Nini hasa yako ndoto, Yangu niwepo Khatari
Leo nimeota ndoto, Niko nchini Khatari
Bado damu yangu moto, Napiga pamba hatari
Sema yako wewe ndoto, Ona Mbali tafakari
Wengi wetu tuna ndoto, Utajiri tukithiri.
Tuselebuke na toto, Wajue chetu kiburi.
Wafe kama viroboto, Sisi tuzidi nawiri.
Nini hasa yako
ndoto, Yangu niwepo Khatari
Miaka nane si
mbali,Bulata kisha kubali.
Yeye ndiye
lijabali, Ya rushwa sitajadili.
Niwaone Brazili,Laivu
naikubali.
Hilisitaki jadili,
Uswahili sikubali.
Nikivua kandambili,
Jua ninaenda mabli.
Ndoto kanipa
jalali, Sijapata kwa kamali.
Nini hasa yako ndoto, Yangu niwepo Khatari
Sitaki
kuabudiwa,Kesho niwe kwenye moto
Ama mfisadi
kuwa, Nchi kuitia moto.
Vyao watu
kunyakuwa,Kulimbikiza vipato.
Sito yauza madawa, Kinga wakose watoto.
Sitaki mimi chachawa, Dunia mengi mapito.
Hata kama nimenawa, Chakula bado cha moto.
Nini hasa yako
ndoto, Yangu niwepo Khatari
Mungu atupe neema, Kipato kilicho safi.
Tupate Hija
salama,Roho zizidi usafi.
Timize ndoto karima, Nyunyiza wake usafi.
Tuziote ndoto
njema, Ziso utaka Ulafi.
Tusibaki
kukoroma, Vitambini tusosafi
Tuwaote Wakulima,Wasovuna
Mikomafi.
Nini hasa yako ndoto, Yangu niwepo Khatari
0 comments:
Post a Comment