Sunday, August 18, 2013

KIPAJI NI ASILI HAKITUPWI!!!!!!!!!!!!

Watanzania wengi wa leo wanaongelea vipaji, pengine kuliko kitu chochote. Wengine huongea pengine bila kufahamu hasa kuwa wanachoongela ni VIPAJI. Kipaji ni UWEZO wa ASILI wa KIPEKEE alionao MWANADAMU,kutoka kwa MUNGU.Ukiangalia KIPAJI kama TALENT (Kiingereza) unaweza
kukumbana na maelezo mengi mengi ( http://www.merriam-webster.com/dictionary/talent) mpaka ukachanganyikiwa, lakini kwa Kiswahili, moja kati ya lugha bora sana ulimwenguni, KIPAJI ni uwezo wa asili tu .Maana ya kipaji kwa mujibu wa wasomi kadhaa, (http://www.bing.com/search?FORM=UP97DF&PC=UP97&q=What+is+a+talent), huishia kwenye maelezo mbalimbali yakiwemo maneno mawili makuu (UWEZO NA ASILI), lakini TANKI linaongezea maneno kadhaa lakini moja tu pengine ndio kubwa, MUNGU, hii ni kutokana na IMANI zaidi, kuwa kama kitu ni asili, basi kimetoka kwa mungu, hivyo si vema kuishia kusema ALICHONACHO MWANADAMU bila kusema aliyempatia, naamini wanazuoni watatusaidia kuelezea hili kupitia vitabu vya dini zetu.  Pengine hata wanyama na mimea humiliki VIPAJI fulani, lakini mpaka leo hii, watu wanapoongelea VIPAJI huwa wanavihusisha na BINADAMU.

Tanzania ya leo, kama duniani kote,imeshuhudia mfumuko wa VIPAJI na MAFANIKIO mengi kutokana na vipaji hivyo. Vipaji vilikuwepo, na vitakuwepo. Na kama kuna kitu kinapatikana kwa USAWA kabisa, pengine ni VIPAJI, maana VINATOKA kwa MUNGU. Hivyo, kazi kubwa kwetu sisi binadamu,inakuwa ni KUVIGUNDUA,KUVIBORESHA NA KUVIENDELEZA. Mataifa yanatofautina katika hili, wengine huthamini baadhi ya VIPAJI kuliko vingine, na hufanya juhudi kadri iwezekanavyo kuweza kuviendeleza VIPAJI wanavyovithamini. Tunaona nchi kadhaa, zikitambulika kwa aina fulani ya michezo, kama BASKETBALL MAREKANI au SOKA BRAZILI.Pia zipo nchi zilizotumia VIPAJI vya UTASHI kufanikiwa KITAIFA kama JAPAN.Tanzania sina uhakika sana, ni kipaji gani kinatutangaza, ila nina UHAKIKA kuwa KENYA inajulikana DUNIANI kwa RIADHA. Kwa hiyo, Kwenye riadha, hakuna mtu kutoka nchi iliyoendelea,anayesema MKENYA hamna kitu, na huo ndio usawa kutoka kwa mungu. Naamini hata Tanzania ilikuwa na uwezo wa kuwa kama Kenya, ila tu hatujaamua kuenzi kipaji hicho.

Siku za nyuma, iliaminika kuwa kupitia RAISI WA MWANZA, Tanzania ilifahamika kwa UWEZO wa kisiasa, lakini kadri muda unavyoenda sijui kama BADO imani hii inaendelea. Lakini, ukweli unabaki pale pale, WATANZANIA walikuwa NA wanavyo na WATAENDELEA kuwa na vipaji KWA sababu vinatokana na MWENYEZI mungu! Na hivyo kama mtanzania anataka kuwa sawa na mtu yeyote duniani, ni VEMA ATATAMBUA NA KUBORESHA kipaji chake, badala ya KULAZIMISHA kutumia kipaji cha mwenzake kuboresha maisha yake. Ukithamini KIPAJI chako UMEJITHAMINI wewe, NA UKITHAMINI chako UMEJITHAMINI wewe, na ZAIDI unakuwa unajiweka katika nafasi kubwa ya kuwa mshindani bora (Menye mafanikio Bora) kati ya washindani wa KIDUNIA. Pengine kutatokea swali la nini hasa ni mafanikio ya kujali kipaji chako, kwa leo, ni vema kuishia kuwa , hata furaha inaweza kuwa mafanikio ya msingi kwa mtu, kitu ambacho hasa unaweza kukipata zaidi kutokana na KIPAJI chako.

