Sunday, April 22, 2018

“MPAJU SPORTS CENTRE (MSC) DAY”



Wakati wa Kufunga Sherehe
Nembo Kuu ya MSC
Mpaju Sports Centre (MSC) ni Taasisi ya Michezo inayopatikana Mbeya-Iganzo, Tanzania. Taasisi hii inaamini katika Nguvu ya Vipawa na Uasilia. MSC imeanzishwa katika misingi ya kuheshimu vipawa na uasili alionao mwanadamu na mazingira yanayomzunguka popote duniani. MSC inaamini
kwa kuthamini,kujali na kuutumia kwa ufanisi uwezo wa asili wa mwanadamu na mazingira yake, Tanzania na ulimwengu kwa ujumla, vinaweza kufanywa sehemu bora ya kuishi leo na hata kesho. Dira ya MSC ni kuwa Taasisi Bora ya Michezo Ulimwenguni. Lengo la MSC ni kuvumbua na kuendeleza vipawa vya michezo mbalimbali Tanzania na ulimwenguni kote. 


Maandalizi ya Jogging
Katika jitihada za kufanikisha dira na malengo ya MSC, Uongozi wa taasisi, ukiongozwa na Juma Ahmed Mpangule na Abdallah Athumani Kiumbo umefanikiwa kukamilisha usajili wa Klabu ya Mpira wa Miguu inayotambulika kama Mpaju Footbal Club. Usajili wake ni namba 12029, wa siku ya tarehe 05 Machi 2018. Kupitia Mpaju FC, taasisi inatarajia Kushiriki kwa mafanikio mashindano yote halali ya mpira wa miguu, hasa yanayohusisha vijana na watoto chini ya umri wa miaka 23. Pia Taasisi inaamini itaweza Kuburudisha mashabiki wote wa mpira miguu duniani na kutoa mchango katika kuboresha shughuli za kifedha zinahusiana na mpira wa miguu Tanzania na duniani kwa ujumla.

Mwalimu Abdallah Athumani Jogging
Tokea juhudi hizi za MSC zianze mnamo mwezi wa Februari mwaka 2017, maneneo ya IGANZO-MBEYA, kufuatia mwanzilishi ( Raisi wa Taasisi) kuihamishia ndoto yake ya kumsaidia mwanae Ahmed Juma Mpangule kujiendeleza katika mpira wa miguu kuwa ndoto ya jamii yote na dunia kwa ujumla, Mpaju FC imefikisha mwaka mmoja na miezi miwili. Hata hivyo katika kuazimisha sherehe za kufikisha mwaka mmoja, tokea juhudi halisi za taasisi kuanza, taasisi ilifanya sherehe ndogo na kuiita MPAJU SPORTS CENTRE DAY. Shughuli na mambo yaliyofanyika na kufana kama yalivyoelezewa kupitia katika majedwali hapa chini. 

Mwalimu Mpaju Akiongoza Jogging
Mpango ulikuwa kukimbia kidogo, kufanya usafi na kuzishindanisha timu za Mpaju FC kwa makundi yake, yaani kuanzia Kundi A- ambao ni zaidi ya Miaka 18 mpaka Kundi F ambao ni chini ya Miaka 7. Lakini kutokana na sababu zisizozuilika kama vile baadhi ya wachezaji kutopata ruhusa makwao kutokana na ugeni wa tukio zima masikioni mwa wazazi, ilibidi makundi ya kushindana yaundwe upya na hivyo kupata timu 3, timu ya Dulayo, Mpaju na Mastaa wa Mpaju, yaani wachezaji wa Grupu B la Mpaju FC.


Timu za Mechi ya Ufunguzi-(Mpaju FC D,E &F)
 Kwa kifupi, sherehe zilifana, kama ambavyo picha zinadhihirisha. Pia zawadi mbalimbali zilitolewa ikiwa ni pamoja na Mwana Mpaju FC wa Mwaka kupatiwa nafasi ya kunyoa nywele katika saloon ya Mpaju kwa mwaka mzima. Mechi ya Ufunguzi ilihusisha watoto wenye umri chini ya miaka 9 ambao ni grupu la Mpaju FC D na E, japo pia kwa sababu za kimafunzo walimu na baadhi ya wachezaji wakubwa waliruhusiwa kucheza. Kundi hili lilitoa mchezaji bora kwa nafasi ya uzuiaji, Castrol.




 

Timu ya Dulayo wa kiwa na Twaha Madodi-Mabingwa  
Mpaju Sports Centre Day, ilishuhudia Uwezo wa Juu wa kusakata soka, kutoka kwa mdau na mzazi wa wachezaji wawili, yaani Nasfari na Ridhwani, ndugu Twaha Salumu Madodi. Pamoja na Mwili wake kuwa wenye umbo kubwa kuliko watu wote uwanjani, bado uwezo wa kumiliki mpira,na kuupeleka sehemu sahihi ulikuwa burudani kwa kila aliyefika uwanjani hapo, na kwa kiasi kikubwa yeye ndiye aliyekuwa mhimili wa tima ya dulayo kutwaa ubingwa wa Bonanza hili. Alimiliki vizuri eneo la kiungo na kuwafnya viungo wa tima ya Mastaa wa Mpaju kama Asajile na wa Timu ya Mpaju mwalimu Mpaju kushindwa kufurukuta kabisa.

 
MPANGO WA RATIBA YA MPAJU SPORTS CENTRE DAY-31 DISEMBA 2017
S/N
TUKIO
MUDA
WAHUSIKA
ENEO
DHUMUNI
1
JOGGING (MAKIMBIZI vYA TARATIBU)
0800-0900
WACHEZAJI

KULETA HAMASA YA MICHEZO KWA JAMII



VIONGOZI
MTAA WA IGANZO




WAGENI


2
USAFI
0930-1030
WACHEZAJI
MTAA WA IGANZO
KULETA HAMASA YA USAFI WA MAZINGIRA KWA JAMII



VIONGOZI





WAGENI


3
MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU
1045-1645
MPAJU SPORTS
UWANJA WA SHULE YA SEKONDARI YA IGANZO
KUJIBURUDISHA NA KUSHINDANIA ZAWADI MBALIMBALI



TIMU A





TIMU B





TIMU C





TIMU D





TIMU E





TIMU F


4
UTOAJI WA ZAWADI
1700-1800
VIONGOZI NA WACHEZAJI MPAJU SPORTS
UWANJA WA SEKONDARI WA IGANZO
KUWAPONGEZA WACHEZAJI KWA UJUMLA








Mastaa wa Mpaju FC

Kulia ni Mchezaji LANGO wakiwa mbele na mwalimu kumalizia Jogging





Nembo Iliyosajiliwa ya Mpaju FC

Mpaju FC Picha Ya Pamoja Siku ya Mpaju Sports Centre (MSC)

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI MPAJU SPORTS CENTRE





0 comments:

Post a Comment