KWANZA TUNAIPONGEZA HATUA NZURI NA KAZI NZURI ILIYOFANYWA NA TUME YA KATIBA MPYA.
LAKINI MAONI YA MABORESHO PIA MUHIMU. NA KAMA ADA, NI VEMA KUWEKA WAZI KUWA MAONI HAYA YANAWEZA KUWA NI SABABU TU YA UPEO MDOGO WA KUIELEWA RASIMU, ILA NI VEMA KUTOA KULIKO KUJA KUJILAUMU KWA KUTO KUTOA MAONI.
WANASHERIA NA WADAU WENGINE WENYE UJUZI ZAIDI TAFADHALINI TUONGOZENI KATIKA HILI
KUTOKA TANKINI
LUGHA YA TAIFA NA LUGHA ZA ALAMA
4.-(1)
Lugha ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano ni Kiswahili na itatumika katika
mawasiliano rasmi ya kitaifa na kiserikali.
(2)
Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), lugha ya Kiingereza inaweza
kutumika kuwa lugha rasmi ya mawasiliano ya kiserikali pale itakapohitajika.
(3)
Serikali itaweka mazingira yatakayowezesha kuwepo kwa mawasiliano ya lugha
mbadala zikiwemo lugha za alama na nukta nundu kwenye sehemu muhimu za umma na
katika vyombo vya habari
vinavyotangaza
habari zake kitaifa kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum.
Kiswahili
kitumike kwenye SHUGHULI ZOTE ZA KIOFISI, ZA KISERIKALI NA BINAFSI KAM LUGHA YA
KWANZA. Hii itangeza UMUHIMU wa Kiswahili na kukifanya kikue na kuheshimika, na
huku ikiongeza UFANISI KITAIFA.
5.
Jamhuri ya Muungano itaenzi na kuzingatia Tunu za Taifa
zifuatazo:
(a)
utu;
(b)
uzalendo;
(c)
uadilifu;
(d)
umoja;
(e)
uwazi;
(f)
uwajibikaji; na
(g)
lugha ya Taifa.
Hizi
Tunu ndio nini hasa kwetu, na zinatoka kwa nani, pia tunazipimaje?
Je!
Fikra Bora, Rasilimali,Vipaji,Ukweli,
Utashi navyo vinaweza kuwa Tunu?
MAMLAKA
YA WANANCHI
6.
Jamhuri ya Muungano ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia
inayozingatia haki ya kijamii, na kwa hiyo:
(a)
wananchi ndio msingi wa mamlaka za nchi, na Serikali itapata madaraka na
mamlaka yake kutoka kwa wananchi ambao kwa umoja na ujumla wao wanaimiliki na
kuipatia Katiba hii uhalali;
(b)
lengo kuu la Serikali litakuwa ni maendeleo na ustawi wa wananchi;
(c)
Serikali itawajibika kwa wananchi; na
(d)
wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali kwa mujibu wa masharti ya
Katiba hii.
Sijui
kama MAMLAKA YA WANANCHI YAKO WAZI SANA HAPA.
MALENGO
MAKUU
11.-(1)
Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha udugu, amani, umoja
na utengamanowa wananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia ustawi wa
wananchi na kujenga Taifa huru lenye demokrasia, utawala bora na kujitegemea.
(2)
Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), lengo hilo kuu litaendelezwa
na kuimarishwa katika nyanja zote kuu, ikijumuisha nyanja za kisiasa, kiuchumi,
kijamii, kiutamaduni na
kimazingira
Lengu kuu liwe Kuboresha Jamii ya
Tanzania kwa kupitia shughuli zinazowanuafaisha na kuwagusa Watanzania wengi
MARUFUKU BAADHI YA VITENDO
21.-(1)
Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu hataruhusiwa kuingia katika ajira
nyingine yoyote yenye malipo ya mshahara.
(2)
Mtumishi wa umma haruhusiwi kuchaguliwa au kuteuliwa kushika madaraka katika
chama cha siasa.
(3)
Mtumishi wa umma aliyestaafu na anayepokea malipo ya pensheni kutokana na fedha
za umma haruhusiwi kuwa mwenyekiti, mkurugenzi au mtumishi zaidi ya vipindi
viwili katika:
(a)
shirika au kampuni inayomilikiwa au kuendeshwa kwa fedha za umma; au
(b)
chombo chochote cha umma
BADO KUIELEWA VIZURI HII ( Hasa namba 1),hapo tunalenga nini, na mishahara yenyewe haitoshi?
HAKI
ZA BINADAMU, WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI
SEHEMU
YA KWANZA
HAKI ZA BINADAMU
HAKI:
Hapa mimi naona bado hapako sawa
- Kwanza, kuwe na haki za Mtanzania, halafu kuwe na haki za Binadamu
- Lugha iwe wazi kuwa Mtaznania ana HAKI YA KUPEWA…………!
- Haki ya Elimu iwe Mpaka elimu ya chuo Kikuu
- Vitu kama Chakula Bora, Afya Bora,Makazi Bora,Elimu Bora,Ajira na Ujira Sahihi,Ulinzi wa aina zote na kadhalika view ni HAKI YA WATANZANIA WOTE na sio makundi Fulani tu. Na ISIANDIKWE SERIKALI ITAWAPATIA FURSA YA KUVIPATA, BALI IWAPATIE KAMA HAKI YAO.
WAJIBU:
Hapa pia kama panahitaji maboresho
- Wajibu wa kufanya na kutafuta na kutambua kazi na majukumu yake halali
- Wajibu wa kulipa kodi bila kushurutishwa na kusaidia ukusanyaji wa kodi
- Wajibu wa kuheshimu na kuzijua sheria za nchi
- Wajibu wa kulinda kuheshimu haki za HAKI za watu wote.
- Wajibu wa kujituma katika kuahakikisha ANAPATA vigezo vya KUPEWA HAKI zake.
MENGINEYO
MPAKA HAPA
Kuna
vitu ni kama havijapewa kipaumbele
- Uwepo wa mchakato wa KUIPATA TUME ITAKAYOKUWA INAFANYA MCHAKATO WA KATIBA. Ni vema katiba ikatamka ili kuhakikisha TUME hiyo inakuwa na utaifa Daima.
- Umuhimu wa kuwa Chombo/Mfumo Huru na Maalumu kwa Ajili ya Ushauri huru wa mambo ya kitaifa na UBORESHAJI wa rasilimali ZETU.
- Msingi sahihi wa Kuchunguza MAZINGIRA YA RUSHWA na KUIDHIBITI rushwa bado hauko wazi. Mfano, kutaifisha mali ya MTOAJI AU MPOKEAJI, kwa manufaa ya Taifa endapo mazingira vidhibiti havitatosha kumtia hatiani mtuhumiwa.
TUSICHOKE KUTOA MAONI, KATIBA NI HATMA YETU WADAU!
CHANGIA MABORESHO TUYAVUGUMISHE TENA
0 comments:
Post a Comment