Familia nyingi za kitanzania, kama taifa pia, KIPAJI kinachopewa kipaumbele mara nyingi ni UWEZO wa darasani, kwa KUAMINI kuwa ELIMU ambayo, tunaipata MADARASANI, hasa ndio msingi wa MAFANIKIO. Kwa mtazamo huo, wengi tumekuwa tukijikuta ni WATUMWA kifikra na hata KUKOSA MISINGI NA MITAZAMO BORA sio tu ya kifamilia, bali hata ya KITAIFA. Hufikia hatua, mtoto ambaye kafeli mitihani, akaonekana hafai katika familia, na kuona mtoto aliyefaulu mitihani hasa ndio mtoto, hata kama kufaulu kwake kulitokana na CHAPO! Hii imepelekea watu wengi kuingia maeneo ya kiutendaji ambayo hawana UWEZO WA ASILI kwenye maeneo hayo, wakati huo huo, wengine wenye UWEZO WA KIASILI kujikuta wakiachwa bila MSAADA wa kuendeleza vipaji vyao. Hili kwa ujumla lazima litakuwa na madhara katika maendeleo ya KIFAMILIA NA TAIFA KWA UJUMLA.

Kifupi ni kuwa, ukikitupa kipaji chako, sio rahisi ukafanya unachokifanya, kwa ufanisi ambao mungu alikuandikia, yaani wa hali juu. Maana PANA zaidi ni kuwa, unapoacha ASILI yako, unajiweka katika hatari ya kutofanikisha mipango yako kwa ufanisi sahihi. Na vilevile, KWA VIONGOZI wetu, wanakumbushwa kuwa wanapotufanya WATANZANIA kusahau vilivyo vyetu vya ASILI, maana yake wanatupeleka njia ISIYO sahihi. "Regardless of the role and regardless of whether the excellence is "celebrated" or anonymous, great managers know that excellence is impossible without talent."(http://businessjournal.gallup.com/content/532/how-great-managers-define-talent.aspx). Kwa mujibu wa kiungo hiki, mameneja hutambua kipaji,kama ni tabia,hisia au fikra za mtu anazoweza kuzitumia mara kwa mara kujipatia ufanisi zaidi katika alifanyalo "a recurring pattern of thought, feeling or behavior that can be productively applied."Hapa funzo ni kuwa kama mtu utatambua umuhimu wa kipaji/vipaji ukaweza kuhusisha na mazingira yako kunanafasi kubwa sana ya kunufaika. Kutokana na machache haya, TANKI linapenda kuwakumbusha watanzania,pamoja na yale yanayotuingizia chakula yetu ya kila siku, bado ni vema KUENZI yaliyo YETU na kujali VIPAJI vyetu, kwa maana ya MATAKWA ya MUNGU na sio vinginevyo, kwa sababu kuna MAFANIKIO makubwa yamejificha kwenye VIPAJI vyetu.

MTOTO AHMED JUMA AHMED  JUMA MOHAMMED MPANGULE
KATIKA JUHUDI ZA KUGUNDUA KIPAJI CHA MTOTO.
KIJANA WA MIAKA MIWILI ( 2 YEARS OLD BOY)


HIZI NI VIDEO KADHAA ZA MASOMO YA SIKU HIYO
 

BAADA YA MAFUNZO, NI VEMA KUJIPIMA

 
Kuyasingizia mazingira ni uongo mkubwa sana, tunaweza kuvitambua na kuboresha vipaji vyetu kulingana na mazingira tuliyonayo, tukiamua na kuelewa kuwa VIPAJI VYETU NDIO SISI. 

