha hili linafanyika uwanja wa Sokoine. Kwa mshangao wa wengi, tamasha hili liliwahusisha vijana wa
kike wanaosakata soka kutoka Mbalali.
|
Wachezaji wa Timu Mbalimbali wakiwasili Uwanja wa Sokoine |
|
Mh Bashiru Madodi akimiliki mpira kuashiria kuanza kwa tamasha la Mpaju Day |
|
Timu ya Mpaju FC U-10 (Jezi Nyekundu) na U-12 (Njano) wakiwa chini ya Mwalimu wao Rajabu Ndelele (Kulia). Mchezaji wa Katikati ndio Renard Christopher, ambaye aliibuka Kiungo Bora wa Mpaju FC na MwanaMpaju wa Mwaka. |
|
Mwalimu Nsyani, akiwa na wachezaji wa Mbalali, Wenye jezi za Bluu ni timu ya Wasichana iliyosakata soka safi siku hiyo |
Baada ya michezo ya ufunguzi, kulifuatiwa na michezo kadhaa ya vijana wenye umri zaidi ya miaka 12, kutoka timu maarufu hapa jiji mbeya. Timu hizo ni Mbeya Youth Academy, Mbalizi Academy,Ilemi Academy,Mtoni Junior, ICON Academy na zingine kadhaa ambazo kwa mujibu wa ratiba hazikualikwa.
Kwa kifupi timu zilionyesha mpira mzuri, hasa Mbalizi,Ilemi na Mbeya Youth Academy kwa vijana wa chini ya miaka 15 na 17. Mpaju FC hawakuwa nyuma kwa kuweza kupata sulhu mbili katika michezo yake huku Mbalizi na Ilemi wakiondoka timu pekee ambazo hazikupoteza mchezo.
Tamasha lilifungwa kwa mchezo mzuri wa Mpaju Veterans na Mpaju FC Combine. Mchezo huo ulishuhudia walezi, wadau na wachezaji wa Mpaju FC waliovuka umri wa miaka 18, wakiwemo walimu wa Mpaju FC, wakionyesha burudani nzuri akbisa ya mpira na kuibuka na ushindi wa magoli 3-1. Pia Mbali na uwepo wa maandazi na juisi na glucose kwa ajili ya timu zote, tamasha lilikamilishwa kwa zawadi kadha kama vile MwanaMpaju FC wa mwaka ambaye alikuwa Renard Christopher, ambaye alizawadiwa nafasi ya kulipiwa michezo miwili katika ligi ya Vodacom, na kupunguza nywele bure mwaka mzima katika saluni ya mpaju pale Iganzo-Stendi ya Chunya.
Picha zifuatazo zinatoa taswira kiasi ya tukio zima. Mungu Ibariki Mpaju Sports Centre, ili Mpaju Day iendelee kuwa chachu ya maendeleo ya Mpira Tanzania na Duniani Kote
|
Mpaju Veterans (Pink) na Mpaju Combine (Blue) |
|
Kocha Nsyani wa Mbalali |
|
Mbalizi Academy Under 15 |
|
Add caption |
|
Icon Academy wakimsikiliza Mwalimu wao Hassan. |
|
Waalimu, Luta (kabana mikono Nyuma),Denis walio pamoja na Twaha Madodi (T-shirt ya Njano), wakiwa tayari kuanzisha mchezo wa Mpaju U-17 dhidi ya Mtoni Junior, wakati Mwalimu wa Mpaju FC Dulayo, (Namba 15) akikagua wachezaji |
|
Mwalimu wa Mbalizi Academy Kassimu Madodi akiwa na wachezaji wa U-15 |
|
Timu zikipasha misuli moto |
|
Mwalimu wa Mbeya Youth (Denis) akiwaasa vijana kabla ya kuanza kuuchezesha mchezo huo |
|
Mwalimu Dens akiwa na vijana wa Mbeya Youth Academy U-17 |
|
Mwalimu wa Mbalizi Academy |
|
Mh. Bashiru Madodi, akijiandaa kuingia kusakata soka, upande wa Mpaju Veterans. Alionyesha uwezo na kuthibitisha kuwa mwanae Madodi Bashiru Madodi ambaye ni mchezaji wa Mpaju U-12 kipaji chake kikubwa kimetokana na Mzee wake. |
0 comments:
Post a Comment