Sunday, August 30, 2020

Ziara ya Mpaju SC Shule ya Msingi Mpolo 2020 haitasahaulika

Kwa mara nyingine, Siku ya Jumamosi tarehe 29 Agosti 2020, Mpaju SC walitembelea shule ya Msingi Mpolo iliyopo Mbalali na kufanya michezo kadhaa ya kirafiki. Hii shule yenye hazina kubwa sana ya Michezo ya nchi hii. Mpaju imekuwa na ukaribu na
shule hii kutokana na ushirikiano inaoupata kutoka uongozi wa juu wa Michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali. Uongozi wa Mpaju unatoa shukurani za dhati kwa ushirikiano wote na wa mara kwa mara. Siku ya jana ilikuwa na utofauti kwa sababu ilishuhudia michezo mikali kati ya wenyeji na wageni wote wakiwa na timu za Wasichana. Mpaju FC (W) walipoteza mchezo kwa (1-0) huku wakiwastaajabisha watazamaji kwa kandanda safi na la kueleweka,hasa ukizingatia muda kidogo walio nao tokea kuanzishwa timu hiyo.Tofauti na ziara zingine, hii imeleta mengi ikiwa ni pamoja na Mpaju SC  kupata nafasi ya kuonana na viongozi wa ngazi kubwa wa halmashauri, kuongea na wazazi walioonyesha nia ya kupenda watoto wao kujiunga na Mpaju SC na pia kutolea mikataba ya awali kwa baadhi ya vijana ambao vipaji vyao viliwavutia viongozi wa Mpaju FC. Nisiwachoshe kwa Maandishi mengi, hebu fuatilia baadhi ya picha za tukio zima.

Wachezaji wa Mpaju wakijikusanya tayari kuanza safari kwenye uwanja wa shule ya Sekondari Iganzo

 

Safari ilikuwa nzuri sana, maongezi na Muziki

Vijana wa Mpolo wakiwapokea Mpaju SC

Mwalimu Nsyani akiwakaribisha Mpaju na kutoa ratiba

Kutoka Kushoto: Juma Ahmed Mpangule ( Kiongozi wa Mpaju SC),Godfrey Challe ( Mwl Mkuu-Shule ya Mpolo),Evaristo Makongolo (M/kiti wa Kijiji cha Mpolo),AliMkumbukwa (Kocha wa Mpaju FC), Amosi Chiwaya (Afisa Elimu Michezo na Mgeni Rasmi wa Michezo-Mbarali),Emmnuel Mwasaga (Mratibu Michezo Tarafa ya Ilongo),Raphael Pius ( Mwl wa Dini na Mjumbe wa kamati ya shule namshauri wa shule),Kijanda Nsyani (Mwl wa Michezo shule ya Mpolo),Charles Tuwuye ( M/kiti wa Kamati ya Shule)


Vijana wa Mpolo U12 vs MpajuFC U-12

Vijana wa MpajuFC U-12


Vijana  wa Mpolo U12 vs MpajuFC U-12

Vijana wa Mpolo U12 

Mechi ya Pili Mpolo U (W)vs Mpaju FC (W)(Orange)

Mechi ya Pili Mpolo U (W) vs Mpaju FC (W) (Orange) 
Mpaju Fc (Wasichana) wakiwa  katika Harakati za kuokoa Kona 


Mechi ya Tatu Mpolo U-15 vs Mpaju FC U-15

Mechi ya Tatu Mpolo Tingatinga vs Mpaju FC U-22

Picha ya Pamoja kati ya (Martha Meja (a.k.a. Morrison, kushoto) na Amina Aron (a.k.a Minatha) wenye nyeupe ambao ni wachezaji wa zamani wa Panama FC iliyokuwa Tanzania VPL) wakiwa na wachezaji wa Mpaju(Maria Aron Kakwale wa katikati Latifa Maarufu kama YONDANI aliyechuchumaa) 

Wachezaji wa Mpaju U22 wakishuhudia mchezo wa Atinisu
Watazamaji na wachezaji wa Mpaju Atinisu wakishuhudia michezo

0 comments:

Post a Comment