KWAKO MDAU
SOKA NI KIPAJI CHAKE MTOTO HUYU?
AU 
AENDELEE KUTAFUTA KIPAJI CHAKE?
TOA MAONI KWA DHATI TAFADHALI, UJENZI WA TAIFA NI WETU WOTE.

MTOTO WA MWENZIO NI WAKO KIJAMII!

10 comments:

  1. nimekuelewa kupitiliza bro!japo sijaona hizo video za dogo ila naamini ntaziona ntakupa feedback!mengi umeyasema,kama mtaalam wa michezo nayatumia sana,huwa napenda kushauri na kuwafanya vijana wajigundue vipaji vyao na kujikubali,ndicho kipo mbele yangu sasa na nna imani ntafanikiwa!' asante bro umesomeka pamoja !..MWANALILA

    ReplyDelete
  2. Mwanalila! Nakuamini sana katika hili!Usikose kuangalia video mwanalila, kuna uhondo wa hali ya juu!

    ReplyDelete
  3. kaka ulichokusema ni sahihi ni muhimu kuendeleza vipaj vya vijana wetu pindi tunapowaona wanamuolekeo na kitu fulani.uchambuzi wako ni makini sana na video za ahmed nimeziona naamin tumepata kipaj cha kweli

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nashukuru, du hata kuweka a.k.a? Bomba mdogo wangu! kumuendeleza ni jukumu letu wote sasa!

      Delete
  4. Ninaomba nianze na; '' KUGUNDUA KIPAJI SI JAMBO RAHISI ''. Na ugumu wake huanzia kwenye kauli ya '' Like Father Like Son ''. Ambayo huwa siikubali, japokuwa katika baadhi ya maeneo hunishinda kuiepuka.
    Mara nyingi huwa ' tunaonyesha ' kipaji, na sio ' kugundua ' kupaji. Kwa sababu binadamu hufundishika, basi huendelea na alichoonyeshwa kuwa ni kipaji chake. Hili lingeepukika kama mazingira ya kugundua kipaji yangekuwa huru kwa vipaji vyote(different talents), jambo ambalo haliwezekani kwa uoni wangu. Kuna watu huitwa wenye vipaji kadhaa, sijui kama inaruhusiwa hiyo.

    Kijana wangu hapo, ninaona Mpira anaumudu, vizuri tu, na anaonekana ni mwenye uwezo mkubwa wa kuelewa na kutekeleza. Nimeshindwa kupata jibu; Hiki ni kipaji cha MPIRA, au cha UELEWA MKUBWA, AU ni UELEWA MKUBWA WA MPIRA, Kipaji bado hatujakigundua!?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nashukuru kwa mchango wako Baraka Nzoshe! Ni kweli nivigumu kujua kama kijana ana uelewa wa Mpira au kipaji cha mpira, na ndio maana, Tanki likawaachia wadau mjadili, lakini kilicho wazo ni kuwa mpira unaweza kuwa ni kati ya vipaji vya kijana wetu. Kugundua/Kuonyesha ni kazi yetu, hatupaswi kuikwepa hata kama ni VIGUMU. Vijana wetu wanahitaji kwa namna moja au nyingine kuandaliwa mazingira ambayo vipaji vyao vitagundulika.

      kumuita mtu ana kipaji, sio vibaya,kwa sababu tumeona mara nyingi kati ya wale waliofundishwa,bado akatokea mwenye uwezo wa kipekee kati hao, na HASA ndicho kipawa kinachozunguziwa hapa, yaani uwezo zaidi ya ule wa kawaida/kujifunza tu! Na kwa kweli, kipaji huwa kina uwezo wa kuonekana hata bila kufundishwa! Hata uelewa wa haraka huwa ni kipaji pia!

