ELIMU YA JUU
NI HAKI YA KILA MTANZANIA,
HIVYO
TUBORESHE WAZO BADALA YA KULIPINGA
Kwa mujibu wa Ibrahim Yamola, Mwananchi katika kiungo (http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1753450/-/12aid4m/-/index.html), Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.
Tanki linaafiki kuwa ni suala JEMA: Na kuamini Wataalamu wa Elimu Wamehusishwa ipasavyo.Marekebisho na maboresho yatafuata, na kama kungekuwa na afasi yakupendekeza maboresho, haraka haraka yafuatayo, yangetoka Tankini:
1. Hili liwe KWANZA ni kundi maalumu la WANAFUNZI na KISWAHILI kiwe ndio lugha KUU ya UFUNDISHIAJI na UDAHIRI. Hesabu AU Kiiengereza, yawe masomo ya nyongeza YA LAZIMA kulingana na uhitaji wa mhusika. Kwa kuwa naamini lengo KUU ni kuboresha ufanisi na utashi wa wahusika. Baada ya kuhitimu kwenye kundi hili, ndio kuwe na MAPENDEKEZO ya kozi wanazoweza kujiunga kwenye mfumo wa kawaida kwa anayependa. ILI KUBORESHA
"Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu
kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na
kufaulu kwa wastani wa daraja B.
Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu
kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya
kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu,
lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha
mitihani hiyo maalumu.
Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama
‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa
vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine."
2. Historia ya mhusika kwenye utaalamu,Ujuzi wake ipewe kipaumbele kwenye mitihani ya udahiri ( Iwe na maksi kwenye Maksi za kujiunga). Na kuandaliwe utaratibu wa kuhakiki historia hiyo kabla ya mitihani ya kujiunga. ILI KUBORESHA- “Mfano mtahimiwa anataka kusomea sheria au uandishi wa habari, atatakiwa kufaulu kwa asilimia 50 somo husika, hivyo endapo atakosa kupata asilimia 50 ya somo lake hatapata cheti kitakachomwezesha kuendelea na elimu ya juu,”alisema Dk Marango NA
Kutokana na maelezo ya TCU, mwombaji anatakiwa kuambatanisha cheti cha kuzaliwa au hati ya kusafiria,wasifu wake pamoja na vyeti vya ushiriki mzuri kutoka sehemu anayofanyia kazi.
Vingine ni nakala za vyeti vya taaluma, picha
ndogo ‘passport size, nakala za vyeti vya taaluma za masomo ya hapo
awali, ripoti ya tathmini ya utendaji kazi wake kazini kwa walioajiriwa
kutoka kwa mwajiri na nakala ya kozi za awali alizokwishafanya.
3. Muda wa Cheti, uwe angalau miaka mitano, kwa sababu Mitatu, ni kidogo, kutokana na ukweli kuwa wahusika wengi katika kundi hili, watalazimika kupambana na mazingira magumu ya kifedha na muda wa kusoma huku wakilinda ajira zao!BADALA YA “Cheti tutakachompatia mtahiniwa kitakuwa halali kwa kipindi cha miaka mitatu na baada ya hapo mwombaji atatakiwa kufanya upya mitihani hiyo.”
4. Mitaala ihusishe "UONGOZI", HASA UONGOZI WA UBORA, LAZIMA kwa wote, na MPANGO uharakishwe kwenye maeneo ambayo hayajaguswa ili kutowanyima nafasi hii nzuri wengi wa walio maeneo hayo. Naamini mpango utafanya vizuri, endapo utakuwa karibu sana na wahitaji. ILI KUBORESHA-
((((((Vituo vya Mitihani
Mkurugenzi huyo alisema mitihani itafanyika kati ya Mei na Juni mwaka huu katika vituo vinne vilivyoandaliwa katika vyuo.
Mkurugenzi huyo alisema mitihani itafanyika kati ya Mei na Juni mwaka huu katika vituo vinne vilivyoandaliwa katika vyuo.
Alisema kuwa chini ya mfumo huo Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM), kitahusika na masuala ya Elimu huku Chuo Kikuu Tumaini
Makumira cha Dar es Salaam (TUMADARCo) kikihusika na Uandishi wa Habari
na Mawasiliano kwa Umma.
Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA), kitahusika na
Kilimo na Wanyamapori wakati Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU) kitahusika na
masuala ya usimamizi na utawala,uhasibu, sheria na Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (ICT).
“Kwa kuwa ndiyo tunaanza, tumeamua kutenga vituo
vinne, lakini mwakani tunatarajia kuongeza viwe vingi ili kukidhi
mahitaji ya wananchi walio wengi,”anasema Dk Maronga.)))))
WAZALENDO MTOE MAONI, SIO KULAUMU TU, LENGO HAPA NI KUJITAHIDI WOTE TUPATE ELIMU YA JUU KADRI IWEZEKANAVYO
0 comments:
Post a Comment