Monday, December 2, 2013

SAYANSI YA NINI BONGO ?



Sayansi ni neno ambalo pengine watanzania tunalitamka sana. Kati yao wapo ambao tunalitamka na kulitumia vizuri, na pia ambao hatulitumii vizuri ama na hata kutolifahamu kabisa kama sio hata kulitamka na kulisikia.Ukianza kuzungumzia maana, unaweza kuzua UBISHI badala ya MJADALA, kitu ambacho ndio JADI yetu WABONGO. Lakini,  KIBONGOBONGO,potelea mbali acha tubishane tu mpaka tufe na NJAA. 

Kimsingi,

Sayansi ni utashi,uelewa utokanao na fikra ama elimu katika nyanja yeyote ile,ili mradi tu upatikanaji huo wa utashi umepitia njia ama taratibu thabiti na madhubuti ikiwemo uhakiki bayana wa KITAFITI. Lengo likiwa ni kuongeza “UTASHI JUU JAMBO FULANI”. Hii ina maanisha, kuwa karibia kila kiumbe kinaweza kuitwa mwanasayansi, ili mradi tu kinakidhi misingi kadhaa katika kutupatia utashi fulani,yaani nadharia sahihi na uthibitisho madhubuti katika kufikia kiasi hicho cha utashi huo. Tafiti za kisayansi, nazo zinapitia hapohapo,kwamba kama ikiwezekana, ili kukamilika kuwa utafiti wa kisayansi, basi uwepo wa nadharia sahihi na uthibitisho madhubuti wa jambo fulani, ni muhimu kukamilisha sifa ya utafiti bora. Pengine tofauti ni kuwa tafiti zina lenga kutupatia MAELEZO kuhusu jambo kwa manufaa yetu.

Mfano: Ukisema MTOTO ASIPOCHEZA SIKU NZIMA, NI DALILI YA KUWA NI MGONJWA, kama kuna nadharia sahihi na uthibitisho madhubuti, kuwa huo ni UTASHI mpya muhimu kwetu,basi nawe ni mwanasayansi, na ULE utaratibu na hatua ulizotumia kufikia UTASHI huo (tangia nadharia mpaka vidhibiti) ndio unabeba sifa za kitafiti kama ni wa kisayansi au la.Kikubwa ni matumizi ya kifikra kwenye kujengea nadharia/mitazamo na vidhibiti kimtaa na kuweza kufikia hapo. Swala la mwanasayansi bora na kiasi cha sayansi yako kutumika kwenye jamii, litupilie mbali, ama angalia mazingira yako, ili mradi usiifuate nafsi/moyo zaidi ya ukweli na uhalisia sahihi,sio wa wengi wape,bali wa wengi bora wapewe.

Sasa, porojo ni nyingi sana juu ya sayansi hasa ukitaka kujua kuwa chimbuko hasa ni kwenye  imani za kidini, wakati UTASHI ulitegemea IMANI tu, ikapitia hatua ya utashi kutegemea uwezo wa kifikra  na mpaka leo hii wakati imeonekana vema uthibitisho wa uhalisia usaidie uwezo wa kiakili/fikra kuonyesha kuwa nadharia ni sahihi na inamaanisha uwepo wa UTASHI sahihi katika maisha yetu. Kuna maubishi kibao, japo sio kama ya KIBONGO,yasiyolenga KUJENGA, bali kuonekana nani zaidi.

KWA NINI TUNAHITAJI TAFITI ZA KISAYANSI

  1. SAYANSI SIO UBISHI
Sayansi haiko kutufanya tubishane, bali kutufanya tufikie muafaka ambao unatufaa wote na hasa tunauamini na kukubaliana kuwa unatufaa, ili kesho tusipate kutupiana lawama. Bila hili, hatuwezi kuwa tunaenda mbele,kwa sababu WATU ni wapekee.Kila mtu anajua na kutaka lake kwa sababu zake 

  1. SAYANSI HAIKATAI IMANI
Sayansi na dini bado ni vitu viwili, vinavyoendelea kuchuana, kama baba na mtoto wa kwanza. Uwepo wa vyote ni muhimu kwetu na kwa vyenyewe. Huna sayansi, pengine utachelewesha kusambaa kwa imani, kwa sababu vitendea kazi vya imani nyingi vinatokana na ugunduzi wa kisayansi na imani pia zinasisitiza kusaka UTASHI kwa udi na uvumba kama sehemu ya kuonyesha kuwa ni muhimu kuwa mwanasayansi ili uendeleze imani. Na pengine unapoacha kuamini tu ndipo uanasayansi wako unapoelekea mwishoni,maana unakosa wa kukuongoza, ama dira.

