Kuongelea Taaluma usiyoijua na hasa kama hii, kidogo mtu unapaswa kuwa jasiri, ama chizi kabisa kama alivyoasa mwalimu Nyerere juu ya kugusa mambo ambayo wengi wamekwisha yafanyia kazi na kuamua tofauti na unavyodhani. Na watanzania ni wepesi wa kumchukia
mtu anapoonekana kuwa muongo,Tanki linaomba watanzania wasilichukie kama huu pia ni uongo kwa sababu katika maisha, mara nyingi kuelewa ni kugumu kuliko kutafsiri, hivyo maana inaweza kueleweka kitaalamu na kikawaida na ama vinginevyo. Tanki, linawakilisha uelewo wa vinginevyo kama mbongo, na hivyo kutoa nafasi kwa wataalamu kutoa mwanga zaidi na sahihi katika mjadala huu muhimu kwa taifa letu. Architecture (A) ni Taaluma ya usanifu wa ujenzi, kimsingi kwa Tanzania
taaluma
hii inahusishwa Zaidi na ujenzi wa nyumba japo inaweza kusaidia hata madaraja
na ujenzi wa namna hiyo pia. Kueleza Maana kunahitaji ujasiri ambao tanki kwa
leo halina. Lakini, tofauti na vile wengi tulivyozoea, kuwa Architects (As) wanachora
ramani za nyumba tu, wataalamu hawa huwa wako mbali Zaidi ya hapo. Huwa
wanatafsiri yale ambayo mtumiaji na mhitaji wa jengo anayawaza ama anatamani
kulingana na taratibu zote za kisheria za ujenzi na mahitaji ya kitaalamu ya
ujenzi, ikiwa ni pamoja na kulipa jengo hilo nakshi sahihi kumridhisha mtumiaji
na mhitaji. Ni wasanii, wanasayansi na pengine ni wafanyabiashara vilevile.
Naipenda maana iliyotolewa na mmoja waigizaji wa SERIES ya MISSING, kuwa (A)
ni taaluma ya Hesabu,Uhandisi na mchanganyiko fikra za Kisanii.Labda alisahau tu kusema
na yenye kuhitaji mtzamo wa kibiashara pia.
Baada ya
muda mrefu, kumejitokeza taaluma nyingine karibia sawa kabisa na hii iitwayo
Architect Technologist (ATs). Kimsingi tofauti ya hizi taaluma mbili inaanzia
kwenye majina yenyewe. Yaani, Zaidi Architects (As), ATs wao wanapaswa
kuubadili usanifu/ubunifu wa majenzi hayo yanayofanywa na As, na kuyafanya
yaweze kujengeka kirahisi ama kiufanisi na kiteknoljia zaidi. Kimsingi tanki
linawatazama wataalamu hawa, ATs kama wasaidizi wa karibu na washirika
wa baadae wa As. Washirika wa karibu kwa sababu wameandaliwa kupokea na
kubadili usanifu kwa ufasaha kuliko wasaidizi wa siku za nyuma, Architect
Technicians (ATNs), ambao hawa ni wasaidizi wa wote. Na ni washirika wa baadae
kwa sababu kwa namna moja au nyingine ATs wanaweza kuendesha miradi ya kiwango
Fulani bila shaka na baada ya uzoefu Fulani, wanaweza kushiriki kwenye miradi
kama wataalamu wenza wa As.Yaani, kufikiria jengo sahihi kwa kazi fulani (Hoteli)-As, na kuionyesha inavyofanya kazi vema Ngamizi/kompyuta (ATs) ni vitu viwili tufauti. Na zaidi kama unaweza kusema vigae hivi vitasaidia kuzuia joto kiasi fulani lisipotee vyumbani, lazima uwe unajua vigae hivyo ni vya aina gani na vijengweje. Hivyo hivyo kwa rangi na kadhalika na hata mengine kama vile kusema UMBO HILI haliwezekani kujengekeka, wakati hakuna aliefanyia tafiti kuthibitsha hilo, zaidi ya yule anayesema haliwezekani.
