Monday, August 20, 2018

MPAJU FC Kushiriki Mashindano ya Wilaya U17-Mbeya


Mpaju FC, imepata nafasi ya kushiriki mashindano ya Wilaya ya Mbeya Mjini, kwa vijana wa Miaka chini ya Kumi na Saba, yanayotarajiwa kuanza siku chache zijazo. Mpaju FC imeruhusiwa kushiriki mashindano hayo baada ya kufanikiwa
kupita ukaguzi wa awali uliofanyika uwanja wa Mwenge Mbeya.

Vijana wa Timu Mbalimbali zilizofuzu kushiriki mashindano ya Wilaya Mbeya kwa umri wa chini ya Miaka 17 wakisikiliza jambo kutoka kwa mratibu wa Mashindano na baadhi ya Walimu.
Mpaju FC wakiwa katika Picha ya Pamoja na timu ya Iyunga Foundation (Wenye Jezi Nyeupe) kabla ya Mchezo wa Kirafiki siku ya bonanza la utambulisho wa timu, ambao uliisha kwa Mpaju kupoteza kwa 1-2.
Kufuatia kupatikana kwa nafasi hii, Mpaju FC walikubali kufanya ziara ya kwenda Mbalali kwa ajili ya mechi moja ya Majaribio, kufuatia mwaliko wa timu ya MBALALI COMBINE, inayoundwa na wananchi katika kijiji cha CHAMOTO.
 
Picha Ya Pamoja ya Mbalali na Mpaju
Picha Ya Pamoja ya Mbalali na Mpaju
Andiko hili, mbali na kutoa habari, limeandikwa maalumu kwa ajili kuwashukuru wana-Mbalali Combine kwa ukarimu na ushirikiano waliotupatia kama wana Mpaju Sports Centre kwa Ujumla. Mpaju tunaamini huu ni mwanzo wa safari ndefu ya mafanikio ya mpira nan chi kwa ujumla.

Timu za Vijana Chini ya Miaka 15 za Mpaju wenye Jezi za Njano na Mbalali kwenye picha ya Pamoja
Erick (Modric) akiwa na Mwalimu wake, alichaguliwa  Mchezaji wa Siku.


Asajile Aron- Kepteni wa Mpaju FC U 17-Waswahili wanasema "Anajua Mpaka Anakera", alikuwa kivutio kwa mechi zote, hasa pale alipoonekana kucheza vizuri kwenye mechi ya miaka 14 (Wenzake) na Miaka zaidi ya 17 akiwa mdogo uwanja mzima.

Juma Ahmed Mpangule .a.k.aMpaju

Kocha Abdallah Athumani (Dulayo), na Juma Mpangule (Mpaju) wakijadili kabla ya mchezo dhidi ya Mbalali, Mchezaji ni Kocha-Mchezaji Msaidizi wa Mpaju-Rajabu Ndelele ( Fundi wa Mpira). Pamoja na kuumia, alikuwa burudani kubwa kwa wana-Mbalali  Combine na Mashabiki wao
Adballah Athumani Kiyumbu a.k.a Dulayo


Mpaju FC wakiwa katika Warm Up Mbalali

Mpaju FC Katika maandalizi ya Warm Up

Amon (Mpaju Fc Stopper) akiwa katika Warm Up. Ni kijana wa Miaka 18, ni Beki kisiki wa timu.

Mpaju FC akiongozwa na Golikipa (MwanaMpaju wa Mwaka) mwenye kila sifa ya UKIPA sana (Miaka 15) Emmanuel.

0 comments:

Post a Comment