Vipaji vikali, Uongozi Madhubuti wa Mpira Mbeya Mjini, Ushirikiano wa wadau wa Mpaju SC na bila kusahau, Timu ya wasichana ya shule ya msingi ya Mpolo-Mbalali, Uso kwa Uso na Mdau mkubwa wa Michezo nchini-Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Dr. Tulia Ackson.
Ile Kauli ya Hatua ni hatua, hatimaye
imejidhihirisha kwenye tamasha la Mpaju Week 2019. Pamoja na Changamoto ya
viwanja, kama vile uwanja wa Sokoine na FFU kufanyiwa Mabadiliko, kufuatiwa
ratiba za ligi na mikutano ya shughuli za kitaifa, bado tamasha
limefanyika kwa mafanikio makubwa katika Uwanja wa Magereza Ruanda Mbeya. Kwetu Mpaju SC, hatua hii tuliyofikia ni muhimu sana kuelekea katika mafanikio tarajiwa.
Uongozi wa Mpaju Sc, unapenda kutoa
shukurani za dhati, kwa Uongozi wote wa Mpira wa Wilaya na Mkoa Mbeya kwa ushirikiano
na msaada waliotoa ikiwa ni pamoja na mameneja na viongozi wote wa viwanja
ambavyo tamasha hili lilikubalika kufanyika. Yaani Sokoine, FFU na Magereza.
Bila wao taamsha hili lisingeweza kufanikiwa kwa kiasi hiki.
Uongozi wa Mpaju SC,umefarijika sana
kupewa nafasi ya kuongea kwa karibu na Mh. Dr. Tulia Ackson juu ya chimbuko na
maendeleo ya Mpaju SC, lakini pia kuweza kumkutanisha mheshimiwa na timu ya wasichana
ya shule ya msingi ya Mpolo. Tunaamini ni hatua kuelekea mafanikio ya wachezaji,shule
ya msingi Mpolo na hata Mpaju SC pia.
Zaidi, Uongozi wa Mpaju, unatoa
shukurani kwa wadau woote (Akiwemo Mh
Bashiru Madodi), kwa kusimamisha shughuli zake na sio tu ili kuwa katika
kundi la wazazi walioleta watoto wao kwenye tamasha hili, bali alibaki mstari
wa mbele kabisa kuhakikisha changamoto ya mabadiliko ya uwanja inapatiwa ufumbuzi
wa kudumu, alisaidia sana kupatikana kwa uwanja wa Magereza ambao ndio
tamasha hili limemalizikia kwa siku zote nne.
Sio mwisho umuhimu, uongozi unatoa
shukurani kwa wadau, makocha na wanamichezo wote wanaoendelea kujitoa kwa hali
na mali kuhakikisha tamasha linaendelea kuwa bora na la kufurahisha leo, kesho
na hata milele.Malk Consultants (Eng Mkisi, Lupakisyo,na Architect Kashula), Dr
Said Mkungume na wengine wengi tunawashukuru kwa ulezi wao walioounyesha katika
tamasha hili. Picha zifuatazo ni sehemu ya maelezo ya siku ya kwanza kwa kifupi.
Bila Kusahau, Uongozi unapenda kuomba msamaha kwa woote, kwa maeneo yote ambayo kwa namna moja au nyingine yaliwakwaza.
Figure 1: Mpolo
Shule ya Msingi, wakiwa tayari kuwakabili Mpaju FC U-12 plae uwanja wa FFU-Mbeya
|
Figure 2: Mpaju FC U-12,
wakimsikiliza Mwalimu wao Kocha Ali Mkumbukwa, wakati wa mchezo wao dhidi ya
Mpolo Uwanja wa FFU Mbeya
|
Figure 3: Mpaju FC wakiliandama
Lango la Mpolo katika uwanja wa FFU Mbeya
|
Figure 4: Golikipa wa Mpaju Fc U-12
(Omega) na Mashbiki wakishuhudia, furahia na kuupa nafasi Mchezo umalizike
ili Uwanja Utumike kwa Mkutano wa Dharura uliojitokeza na kulazimika
kufanyika Asubuhi uwanja wa FFU Mbeya
|
|
|
Figure 5: Washiriki wa Tamasha La Mpaju Week 2019, siku
ya kwanza wakihama Kutoka uwanja wa FFU kuelekea Uwanja wa Magereza. Uongozi wa
Mpaju SC, kwa kipekee kabisa unamshukuru Mh Bashiru Madodi kwa msaada wake
katika kuhakikisha tamasha linaendelea vema siku hii. Bila Kumsahau Kocha wa
Ilemi Youth (Ruta Tiba) aliyekuwa bega kwa bega na Mpaju SC katika kuokoa
tamasha hili
Figure 6: Vijana wa U-15 wa Ilemi
Youth wakiwa katika picha ya Pamoja, kabla ya kuichapa Mpolo goli Tatu bila
Majibu (0-3). Ni timu tishio sana.
|
Figure 7: Vijana wa Mpolo U-15
wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuchuana na Ilemi Youth
|
Figure 8: Super Eagle U-12, ( Ambao
pia ni Mabingwa wa mashindano yaliyopita ya Mpaju Cup 2019) wakiwa katika
picha ya Pamoja kabla ya kuwavaa Ferrari FC
|
Figure 9: Ferrari FC U-12 wakiwa
katika Picha ya Pamoja kabla ya kupambana na Super Eagle
|
Figure 10: Super Eagle U-15 wakiwa
katika picha ya Pamoja kabla ya kuwavaa ICON FC
|
Figure 11: ICON FC U-15,wakiwa katika
picha ya pamoja kabla ya kupambana na Super Eagle
|
Figure 12: Mwenyekiti wa Chama cha
Mpira Mbeya Mjini Mzee Gondwe akiongea
na
Baadhi ya Walimu na wachezaji waliohudhuria kuhitimisha siku
ya ufunguzi
Figure 13: Mh.Bashiru Madodi, Mmoja wa
Wadau wa Mpaju SC na Mzazi wa Mchezaji wa
Mpaju FC (Madodi Bashiru) akitoa nasaha kwa wadau
waliohudhuria ufunguzi.
Figure 14:Mpolo Shule Msingi
(U15-Wasichana) Kushoto na Mpaju FC U-12 na Marefa wa
Mchezo wakiwa
Tayari kwa Mchezo Uwanja wa Magereza Mbeya
|
Figure 15: Mh.Naibu Spika, Dr.Tulia
Ackson, Madodi Bashiru na Babu Bakhari ambao ni wachezaji wa Mpaju na wadau wa Mpaju Week 2019 (Kulia Kwake),
baada ya maongezi ya karibu sana Pale Nyumbani Kwake na vijana wa Timu ya
Wasichana ya Mpolo (Kushoto Kwake). Hakika ilikuwa siku nzuri sana kwa Mpaju SC na wadau wake.
|
0 comments:
Post a Comment