Kama ilivyo
ada kwa binadamu, ni WABISHI sana kukubali WAZO JIPYA. Kuna wataalamu waliuawa
kwa sababu tu wanasema dunia sio bapa. Hivyo hivyo, kwetu Tanzania, mpaka sasa
kuanzishwa kwa ATs kunaonekana kama ni kwa kisiasa Zaidi, maana mijadala juu ya
kuwatambua wataalamu hawa inachukua muda mrefu na sura tofauti kiasi cha
kuwafanya vijana wanaomaliza vyuo kama ATs, wajiulize kama walifanya chaguo
sahihi au la! Ukithubutu kuongelea, utaulizwa maswali magumu mpaka ujute,
lakini swali kubwa ni, je kutokuongea ni kwa faida ya nani? Wengi hawapendi
kusikia maneno ya mitaani, hasa wataalamu na wanasayansi, lakini wanasiasa
wengi wanafanya vizuri kwa kuanza kusikiliza maneno ya mitaani, maana FUNUNU
ndio mwanzo wa tafiti. Kufuatia ujinga huu wa kijiweni, Tanki lina mawili matatu
kwenye eneo hili.
ARCHITECTS
Kwa ujumla
hawa ndio wakuu wa taaluma hii nchini. Mabadiliko yanapaswa kuanzia kwao kama
tunataka yatuletee manufaa kirahisi. Imekuwa kawaida kwa taaluma mbalimbali
kama hizi kumegwa ili kuongeza SPECIALIZATION. Tumeona kwenye Wakadiriaji
Majenzi,Wapimaji na ramani,Wahandisi Umeme,Mawasiliano na hata Ustawi wa jamii
na Utawala. Kwa mtazamo huo, pengine ni wakati sasa kuwaruhusu wengine pia
washiriki katika KEKI yetu. Hili lina faida wakati Fulani, ya KIFANISI na
KIUCHMI kwa WOTE. Muhimu ni kujiuliza, ni kweli As wanahitaji ushiriki wa ATs,
ama ni misukumo tu ya kisiasa inaingilia taaluma? Ama swali jepesi, ni kama kati
ya Architect na Architect Technician tunahitaji mtaalamu mwingine kulingana
na mahitaji ya Taaluma kiutendaji. Kwa mfano; TIMU ya ujenzi ikiwa na CLERK OF WORKS, mwenye taaluma ya
ATs, inaweza kuongeza ufanisi Zaidi? Kweli kuna UPUNGUFU, kati ya
USANIFU/UBUNIFU na UTENDAJI/UHALISIA, ambao TEKNOLOJIA inaweza KUZIBA pengo?
As
wanapaswa kuwakaribisha kwa ROHO safi ATs KAMA, wanakuja kuboresha TAALUMA na
kuifanya ikamilike kwa kuziba PENGO HILO. Na wana paswa KUONYESHA kwa vitendo
kwa WATEJA wao, yaani WATANZANIA kuwa ATs wataleta madhara tu, maana WAO
wanatosha na WANATEKELEZA sit tu yote bali na Zaidi ya ambayo ATs wanakuja
kuyafanya. Hili ndio sahihi, kwa sababu litaonyesha kuwa ATs hawahitajiki, na
pia kuna madhara kuwa nao. Lakini, ikiwa ni maneno tu, inakuwa na mushkeri. Pengine
kuna upungufu umekuwa ukiwakera WATANZANIA, ila tu kwa sababu hawajui kama unawezekana
kuondolewa, wakawa wanaendelea kuvumilia,na pengine hawajui radha nyingine.
Maana wanasema motto akizoea chakula cha mama yake huamini ndio bora kuliko
kingine.
ARCHITECTS TECHNOLOGISTS
Inaaminika
kuwa NADHARIA bila VITENDO ni BUTU na VITENDO bila NADHARIA ni UPOFU. Hili
linaweza kufanana kidogo na hizi taaluma. Msingi wa ATs ni kuweza kutafsiri
taswira ya As na KUWEZA kuiunganisha na UHALISIA kwa watendaji wengine kiufanisi
Zaidi kupitia TEKNOLOGIA. Hivyo kimsingi hawa sio wataalamu wa KUTAFSIRI
TASWIRA ya TAJIRI, na kuifanya IUNGANISHWE na UNAKSI WA JENGO, SHERIA NA
TARATIBU ZA UJENZI na MAHITAJI YA WATUMIAJI. Wanaofanya hili ni As. Kwa mtazamo
huu, ATs wanapaswa kujikita kwenye eneo lao la KIUTENDAJI Zaidi. Kimsingi
wanapaswa kujiandaa kuwa na ubunifu,utashi na uwezo katika uelekeo huo kwa kutumia
Teknolojia sahihi. Kama mafunzo na maandalizi yao yatakuwa yakiishia kwenye uelekeo
wa As na ATNs Zaidi, itakuwa UTATA. Mazingira yanaonyesha hali hii ya Utata
ndio KIKWAZO,maana inakuwa kama TANZANIA inaongeza As wenye UPEO usioridhisha
sana wa KISANIFU na kuwabandika NEMBO ya ATs, kisha kuwamwaga SOKONI ambako
wanaenda kufanya kipande ama kazi yote ya As,yaani wanapewa nafasi ya kuonja keki kwene sherehe isiyowahusu wakati waalikwa bado wako kwenye foleni. Kikwetu hii huwa inauma sana,hata kama mwalikwa pia hakuchangia,anaweza hata kufoka na kuharibu sherehe kabisa.