      Kwa hiyo, cha kujiuliza, ni nini unadhani, mpira wa miguu unaweza kuwa ndio kipaji chake au la! Kwa kutazama ufanisi wake katika suala zima la mpira wa miguu, kwa kiwango kidogo ulichoona!

      Delete
    2. Kinaweza kuwa Kipaji. Utata ni kujua. Mfano tungempatia mpira wa 'Rugby' na akakimbianao vizuri, tungeweza kuita ' Kipaji cha mpira wa Rugby '!?.

      Hata hivyo, kwa ulimwengu wa sasa sidhani kama inamhitaji binadamu kuwa na kipaji kiviiile ili kufikia anachotaka. Mfano 'Rooney' au 'Suarez'. Kama tunataka aje kuwa mchezampira tunaweza fanya hivyo. Ikitokea kuwa ni kipaji chake itakuwa bora zaidi.

      Ila kwa kumuona hapo anaoneka kuwa ndio kipaji chako.

      Delete
    3. Ni kweli kabisa, tunaweza kulazimisha mtu akafanya kitu chochote tunachotaka, kwa dunia ya leo, lakini,ukweli unabaki palepale, kuwa hilo linahitaji nguvu zaidi kuliko kumfanya mtu afanye vizuri kwenye eneo lake! Mfano, kuna watoto wenye uelewa darasani, kiasi cha kuwa wanaweza kusoma biologia ama hesabu ama siasa ama lugha ama kwenye nyanja za namna hiyo. Kwa uwezo wao huo, mara nyingi bila utashi mzuri, huwa tunajikuta tumewakita/wamejikita kwenye eneo kimsingi, halikuwa na muelekeo wa vipaji vyao, yaani, anakuwa daktari, wakati angefaa zaidi kuw mhandisi, ama anakuwa mwanasiasa wakati angefaa zaidi kuwa Mpimaji na Ramani, tunafurahia sana ufanisi wake katika siasa, kwa SABABU hatujui TUNACHOKOSA kwa ntu huyo KUTOKUWA kwenye MUELEKEO WA KIPAJI CHAKE!!!!!!!!!!! Mfikirie MESSI angekuwa MWANARIADHA, na kutoperform katika kiwango hicho au KAMA PENGINE kipaji chake sahihi ni basketball, hivyo huenda angevunja record za MICHEAL JORDAN N.K!

      NIKIREJEA pendekezo la TANKI kwenye MAANA ya kipaji, "UPEKEE ULIONAO KUTOKA KWA MUNGU", hivyo tnategemea kuwa UFANISI MKUBWA UTATOKA HAPO!

