Mpaju Cup 2019, ni ligi ya majaribio iliyofanyika jijini Mbeya kwa vijana chini umri wa miaka 17,15 na 12.Ligi hii ya majaribio ililenga kuona uwezekano wa kuwa na ligi ya vijana wadogo Mbeya kwa kuzingatia hali halisi ya kimazingira. Hivyo ilifanyika kwa eneo la kata ya Iganzo. Kwa siku ya Leo
tarehe 29 Septemba 2019, ligi imefungwa rasmi na kiongozi wa mpira wa Mbeya Mjini (Kama alivyoahidi). Kiongozi alikiri kufurahishwa na umati wa vijana na mchezo mzuri waliouonyesha vijana katika tamasha hilli dogo la kufunga mashindano haya. Mbali na kukabidhi zawadi,Kiongozi aliahidi kuendelea kuhakikisha jitihada hizi zinafikia hatua nzuri zaidi.
tarehe 29 Septemba 2019, ligi imefungwa rasmi na kiongozi wa mpira wa Mbeya Mjini (Kama alivyoahidi). Kiongozi alikiri kufurahishwa na umati wa vijana na mchezo mzuri waliouonyesha vijana katika tamasha hilli dogo la kufunga mashindano haya. Mbali na kukabidhi zawadi,Kiongozi aliahidi kuendelea kuhakikisha jitihada hizi zinafikia hatua nzuri zaidi.
Mwenyekiti wa CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MBEYA MJINI -(MUFA) ( Mzee Gondwe ) akiongea na wachezaji wa timu zilizoshiriki Bonanza la Ufungaji wa Mashindano ya Mpaju Cup 2019 katika Uwanja wa James. |
Hongera sana Mpaju juhudi zako naziona na zitazaa matunda siku za usoni
ReplyDeleteThanks Kaka
DeleteHongera sana Kaka, kaza buti, manufaa na mafanikio tutayaona baadae
ReplyDeleteKabisa
DeleteMr. Liverpool, naona uzalendo umeuleta nyumbani na kwa kujua wapi tunakosea ukaanza na shina safi sana mkuu mungu akuongoze ktk hili.
ReplyDeleteKingine labda ni wakati muafaka sasa kuhamasisha jamii yetu haswa wale wanaoishi maisha ya kati hadi juu kwamba mpira ni ajira km ajira nyengine waanze kuwaruhusu vijana wao kuishi na kufuatilia ndoto za mpira km career zingine.
Hizi jamii zina vizazi vya watt wenye afya nzuri kimwili(physical) na akili(mentally)(wanafundishika inshort) mbali na uwezo wa kifedha(wa wazazi wao) unaoweza kuwasapoti km kweli wazee wao wakiinvest kwa vijana wao ndani ya maisha ya soka.
Tumeona vijana wengi sana toka familia bora wakipambaniwa na wazee wao kupata elimu bora wengine kutafutiwa shule nchi za nje huko na kweli mwisho wa siku wanakua educated barabara mana eleimu ya wenzetu haidanganyi basi nadhani km spirit/sapoti hii ya wazazi hawa itatumika kukuza vijana hawa ktk maisha ya soka ndani ya muda mchache tutapata wachezaji wengi sana na kuunda timu ya taifa nzuri tu siku za usoni
Kaka nimelichukua na kimsingi linafanyiwa kazi sana na Mpaju. Kwa sasa kuna wazazi wengine wameanza kuishikisha mpaju sc katika kurekebisha tabia za watoto wao. na wanaonyesha kuwa matokeo ni mazuri. Mfano , kuna vijana wameonyesha kushiriki shughuli za nyumbani ili waweze kuruhusiwa na kupewa vifaa vya michezo, ikiwa ni pamoja kuongeza suala la nidhamu. Hivyo naamini kuna siku watabadilishiwa na lishe tu, hatua ni hatua hata ikiwa ndogo kiasi gani
DeleteNatazamia kumuona mpaju junior ndani ya YNWA mana ulitabiri hili kabla.
ReplyDeleteMungu amfanyie wepec inshallah
Inshallah, Ndoto yetu itatimia Kaka. Huyo hapo https://www.youtube.com/watch?v=MtNu9Ppu7cM&t=31s
Delete