Kwa hiyo
ATs, wanapaswa KUWAONYESHA As nini hasa Tofauti yao na WAO kwanza. na ni nini
hasa tofauti yao na ATNs. Na zaidi, Wanaoamini kuwa ATs ni muhimu na ATs
wenyewe, wanapaswa kuwaonyesha WATANZANIA kwa Ujumla ambacho WANAKIKOSA kwa kutoka
na As, ama WANACHOATHIRIKA kwa kuwa na As bila ATs. Bila kusahau pia,
kuwaonyesha As na ATNs, wanachokikosa kwa kuwa pekee yao bila ATs.
UJIO WA BUILDING INFORMATION MODELLING-BIM
Hili ni zao
la teknolojia, sasa dunia inakimbilia kwenye kuhakikisha kila mtu anashiriki
kwenye mchakato wa ujenzi kwa uwazi kabisa kupitia HIFADHI ya pamoja ya taarifa
zote za kitaalamu. Moja kati ya vikwazo vinavyojitokeza ni ugumu wa As
katika kushirirkiana na ATNs.
Mawasiliano yamekuwa kikwazo katika kuongeza ufanisi na tija kwenye sekta ya
UJENZI. Wakati BIM inaonekana kutatua hili, na kukubaliwa dunia, sisi tunajiuliza
kama tuwakaribishe ATs au la.Kama BIM itashika moto nchini, ATs ni wataalamu
ambao tutawahitaji sana kuhakikisha tunafanya vizuri. Hii ieleweke kuwa hapa
ATs ni utaalamu na sio cheti cha usajiri au cha kuhitimu cha ATs.
BIM
inawezesha TAJIRI/CLIENT kuhusika na kuona jinsi jengo
litakavyoweza kuwekwa kwenye ardhi, katika uhalisia wake kabla ya kwenda
kujengwa,ama jinsi mwanga wa asili utavyokuwa unapunguza matumizi ya umeme. Haya na
mengine mengi yatahitaji sio tu muda bali mafunzo, ambayo pengine yakawa sio tu
ATs bali hata watu wa ICT, ambao mara nyingi huchukuliwa kama ni watu wa baadae
sana. Lisemwalo lipo, UMIMI unaondoka jamani, ni vema tukaondokana nao kabla
haujaondoka na sisi.Kama ATs ni wataalamu muhimu katika kuharakisha BIM nchini, maana yake mjadala utanuke zaidi na kuona ni jinsi gani tunajichelewesha kukamata soko la afrika katika Ujenzi. Maana BIM mpaka sasa ni sehemu chache tu ambazo zimejaribu kutumia ikiwemo bondeni pale kwa mzee Madiba.
WASHIRIKA WENGINE WA UJENZI
Ujenzi una
washirika wengine wengi kama wahandisi na wakadiriaji majenzi. Hawa wote wana
vita zao za ndani kwa ndani, hata kama kwa namna moja au nyingine hazijafikia
mahala pa kulipuka. Nao pia hawana budi kujiuliza kama UJIO wa ATs, ni neema
ama hatari kwao? Kwa kawaida ujenzi unategemeana sana, na hivyo kama wengi
wataona ujio wa taaluma hii ni neema, hawana budi kuwaambia WATANZANIA haraka
kuwa ATs ni muhimu. Huu sio wakati wa Bodi ya wahandisi kujitenga na bodi ya
Wasanifu na Wakadiriaji majenzi, ama kujitenga na bodi ya wakandarasi. Ni
wakati wa kuunganisha nguvu na kudumisha mawasiliano na kuona ni wapi sekta ya
ujenzi inaenda. Ni vipi sekta hii itaondokana na kuomba msaada wa KUPENDELEWA
na SERIKALI na kuwa inaomba KUISAIDIA serikali. Ni wakati wa kuona washiriki
wake wanaogopwa nje ya mipaka ya TZ, kwa uwezo na sio vinginevyo. Na ni wakati
AMBAO ukweli ni kuwa KUKUMBATIA KAZI,TAALUMA, NA kadhalika ni KUJINUFAISHA kwa
KUTEKETEZA TAIFA. UBORA wa sasa HAUPATIKANI bila ushiriki wa kila mtu ipasavyo.
