Monday, August 4, 2025

Mpaju FC ATINISU Yawachabanga ICON FC Queens Magoli 6 kwa 2.

DENI LA 2021 LIMEKWISHAAAAAAAAAAAAAA


Wakati Airport Rangers wakitawazwa Mabingwa Wapya Mo Quality Ndondo Cup 2025,  MPAJU FC QUEENS a.k.a ATINISU wametangaza rasmi kuwa siyo tena timu ya kuzungumziwa kwa historia ya jana, bali ni timu ya kuogopwa kwa leo na kesho. 

Habari Kamili iko hivi!!!!!!! 

Huu Ulikuwa Mchezo wa utangulizi kabla ya Fainali ya MO Quality Ndondo Cup 2025 baina ya Mbingwa wapya Aiport Rangers (2-0) African Boys. 

Lakini Mambo ya Hatari yalikuwa kabla mchezo huu. Yaani Mpira wa miguu wa wanawake Mbeya ambao ulitawaliwa na burudani, mshangao, na historia mpya leo hii baada ya Mpaju FC Queens (Atinisu) kuibuka na ushindi wa magoli 6–2 dhidi ya ICON FC Queens, matokeo yaliyogeuza furaha ya wenyeji kuwa simanzi ya hadharani. 

Kwa mashabiki wa ICON waliokuja wakiwa na matumaini makubwa kufurahia ushindi mwingine dhidi ya wawakilishi wa Mkoa katika WRCL 2025/26, hii haikuwa siku yao. Ilikuwa siku ya Mpaju. Ilikuwa siku ya kulipa kisasi. Ilikuwa siku ya kuandika upya historia ya Derby ya Mbeya. 

UBORA KUTOKA BENCHI HADI UWANJANI 
Licha ya uchezaji bora wa wachezaji uwanjani, leo pia ilikuwa siku ya kihistoria kwa benchi la ufundi la Mpaju FC Queens. Chini ya kocha mkuu Ally Ramadhani a.k.a Babu Ally, na wasaidizi Saimon David pamoja na Juma Mpangule, Benchi la ICON limegaragazwa kabisa, kiasi kuishia kumwita refa kila wakati bila mafanikio ya kupunguza kipigo. 

Mpaju FC Queens haikucheza tu ili kushinda waliandika historia. Kocha Babu Ally alionesha ukomavu wa hali ya juu, busara ya mabadiliko, na mfumo uliowapa ICON masaa 90 ya maumivu ndani ya dakika 90. Kwa wengi waliokuwepo leo, ni wazi kabisa: "Kocha Babu Ally ni kati ya makocha bora kabisa ambao Tanzania inaweza kujivunia leo na kesho." 

Mchezo Ulivyoenda 

ICON walianza kwa kasi, wakifunga bao la kwanza. 
Lakini mambo yalibadilika haraka: 
⚽ Josephine “Haaland” alisawazisha. 
⚽ Jerry akaongeza bao la pili kabla ya mapumziko. 

Kipindi cha pili kilishuhudia vumbi la magoli: 
⚽⚽⚽ Josephine akaongeza hat-trick yake na kufikisha magoli manne. 
⚽ Jerry akaongeza la pili binafsi. 
❌ Beki wa MPAJU FC QUEENS Leah akajifunga kwa bahati mbaya. ICON 2–6 Mpaju FC Queens na bado Mpaju walionekana bado wana nafasi ya kuongeza. 

Mastaa Uwanjani Josephine (Haaland): 

Hat-trick + 1 – moto wa kuotea mbali. 
Jerry: Magoli 2 na mchango mkubwa wa kiuchezaji. 
Hidaya a.k.a Mayele na Faith: Kiungo kilichokaa kimataifa — walitawala, walibuni, na waliongoza. 

Historia Ya Kisasi Mwaka 2021, ICON walishinda 9–1 dhidi ya Mpaju. Ilikuwa aibu, ilikuwa mwanzo. Mwaka 2025. Mpaju FC Queens wameandika ukurasa mpya, kwa kisasi cha 6–2 kilichojaa ustadi, kasi na nidhamu. 

 
Rekodi Kamilifu Ya Derby hii Hapa

HAKIKA MPAJU FC QUEENS – MABINGWA HALISI WA DERBY YA MPIRA WA MIGUU WA WANAWAKE MKOA WA MBEYA

0 comments:

Post a Comment