      Delete
  5. Kipaji kinaweza kikatokana na uhalisia wa mazingira husika kwa mtu au mtoto kwa mfano nchi kama Brazil MPIRA WA MIGUU, China KUNG FUU, Marekani MUSIC, MOVIE, NGUMI, South Africa RUGBY, Kenya RIADHA na wakati mwingine watu wanaweza wakajifunza kutokana na Uhalisia wa maisha kutokana na Familia inayomzunguka labda kutoka kwa baba yake, mjomba wake, kaka yake na watu wengine wa karibu yake(yako) kwa mfano Jerrison Tegete kutoka kwa baba yake, Farshad Mogela kutoka kwa Zamorani Mogela, Paulo Maldin kutoka kwa Baba yake na wengine wengi na hii hata ukizingatia kwenye Taaluma nyingine kama Siasa G.W Bush kutoka kwa baba yake, Uhuru Kenyata kutoka kwa baba yake, Hussein Mwinyi kutoka kwa Baba yake na pia Waalimu wengi watoto wao huwa wanakuja kuwa walimu katika ngazi tofauti tofauti.
    Tukija kwa upande wa mtoto Ahmed Juma Mpangule mi naona kuwa anakipaji cha mpira wa miguu kwa kuweza kupiga mpira kwa nguvu kutokana na uwezo wake na nguvu zake na kikubwa zaidi anauwelewa mkubwa wa kufuata maelezo anayopewa na mtu anayemueleza kwa sababu ukizingatia kwa huo umri wa miaka 2 watoto wengi wanaweza wasiweze kufuata maelekezo kama yeye anavyoweza kuyafuata kwa asilimia 90% icho nacho ni kipai kingine kwa huyo mtoto ukilinganisha na umri wake wa miaa 2.Cha msingi na kikubwa zaidi ni kuanza kufuatilia mazingira mazuri zaidi ili aweze kujua jukumu lake ni kuwa mcheza mpira kwa kumnunulia vifaa vya michezo na ikiwezkana uunde kuomba ushauri kwenye Academy za mpira wa miguu za watoto wadogo au ikiwezekana ukapeleke huko moja kwa moja ili kakabobee kuwa kachezaji mpira bora au ikiwezekana kawe kanapelekwa wakati wa mazoezi na baada ya mazoezi kawe kanarudi nyumbani ili kazoee mazingira hayo ya mpira wa miguu.Ila naamini katafanikiwa kwasababu ya mtu wa kumsimamia anaweza kuyafanya kwa nafasi kubwa haya masuala ya usimamizi.Ila sio mbaya pia kama ukijaribu kumjaribu kwenye vipaji vingine kama Basketball, Tenniss, Riadha, Uigizaji na utengenezaji na kudirect Movie anaweza akawa mzuri zaidi kuliko mpira wa miguu ambao umetambulika mapema kuwa ndo kipaji chake. Alafu ukizingatia kuwa VIPAJI NDO VINALIPA ZAIDI KIMASLAHI YA KIFEDHA KULIKO TAARUMA YOYOTE DUNIANI.
    UMEFANYA MAAMUZI YA MAANA SANA KWA KUMUANGALIA HUYO MTOTO KWENYE SIDE B YA UPANDE WA VIPAJI.

    ReplyDelete
  6. Nashukuru J4, naona unamuelekeo karibu sawa na baraka, labda tofauti uchambuzi! Pia nashukuru kwa kuonyesha, kutambua mtazamo wangu wa NJE YA BOX! Kujaribu vipaji tofauti,tofauti na mazoea ya elimu ya darasani.

    Naafiki sana kuwa mazingira yana mchango mkubwa kwenye vipaji, kitu ambacho kinaweza kabisa kuthibitisha kuwa pengine MAANA ya kipaji kama ilivyoongezewa na TANKI, inaweza kuendelea kutumika, YAANI "UPEKEE KUTOKA KWA MUNGU" maana hata mazingira ya asili yana uhusiano na upekee kutoka kwa mungu!

    Lakini tumeanza kushuhudia, WAJAPAN wanawafunga wamarekani BASKETBALL, watanzania wanashiriki NBA, mchina mpira wa mguu unamshinda, japo ni kati ya waanzilishi, na hata ulaya, hawawaze Brazili, hii yote pia inaonyesha kuwa huenda watu huwa hatuhangaiki kutambua na muboresha vipaji vyetu kwa kusema mazingra yetu hayaturuhu, badala ya kuona jinsi gani tunaweza kujichanganya na mazingiras sahihi! George Opong Weah, katokea nchi isiyo fanya vizuri africa, na kutikisa dunia, kwa sababu hasa kipaji kilikuwa kikali kuliko wengi wa kwenye nchi zenye mazingira mazuri, ambao wanawezeshwa na mazingira zaidi. Kuna mifano mingi ya namna hiyo, na ile ya kuonyesha kuwa MTU anaweza kulazimisha kitu kwa sababu ya mazingira, na akafanikiwa, JAPO kumbe angeenda kwenye kitu ambacho HASa MUNGU alimpatia, angefanya vizuri zaidi. KUNA WATU kwa kuwa na shule nzuri, WALIDIRIKI kulazimisha KUSOMA masomo AMBAYO kimsingi SIO eneo sahihi, MATOKEO MARA nyingi huwa ni MAJUTO FULANI SIKU ZA USONI.


    ReplyDelete