MTAZAMO/MONI/PENDEKEZO/n.k
1. Pengine
hili sasa kwa NCHI kama TANZANIA linamaanisha kupokonya KEKI kubwa ya As, kwa
sababu kwa Mtanzania habari ya UNAKSI na UTAALAMU sio MUHIMU labda kwa MIRADI
mikubwa sana,ambayo pengine haichukui asilimia kubwa ya kazi za Wataalamu hawa.
Lakini maslahi ya watanzania yanapaswa kupewa kipaumbele, kwa maana ya
UBORESHWAJI wa TAALUMA na HUDUMA na SIO vinginevyo. Kama ATs hawafai, tufute,
maana vijana wanazidi kumaliza, na kama tunamashaka na ubora, basi wasajiliwe
(kwa muda chini ya As), wakati tunapembua Zaidi. Kuna umuhimu wa kujadili
kitaifa Zaidi, ili tujue undani badala ya kulisikia chinichini, na pengine hata
wafanya maamuzi wakiulizwa hawalijui kabisa. Ni kawaida sana mambo kuzuiliwa
kwa hofu ya KIMASLAHI ZAIDI ya KITAALAMU. Na matokeo yake ni kudhorotesha
maendeleo ya VYOTE kwa WOTE.
2. Dunia
haitusubiri sisi, TEKNOLOJIA inakimbia. Mfano mwepesi ni ujio wa Building
Information Modelling. Ni wakati sasa tutambue kuwa Teknolojia ni kitu chenye
uzito wa peke yake, na kama hatutakiheshimu, ni wazi kuwa tutatupwa nje ya
SOKO. SIjui kama wakati Tanzania inaanza kutumia Ngamizi, Kompyuta, kufanya
usanifu, kama kulikuwa na usumbufu wa namna hii au unaofanana na huu. Maana
kama hali ilikuwa hivyo, basi huenda imechangia kutuchelewesha katika matumizi
ya Ngamizi kwenye taaluma hii. Leo hii naamini As wanaotumia na wasiutumia
Software mbalimbali, kama ARCH CAD,AUTO n.k kadhalika watakuwa wanashirikiana
vizuri na wanajua maana na tofauti ya pande mbili, yaani teknolojia na sayansi
ya taaluma katika utendaji. Kwa mtazamo huo huo, nafikiri tunaaswa kutambua
kuwa ukijikita kwenye sayansi a taaluma una weza kukosa uwezo sahihi wa
kiteknolojia, na hivyo kuhitaji mwingine kubobea kwenye eneo hili ambalo ni
muhimu kwa maendeleo ya pamoja.
3. Taaaluma
kama hii ya (A) sio ya kuifanyia mzaha, na kuifanyia USOKO huria kama ambavyo
tunafanya kwenye vitu vingine. Hii ina maanisha, ni lazima kuwe na tafiti
sahihi, kuhakikisha kuwa uamuzi unaochukuliwa ni wenye kulinda UBORA wa taaluma
na MAISHA a watu. Hivo hata ATs, wanapaswa kulijua hili, na kutochukulia kama
wanazuiwa kwa maslahi binafsi, hata kama kutakuwa na ukweli. Kilicho sahihi ni
kufikiria kuwa, vyovyote iwavyo wanazuiwa kwa SABABU kuu YA WATANZANIA,
wakiwemo watoto na wajukuu wao mpaka vitukuu vyao. Na Zaidi ni wenyewe, maana
tuendako, bila misingi imara, yeyote anaweza kudhulika wakiwemo wao. Lakini,
pia kwa upande huo huo, tutambue pia kuwa MAZINGATIO ya ujenzi ya MWAKA 47 na
sasa ni tofauti. Leo,mazingira,ubora,gharama n.k ni vitu vyenye sura tofauti na
siku za nyuma. Hii ina maanisha, mtaalamu wa zamani aliweza kuzingatia vitu
vichache na kwa uchache nab ado akakubalika, kuwa kafanya kazi timilifu. Lakini
leo nguvu ya soko na utandawazi umeleta taswira tofauti juu ya utimilifu wa
kazi, na hivyo, kama mtaalamu ataendelea kuwa na mzigo mkubwa, kuna uwezekano
mkubwa sana, akatoa sio tu kazi timilifu bali hata kazi isiyo na ubora
timilifu, kitu ambacho kinawiana kabisa na KUHATARISHA MAISHA ya watumiaji kwa
KUWARUHUSU ATs kuvamia Taaluma. Tunajione maamuzi mengi ya kisiasa
yanavyotudhulu kwa kumbukumbu za mwalimu alifanya hivi ama mbona tulikuwa
tunafanya hivi tu na kitu kinajipa.
