Saturday, December 20, 2025

TDS GIRLS MABINGWA WA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KWA MPIRA WA MIGUU WANAWAKE (WRCL 2025)

PONGEZI NI MUHIMU NA MAFUNZO NI MUHIMU ZAIDI

Tunawapongeza TDS Girls kwa ubingwa wa WRCL 2025, ushindi unaoonesha maandalizi, nidhamu, na ubora wa soka la wanawake. Mafanikio yao ni kielelezo cha kile kinachowezekana panapokuwepo msaada na mipango thabiti. Ni wazi jitihada zinazofanywa kwao zitaendelea kusambaa Tanzania kote.

Tunatoa pongezi pia kwa Mandozi Academy kwa uchezaji bora na ushindi wa 3–0 katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu. Mechi hiyo ilichezwa kwa heshima na sportsmanship ya hali ya juu, ikitoa furaha na funzo muhimu kuhusu ushindani wa kweli.

Kwa timu kama Mpaju FC Queens (Atinisu), WRCL 2025 imekuwa safari ya kujifunza, kuvumilia, na kuwakilisha Mbeya kwa heshima licha ya changamoto za usafiri na maandalizi. Ushindani wa kweli haupimwi kwa matokeo pekee, bali kwa namna timu zinavyoshiriki na kukua.

Tunatoa wito kwa wadau, hususan TFF, kutumia matokeo na uzoefu wa mashindano haya kama msingi wa kuboresha mazingira ya soka la wanawake, ikiwemo kusaidia gharama muhimu kama usafiri kwa timu zinazofuzu.

Zaidi ya uwanja, tunajenga mustakabali wa soka la wanawake kwa pamoja.

Aptitudes Are Authoritative.
Buruhani Ina Mamlaka.






0 comments:

Post a Comment