Sunday, December 23, 2012

Own Thinking Tank/Tanki la Fikra


Nakubaliana na wewe kuwa pengine hakutakuwa na jipya katika hii Blogu
ila
Si kila tunalolijua tunalielewa vizuri
na
'uongeaji bora huboreshwa na usomaji bora, usikilizaji bora na uongeaji bora'


'Tanki la Fikra', ni mkusanyiko wa kufikirika wa fikra bora ambao ni kama tayari upo kwenye hii Blogu,yaani kupitia washiriki wake mbalimbali.  Tanki hili linaamini kuwa,'Watu hufanya kitu kwa ufanisi mkubwa wanapokuwa wanaamini na kukubali kwa dhati kutoka katika fikra zao!'Hivyo  basi, ukiweza kuboresha fikra za watu hao tayari utakuwa umewapatia uelekeo mzuri wa kimafanikio. Mafanikio bora ndio kitu ambacho wote kama wanadamu wa kawaida tunakihitaji,hasa katika hii dunia iliyojaa ukatili na mabadiliko yatokanayo na utandawazi.Kwa hiyo,kama mwenzetu,tunaomba ushiriki kikamilifu katika Tanki letu hili.Njoo tuokoe maisha yetu,ya familia zetu na Taifa letu kwa kupitia mapinduzi ya Ubora wa Fikra kwa pamoja. 

 Uko tayari? kwa nini unafikiri uko au hauko tayari?

4 comments:

  1. ooh! i like it ,,really enlightening!!!hope to get more from you!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Worry not! we are yet to start actually! I too hope to get more from you

      Delete
  2. Nakubaliana na wewe kabisa, Fikra ni jambo pekee linaloleta maendeleo katika maisha. Kama mtu ataweza kuwa na fikra katika maisha yake na kuzitumia vizuri fikra hizo basi maendeleo yatapatikana kwa haraka sana. Big up Bw. Mpaju kwa kuwa na Fikra ya kuanzisha Blog hii.

    ReplyDelete