Makundi na
shindani sio mbaya, kwa sababu taaluma hizi zina asili hiyo. Yaani, watu
hucheka na kuongea wkiwa nje ya kazi, lakini wanapoingia kaziani, ni ushindani
na utaalamu tu vipaswa kupewa kipaumbele. Kinachojitokeza sasa ni upandikizi wa
ushindani na chuki zisizo na tija, yaani kama akinananihii. Hili sio zuri,
lakini kama waswahili wasemavyo, AKIMWAGA MBOGA, MWAGA UGALI, mkiumwa njaa
mtaelewana.
Kama kawa,
WABONGO, cha kwanza ataangalia REFERENCE ili aanze kubishana. Lengo hapa ni
kuamsha hamasa ya kulielewa hili swala kwa undani, kujua kama kuna umuhimu wa
kumwaga mboga,ili wote tusile.Swala la kasema nani, kwa sasa sio muhimu,muhimu
ni MJADALA juu ya ATs Tanzania, kama
sehemu ya kuboresha ARCHITECTURE na UJENZI kwa ujumla. Na zaidi ni kuwa kuna umuhimu wa kujadili mambo katika mtazamo wa Kitaifa zaidi kuliko kimaslahi ya kitaaluma.
SWALI LA KIZUSHI: Architectural Technology, tuna TAALUMA AU JINA?
…………IT
IS JUST THE BEGINNING………………
i like it sir...ni changamoto nyingi tumeshakutana nazo sana huku makazini kuna wanaojitahidi kuelewa na wengine kubeza kabisa...utata unakuja hapa sisi ni kina nani na kazi tunazofanya ni zao pia na ni kina nani wametu train .....wabezaji husema architects ndo walio tu train kwa hiyo tutabaki kuwa ATNs....napenda kukili makosa ya sisi tuliotangulia huku mitaani japo tunafanya kazi as kupata pesa kwa sasa ila HATUNA UMOJA kabisa juu ya hili...wakati tunasoma tulikuwa tunafikilia kumaliza na kuingia mtaani...hatuna mwongozo wala ukweli juu ya elimu hii. sasa INATUPASA KUWA NA UMOJA NA KUUNDA MOVEMENT za kujulisha uma sisi ni kina nani.....
ReplyDeleteUko sawa, kuwa na umoja ni muhimu. Ila mjue umoja wenu haupaswa kuwa na lengo la kubishana, bali kuwabainishia watumia huduma yenu tu,kuwa nyie sio wao na ni nini wanakosa kwa kutowatumia nyie. Na njia nyepesi ya kulifanya hilo, NI KUFANYA KAZI katika UBORA wenu, yaani wenye UTOFAUTI ni WAO.Naamini, HATA Architects, waliomakini wanajua ni jinsi gani wanahitaji ATs. Tatizo la TZ, huwa hatujui kwa nini tunahitaji kitu fulani, ndio maana mtu anadhani kuwa TECHNICIAN maana yake,kufanya kazi chini ya MTAALAMU kama MBUMBUMBU,kuwa HUNA LOLOTE MBELE YA MTAALAMU. Kumbe HAO NI WATU WAWILI TOFAUTI, wanaotegemeana katika utendaji .Dunia ya sasa hata TARISHI ANA UMUHIMU WAKE OFISINI, hivyo MAISHA ni ya kutegemeana zaidi ya KUENDESHANA. Muda si mrefu majibu mengi ya matatizo ya namna hii, yatapatikana. Nashukuru.
Delete