Wakati Kikao cha 11 sijui, kikiwa
kibichi kabisa,tayari kumekuwa na mambo kibao kutoka Bungeni, ambayo unaweza
kuyatafsiri vyovyote utakavyo. na Watanzania kama kawaida yetu, KILA mmoja
anachagua wa kumtetea. Ili mradi mtu utoe HOJA. Tanki linaomba kuchangia kidogo,
katika mijadala yetu mbalimbali juu ya mwenendo wa BUNGE letu, NA TANKI NALO NI LA BONGO
VILEVILE, hivyo ulisome KI-BONGO BONGO.
Ukiangalia Kifungu cha 63 (2) cha Katiba ya Juamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama sehemu ya pili, Bunge
“………… chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano
ambacho kitakuwa na madaraka,
kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake
vyote katika utekelezaji wa majukumu
yake kwa mujibu wa Katiba hii.” Sehemu ya kwa nza ni ya Bunge inamuhusu RAISI. Simo.
Tanki linaona kama inanitosha kuona kuwa BUNGE kazi yake ni Kuwasaidia wananchi
kuisimamia serikali katika kuwaongoza kuyatafuta maendeleo yao. Yaani kuwakagua
WATAWALA na TARATIBU ZAO, NA KUWASHAURI JUU YA YALE YANAYOWAFAA WANANCHI,
IKIWEMO KUHOJI JUU YA YALE YAENDAYO KOMBO. Hii ni muhimu ili kuhakikisha, WANANCHI wananufaika na NCHI yao,kama
walivyoona iwe kupitia KATIBA. Linafanyika kupitia utungaji wa sheria.
Hivyo, njia nyepesi ya
kulipima BUNGE letu, ni kufikiria kuwa TUNATAWALIWA na watu tofauti ( Mfano
Waingereza/WAKOLONI ) halafu, wabunge/mawaziri wetu wawe wanachangia mambo
ambayo wangependa serikali ya WAINGEREZA ifanye na yale ambayo isifanye! Na
hivyo hivyo ukitaka kumjua MBUNGE wako kama anafanya kazi sahihi, angalia kama
anayoongea/kufanya ambayo yanafaa chini ya UTAWALA huo wa KIKOLONI.
Kwa mtazamo huo, pia unaweza
kupima hata, uongozaji wa BUNGE, kama je uongozaji unapelekea WABUNGE
kuwafikishia UJUMBE sahihi WAKOLONI/WAINGEREZA? Kama haitoshi, ukitaka kujiona
kama, unatoa hukumu sahihi kwa yanayotokea BUNGENI na kwa WABUNGE, jiangalie
kama ungeamua hivyo hivyo kama ingekuwa ni chini ya UTAWALA wa kikoloni?
Njia nyepesi ya kupima ubora
wa sheria unayoitaka, ni kupitia kuandaa sheria ambayo ungependa imuongoze adui
yako. Hivyo MTU SAFI ataandaa sheria hiyo kwa kungalia jinsi inavyoweza kumbana
yeye kwanza. JE,tunaye mtu safi? Hapana. Ubora wa bunge utapatikana kama
wabunge wetu watakuwa na mtazamo wa namna hiyo. Lakini Kubwa zaidi, kama SISI
wananchi tutakuwa na FIKRA BORA za kulitazama hili. UBORA wa BUNGE, liwe kama
TUNATAWALIWA NA ADUI ZETU. MBONGO , JIULIZE KAMA UNAYEMUONA ANAFAA, UNGEMUONA
ANAFAA KAMA ANGEFANYA HIVYO CHINI YA UTAWALA HUO.
USIJIBU.
0 comments:
Post a Comment