  1. UTATUZI WA MATATIZO
Utatuzi wa matatizo unahitaji FIKRA na pia UTHIBITISHO wa UHALISIA kimaisha. Hili moja kwa moja linatupelekea kuhitaji sayansi, ili kuwa na uhakika kuwa TATIZO ni nini hasa Na UTATUZI WAKE ni upi hasa. Maana bila ya hivyo, tutakuwa tunabahatisha kila wakati,kitu ambacho ni sawa na KULA SUMU. Mfano, ni pale tunapojua kuwa RUSHWA ni TATIZO,lakinihatuwezi kuijua rushwa kisayansi. Matokeo yake, tunaanza kukubaliana na wazo la KIONGOZI bila utafiti wa kisayansi, matokeo yake tunakuja kugundua kuwa hatukutibu UGONJWA bali tuliongeza,tayari tumeumia. Kama haitoshi, maendeleo yanahitaji UVUMBUZI NA UBUNIFU KADHAA WA KADHAA, ambao unahitaji utashi utokanao na UTAFITI wa KISAYANSI. Ndio hivyo wenzetu wanavyoendelea jamani.

  1. UBORA WA KIFIKRA
Kama haitoshi, dunia tulionayo ni ya KISAYANSI, hivyo kama hatuwezi KUFIKIRI kisayansi, maana yake hatuongei lugha moja na wenzetu,hivyo hatuwezi kuwaelewa. Na matokeo yake watatudanganya usiku na mchana. Huwezi kujua kama utafiti uliofanyika kuhusu DAWA ya MALARIA unayoitumia ulikuwa sahihi, na hivyo kuthibitisha MATUMIZI ya DAWA hiyo kwa binadamu,kama MWENYEWE HUNA misingi ya tafiti za kisayansi. Vile vile unaweza hata KUOGOPA kivuli chako, kwa sababu UTASHI wa kisayansi UKO mbali, na hivyo kujichelewesha kimaendeleo. Mbaya kabisa, utaendelea KUJILISHA sumu za UTASHI kwa kudhani unatibu matatizo yako kumbe la hasha,hakuna kitu,unaahirisha maumivu tu.

HITIMISHO
Tunahitaji kufahamu matumizi ya neno sayansi na kuelewa hasa sayansi ina umuhimu gani katika KARNE hii bila kujali itikadi zetu ama imani zetu ama asili zetu. Mwanasayansi anaweza kuwa mtoto,mtu mzima, mwanamke ama mwanaume na hata pengine wanyama na mimea ituzungukayo kama sio MUNGU. Imani za kuwa kuwa mwanasayansi lazima uwe na hesabu kibao ama fizikia na sio siasa, si za msingi kwa maisha haya, ama kuwa lazima uwe umefikia chuo kikuu, hazitusaidii kwa sababu matatizo mengi sana yako majumbani mwetu ambayo kwa kujua misingi hii ya sayansi,mtu anaweza kutatua matatizo yake kisayansi kwenye kiwango chake.

Mbongo lazima ubishe, kwa sababu sio mwanasayansi,hivyo hutaanza kuangalia ANDIKO kama ni la KISAYANSI, bali utaanza kubisha.Lakini jiulize “mtoto akichezea wembe mpe”, ni msemo wenye maana gani? Kama sio kuwa NADHARIA ya msingi kabisa kuwa mtoto anaweza kuwa NI KING’NG’ANIZI, na huku hajaelewa mambo mengi kwa sababu bado angali na umri mdogo hivyo anajifunza,hajaona mengi na anapaswa kuwasikiliza sana wakubwa na kupima kabla ya kubisha na kuendelea, na uthibitisho kuwa wembe si rahisi UKAMUUA,bali utampa fundisho ambalo litamfanya ASICHEZEE BOMU siku nyingine akiambiwa linaua, ni kweli na ni UTASHI sahihi kwa jamii yetu!

Kudharau haya kumetupelekea sasa, si ajabu, mtaalamu wa UJENZI anataka aulizwe kuhusu ujenzi tu, na pengine katika eneo lake tu, kwa sababu mengine hayamuhusu, hivyo ripoti ya gazetini kuhusu siasa ataimeza na kuitema popote kwa UHAKIKA kabisa,ama atasema hili sio tatizo langu,japo ni mkazi wa eneo husika. Mcheza mpira haamini kama kuna misingi ya mpira, zaidi ya kipaji, wala mwanasiasa anaamini uongo ndio msingi mkuu wa siasa, na  mwanahisabati kajitoa kwenye maboresho ya katiba. Mkubwa hataki kuulizwa na mdogo, na mdogo anaamini tamthilia na blogu kama hii, kuliko wakubwa zake.

“Mankind has tried the other two roads to peace - the road of political jealousy and the road of religious bigotry - and found them both equally misleading. Perhaps it will now try the third, the road of scientific truth, the only road on which the passenger is not deceived. Science does not, ostrich-like, bury its head amidst perils and difficulties. It tries to see everything exactly as everything is. (Professor Garrett P. Serviss)”. 

............ITAENDELEA......

0 comments:

Post a Comment