1
Enyi wetu wa zamani,Radhi yenu
niwieni.
Wekeni yenu pembeni,Someni yangu
hewani.
Mimi
sio wa zamani,Napenda jua zamani.
Yangu
haki naamini,Yangu kuweka hewani.
Kwa wote mlo
makini,Yawekeni akilini.
Yeyote mwenye imani, Msingi wake
zamani.
TUMEITUPA ZAMANI, TUTAJUAJE
MBELENI.
2
Ukisahau zamani,Umesahau mbeleni.
Wale walio mbeleni,Wali ijali
zamani.
Mazuri yao zamani,Tuyafanye zetu
mboni.
Mabaya yao zamani,Tusiyatupe chooni.
Tuyaweke vitabuni,Wajifunze wa
mbeleni.
Yasiishie darasani,Yabobee mitaani.
TUMEITUPA ZAMANI, TUTAJUAJE
MBELENI.
3
Mijini na vijijini,Kote kwetu
jamani.
Ni wapi hasa mjini,Hapakuwa
kijijini.
Sisemi toka mjini,Sisemi nenda mjini.
Ukijua muda nini,Hoja iko
akilini.
Mijini Vijijini,Muhimu ni una
nini.
Wangapi tupo mijini,Mizizi si
vijijini?
TUMEITUPA
ZAMANI,TUTAJUAJE MBELENI.
4
Ukiitaka
amani,Waheshimu wa zamani.
Wanayo
mengi madini,Yatufaayo mbeleni.
Hebu
acheni utani,Nafsi sio Madini.
Tumeanza
kiutani,Kuidharau zamani.
Tutaisaka
amani,Ng’ambo nako milimani.
Kurudi
tutatamani,Kusaka hii amani.
TUMEITUPA
ZAMANI,TUTAJUAJE MBELENI.
5
Jamani
yetu zamani,Jamani tuithamini.
Kwa
akili jadilini,Na uwingi umakini.
Mtoe yetu maoni,Ya mwenu hasa
vichwani.
Roho
zetu hatarini,Hili liwe fikirani.
Ujinga tunathamini,Walio juu na
chini.
Akili zetu udini,Afya, chakula
cha nini.
TUMEITUPA ZAMANI, TUTAJUAJE
MBELENI.
6
Elimu iko sokoni,Elimu sasa
vimini.
Mkubwa aseme nini,Mkubwa kawa wa
chini.
Kufoka afoke nani,Kufoka afoke
nini.
Vitabu tena vya nini,Kila kitu
kiganjani.
Kusoma sana kwa nini,Kusoma
faida nini.
Muda wote vijiweni,Ubishini ni
kazini
TUMEITUPA ZAMANI, TUTAJUAJE
MBELENI.
7
Mamia mamilioni,Hoja zetu ni
laini.
Zikitufaa machoni,Si muhimu akilini.
Tazama
mitandaoni,Hakika utabaini.
Asubuhi
na jioni,Tuna hoja milioni.
Kwa makini tathimini,Thamanize huoni.
Kadhaa zenye thamani,Azisomae ni
nani?
TUMEITUPA
ZAMANI,TUTAJUAJE MBELENI.
8
Mazuri
tujadilini,Yajae na akilini.
Ya
kijinga yaacheni,Yafie mwangu kichwani.
Hapo na tutabaini,Tekinolojia
nini.
Wazee wetu zamani,Walijua vya
thamani.
Akili walithamini,Waliacha ya
moyoni.
Tuwajibike jamani,Ndio msingi
makini.
TUMEITUPA
ZAMANI,TUTAJUAJE MBELENI.
9
Ni
nani hasa ni nani,Ambaye yuko makini.
Aturudishe
zamani,Atuongoze mbeleni.
Awe
hasa ukwelini,Atufaye masikini.
Nawaona
wa zamani,Si muoni wa mbeleni.
Najihisi ni motoni,Bora iwe ni
ndotoni.
Subiri
serikalini,Subiri mpaka lini?
TUMEITUPA
ZAMANI, TUTAJUAJE MBELENI.
10
Nina mengi ya kughani,Wachache
watabaini.
Ubovu wa fikirani,Wameishia
njiani,
Hawatasoma ya chini,Ya juu
welevu chini.
Hawasomi
yalo chini,Hawawahi Kanisani.
Sio
wa Misikitini,Sio waenda kazini.
Wao lengo si maoni,Ulumbani
milioni.
TUMEITUPA ZAMANI, TUTAJUAJE
MBELENI.11
Tazama
yangu zamani,Jiulize kuna nini.
Hesabu sio makini,Hata unifanye
nini.
Huniwezi uwanjani,Huniwezi
hasilani.
Wa hesabu themanini,Uwanjani
sifurini.
Amina bingwa jikoni,Amiri bingwa kwayani.
Amina bingwa jikoni,Amiri bingwa kwayani.
Tukifanya mitihani,Sifuri ni
yake nani.
TUMEITUPA ZAMANI,TUTAJUAJE
MBELENI.
