Baada ya kuona maswala ya SIASA siyaelewi kabisa (Hasa kwenye mchakato wa katiba), nikaona nifungue kidogo Falsafa na Sayansi ya mambo ya Kisiasa. Nikajifunza mengi tu na kwa kifupi, nikaona kuwa mambo yahusuyo taratibu tulizonazo kama KUUNDA KATIBA wanaweza kutusaidia wataalamu hawa kabisa,
ikiwemo na kutupatia muongozo wa nini kifuate baada ya kipi, kama tutaamua kwenda kwa stepu!
Baada ya kuuliza hapa na pale, nikasikia wataalamu walipewa nafasi wakatoa mawazo mengi likiwemo la MUUNDO WA SERIKALI/MUUNGANO UNAOTUFAA KUWA NI -WA MOJA-:
Sasa, kila kukicha Mara UKAWA,mara MBILI, mara TATU! Jamani, kwani hatuwezi KUWAITA TENA wakatuelezea wananchi MBELE YA BUNGE ili, wanaobisha nao wawabishie KWA hoja! Kuna maana gani ya kukaa tunapoteza PESA ZA WAKULIMA, kusomesha watu halafu wakiwa tayari kutumikia taifa, tunawaambia WABAKI na mambo yao ya VITABUNI? Kama wanatudanganya, waadhibiwe basi!
Wakati umefika, tuheshimu ya VITABUNI, hata kwa kujitahidi KUYAKARIBIA TU. Naamini, Hivyo ndivyo wenzetu walivyofanya na kufanikiwa. Mimi naamini kama kweli SIASA ni UTAALAMU, lazima JIBU LIKO MOJA LINALOTUFAA, NA kushindwa KULIPATA, ndio kunapelekea mabishano, kwa SABABU kama penye UKWELI UONGO HUJITENGA, basi penye UONGO, UKWELI pia HUJITENGA. Sasa kwenye mambo ya MAANA hatupaswi kucheza PATAPOTEA, tufuate watu wenye HIYO TAALUMA kwanza!
Monday, May 19, 2014
Home »
» "Penye UONGO, UKWELI pia HUJITENGA"
"Penye UONGO, UKWELI pia HUJITENGA"
Monday, May 19, 2014
No comments
Related Posts:
MPAJU FC YAKAMILISHA USHIRIKI WA TASCA CUP MPAJU WEEK 2021 IKO PALE PALEMpaka sasa wadau wa soka wa Mkoa wa Mbeya wanajiuliza kulikoni, Mwaka huu hakuna Mpaju Week 2021 au Mpaju Day 2021? Jibu ni kuwa Kituo cha Mpaju SC kimekuwa katika ushiriki wa TASCA CU… Read More
LIGI YA MKOA MBEYA- MPIRA WA MIGUU KWA WANAWAKE MPAJU FC (ATINISU) WAANZA VEMA Waifunga Kyela Queens 2-1. NEEMA RAPHAEL (POGBA) ( Wa Tatu kutoka Kulia,waliosimama) NA YACINTA (YANTE) (Wa Pili kutoka Kulia,waliopiga goti) ndio waliopeleka tahadhari Kyela le… Read More
Wanasoka Wafurika Uwanja wa Sokoine Kutoa Pole Kwa MATHIAS GERALD MDAMU(Baadhi ya Matukio yahusuyo Mpaju FC)Michezo ya hisani Yapigwa, Timu ya Taifa ya Ilemi 1- Mbeya All Stars 0NaMpaju FC 2-ICON FC 0Wachezaji wa Mpaju wakiwa katka picha ya pamoja na wachezaji wa MBEYA ALL STARS, waka… Read More
MPAJU CUP 2021 YAMUENZI BABA WA TAIFA- JK NYERERE MASHINDANO YAFUNGWA SIKU YA TAREHE 14 OCTOBA 2021Refa FRANCIS (Kijana Mdogo Kabisa) akiwakagua wachezaji kabla ya mchezo-Uwanja wa Ilemi ChuoPICHA YA PAMOJA YA WALIMU NA WACHEZAJI KTUOKA TIMU ZILIZOSHIRIKI NEW TALENT U… Read More
GRACE FC CUP MBEYA 2021MPAJU FC U-15 YATWAA UBINGWA KIBABE YAICHAPA NEW TALENT ACADEMY 3-0Mwenyekiti wa Mpira Wilaya Mzee Gondwe akikabidhi Jezi na Mpira kwa Mabingwa wa Grace Cup 2021-Mpaju FC U-15.Picha ya Pamoja ya Mpaju Fc, New Talent… Read More
0 comments:
Post a Comment