Friday, November 1, 2013

MATOKEO MAKUBWA SASA-BIG RESULTS NOW (BRN)

UFAULU USIORIDHISHA ni BORA kuliko UFELI USIOKUBALIKA.

Tamko la kubadilisha mfumo wa Alama wa matokeo a kidato cha nne na cha sita, umepokelewa kwa hisia tofauti na Watanzania ambao wana hamu ya kuona MATOKEO MAKUBWA SASA. Kufuatia matokeo ya
kutisha ya kidato cha nne 2012/13.

( http://www.moe.go.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=1731:taarifa-kwa-umma-kuhusu-mitihani-na-upangaji-wa-alama&catid=1:latest-news)
serikali iliona vema kuja na mpango madhubuti wa kuboresha elimu. Na kwa kuanzia, imeripotiwa kuwa kidatao cha nne na cha sita kitatumia mfumo tofauti ama unaofanan na unaotumika vyuoni.

Wakati tukisubiri maoni a wadau na wataalamu mbalimbali, tanki linaonelea vema vema kuonesha mtazamo wake, kama ifuatavo:
1
Ni vema kujua tatizo, kitu ambacho taarifa hiyo ilionyesha kuwa ni zaidi ya ALAMA, kuna swa la mfumo na hata maslahi na waalimu,pamoja na vitendea kazi sahihi. Hii itatupelekea kutibu kiini na sio matokeo. 
2
Tanki linaunga mkono nia ya kutaka kuboresha Tathmini Endelevu ya wanafunzi, na PROJECTS, kama sehemu ya kuboresha elimu na kuwawezesha wanafunzi kujifunza kufikiri zaidi. Hizi ni muhimu sana.
3
Pia,Tanki linakubaliana na kutambua kuwa mwanafunzi aliehudhuria kidato cha nne ama cha sita, sio sawa na asiyehudhuria katika kiwango hico cha elimu, kwa hiyo si sawa kutotambua kiasi alichopata kama ilivokuwa siku za nyuma amabpo mwananfunzi huyo hakupewa cheti zaidi ya utambulisha wa mahudhurio tu. Ni vema wakapewa cheti cha ufuulu wao usioridhisha. Hii hata kwa ngazi ya Vyuo vikuu,ni vema ikaangaliwa, ili mwanafunzi anayefeli katika ngazi ya walau theluthi mbili ya digrii, apewe cheti kinachotambua kiwango hco cha elimu.

HITIMISHO
Elimu Bora ni ile inayotuwezesha kuyamudu mazingira yetu. Vyovyote iwavyo, ni lazima tutambue umuhimu wa MIFUMO na MCHANGO wa WANANCHI WENYEWE katika KUBORESHA elimu. tuitambue ELIMU kuwa ni zaidi ya MADINI. Kuwa na vyeti vingi wa wahitimu na waliofaulu sio ina weza kumaanisha MATOKEO MAKUBWA YA ELIMU, lakini ikawa vilevile ni SUMU KUBWA kwa JAMII. Tunahitaji mfumo unaoweza kuwafanya wananchi wawe ndio wasimamizi wakuu wa ELIMU ya watoto wao na na SERIKALI iwe inawasaidia tu. Badala ya kuwafuata CHINI waliofeli na KUWABEBA, ni vema tuone pia NJIA ya KUWAPANDISHA juu KIUBORA ZAIDI YA KIALAMA.

"TATIZO KUBWA ZAIDI KWA SASA TANZANIA,SI UCHACHE/UWINGI WA WATU WENYE ELIMU,BALI WATU WENYE ELIMU BORA YA KUWEZA KUNUFAISHA FAMILIA ZAO NA NCHI KWA UJUMLA"

0 comments:

Post a Comment