12
12
Kwetu ni Uswahilini, Sio huku ushenzini.
Maisha Bora Mbugani, Sio jilunda Mjini.
Tiba Hospitalini, Sio fia Marekani.
Tunairuka zamani,Tudondokee puani.
Tuharibike vichwani,Tumeguke na nyongani.
Tunapenda mitihani,Tunapenda ya
vyetini.
TUMEITUPA ZAMANI, TUTAJUAJE
MBELENI.
13
Hebu mniambieni, Wapi kwetu viwandani.
Waulize wa zamani, Toka kote mikoani.
Walienda viwandani, Wengine maofisini
Kidogo cha mfukoni, Kiliwafaa nyumbani.
Elimu bure shuleni, Usafiri hadi Relini.
Leo Ujinga vichwani,Mabenzi barabarani,
TUMEITUPA ZAMANI, TUTAJUAJE MBELENI.
13
Hebu mniambieni, Wapi kwetu viwandani.
Waulize wa zamani, Toka kote mikoani.
Walienda viwandani, Wengine maofisini
Kidogo cha mfukoni, Kiliwafaa nyumbani.
Elimu bure shuleni, Usafiri hadi Relini.
Leo Ujinga vichwani,Mabenzi barabarani,
TUMEITUPA ZAMANI, TUTAJUAJE MBELENI.
14
Hayatufai jamani,Hayafai
asilani.
Tukikumbuka zamani,Tumetoka
sifurini.
Tujali yetu zamani,Tuwe bora
fikirani.
Watanzania jamani,Ukweli sasa
semeni.
Amani
i hatarini,Ubovu u fikirani.
Serikali hasa nini,Si tutoke
sifurini.
TUMEITUPA ZAMANI, TUTAJUAJE
MBELENI.
15
Viongozi wa zamani,Tuliwapata zamani.
Hapana nyie
bisheni,Imani yangu acheni.
Busara fikirani,Akilini
umakini.
Uongozi una Dini,Daudi na Selemani.
Hakika utabaini,Uongozi
sifa nini.
Kisha mtafakarini,Kura
zatufaa nini.
TUMEITUPA ZAMANI,
TUTAJUAJE MBELENI.
16
Mipango mingi
Bungeni, Kumi asilimiani.
Wakuu wengi
nchini, Masilahiyo mbonini.
Reli zetu za
zamani, Anayeziua nani?
Vipaji vyetu
makini, kavitelekeza nani?
Kiswahili chetu Dini,
Asiyejali ni nani?
Mti fisadi nchini, Aliyeupanda nani?
TUMEITUPA ZAMANI, TUTAJUAJE
MBELENI.
17
Hebu zama kimakini,
Ujue tatizo nini
Walio serikalini, Elimu wao Tisini.
Mengi yetu ya zamani, Wanayasifu surani.
Wayasema jukwaani, Yanawabeba kurani.
Wajapo tu vitendoni, Wameyatupa Kapuni.
Mboni mwao nafsini, Yetu kesho kwao nini?
TUMEITUPA ZAMANI, TUTAJUAJE MBELENI.
18
Ubora tu fikirani,Jibu lililo
makini.
Serikali
isemeni,Serikali i pembeni.
Iwaone
hasirani,Iwakute vitendoni.
Tutokeni
siasani, tujikite kilimoni.
Tukiitwa
jukwaani, tuwaite mashambani
Wakaribishe
nyumbani, Sio mwetu mifukoni
TUMEITUPA
ZAMANI,TUTAJUAJE MBELENI.
19
Uzeeni ujanani, Ujanani uzeeni.
Umakini duniani,Ujanani Uzeeni.
Utusi kwenu nyumbani, Ujikute jalalani.
Ujinga wa ujanani, Utoto wa uzeeni.
Ubora wa Uzeeni, Ubora kesho nyumbani.
Ubinafsi nyumbani, Utumwa wetu mbeleni.
TUMEITUPA
ZAMANI,TUTAJUAJE MBELENI
20
Ninamuomba
manani,Afumbue zetu Mboni.
Tuelewe
ya zamani, Yatufae kwa mbeleni.
Yasitutie
vitani, Yatutoe sifurini.
Tuwapate
makuhani, Kama Musa na Haruni.
Wasije
mahayawani, Wenye nuko nafsini.
Tuboreke
fikirani, Tuone chele pumbani
TUMEITUPA
ZAMANI,TUTAJUAJE MBELENI
Ama kweli ZaMaNi inapendeza Zamani hata mapenzi yalikuwa zamani, kuwajibika zamani kwa kila mwenye shughuli yake, malezi yalikuwa zamani baba aliwajibika na mama pia, thamani ya kila mtu ndugu jamaa marafiki jirani nk ilikuwa zamani hata thamani ya mpangaji kwa mwenye nyumba ilikuwa zamani.
ReplyDeletenimeipenda na kupenda mengi ya zamani.
Asante sana bro.
Nashukuru sana! Usiitupe zamani,Yako uipe thamani. Uifanyie ya ndani, ikuongoze mbeleni.
Delete