Wednesday, September 11, 2013

MADAWA YA KULEVYA-KULIKONI TANZANIA?

Madawa yenye kulevya, Nahisi Yametulevya.
Juma Sala na Kaluvya, Hakuna yasomlevya.
Tulilamba tukachovya, Tunajidunga  kilevya.


Akili yamezilevya, Fikira yamezilevya.
Mipango yameilevya, Juhudi yamezilevya.
Wajibu yameulevya, Hakize yamezilevya

Kilimo yamekilevya, Sayansi yameilevya
Afya yameilevya, Elimu yameilevya
Majenzi yameyalevya, Safiri yamezilevya
Kweli madawa yalevya, Na Jumla Yametulevya.

Tamaduni yamelevya, Katiba yameilevya.
Bunge yamelilevya, Siasa yameilevya.
Uongozi yamelevya, Madaraka yamelevya

Mahakama yamelevya, majeshi yameyalevya
Wizara yamezilevya, Balozi yamezilevya.
Habari yamezilevya, Mitandao yamelevya

Mipira yameilevya,Riadha yameilevya.
Masumbwi Yameyalevya, Mdako yameulevya.
Muziki yameulevya, Sinema yamezilevya
Kweli madawa yalevya, Na Jumla Yametulevya.

Vijana yanawalevya, Wazee yaliwalevya
Watoto yatawalevya, Wakubwa yamawalevya
Masikini yalevya, Tajiri anayalevya

Hata wewe yakulevya,Hata mimi yanilevya
Jirani yamemlevya, Fulani yamemlevya
Zanzibar yawalevya, Tanganyika yatulevya

Zamani tuliyalevya, Si leo yanatulevya
Dunia imetulevya, Tayari yametulevya
Ukweli yanauvivya, Moja tano yatulevya
Kweli madawa yalevya, Na Jumla Yametulevya.

Related Posts:

  • Udhibiti wa Idadi ya Wachezaji wa Kigeni Ligi Kuu Tanzania Bara Maamuzi ni vema Yakazingatia vizuri WAKATI WETU. Kama nimeelewa hoja, ni kuwa kwa kuwapunguza wachezaji wa kigeni walau kwa asilimia walau 50, kuna uwezekano tukaongeza nafasi ya wachezaji wa nyumbani kupata nafasi katika ti… Read More
  •  MPAJU WEEK 2020“JAMII YETU-KIOO CHETU” Kauli mbiu ya Mpaju Week 2020 ni JAMII YETU NDIO KIOO CHETU. Mpaju SC inaamini changamoto zinazoizunguka jamii yetu zinatokana na kushindwa KWETU kuzitatua. Mpaju SC inaikifikishi… Read More
  • Ziara ya Mpaju SC Shule ya Msingi Mpolo 2020 haitasahaulikaKwa mara nyingine, Siku ya Jumamosi tarehe 29 Agosti 2020, Mpaju SC walitembelea shule ya Msingi Mpolo iliyopo Mbalali na kufanya michezo kadhaa ya kirafiki. Hii shule yenye hazina kubwa sana ya Michezo ya nchi hii. Mpaju ime… Read More
  •  MPAJU WEEK 2020(Disemba 15-22)Uwanja wa Magereza Chuo-Ruanda Mbeyanani kufungua Dimba timu za wasichana?MPAJU FCVS SUPER EAGLES Mpaju FCSUPER EAGLE… Read More
  • WADAU WA SOKA JIJINI MBEYA WAFURAHIA MPAJU WEEK 2019 Washuhudia Mambo Mengi: Vipaji vikali, Uongozi Madhubuti wa Mpira Mbeya Mjini,  Ushirikiano wa wadau wa Mpaju SC na bila kusahau, Timu ya wasichana ya shule ya msingi ya Mpolo-Mbalali, Uso kwa Uso na Mdau mkubwa w… Read More

2 comments:

  1. Kwa mashahiri hakika uko mahiri, toka lile shahiri,
    hakika ya zamani mahiri, hakika wewe siyo bahiri,
    Mungu akujaze umahiri, ufaulu wako uwe mzuri,
    KILA LA HERI MUNGU AKUPE HERI.

    ReplyDelete
  2. Nashukuru kwa comment, kwa Shairi u mecomment
    kwa vina umecement, kuihakiki comment
    Na kesho ukicomment, mizani mia cement
    comment jina cement, comment jenga comment

    ReplyDelete