Ukimchukulia mtoto mdogo kabisa
anayezaliwa! Unaweza kusema hajui kitu na pengine ni sawa kusema hana Tatizo!
Lakini ukijaribu kufikiria unaweza kuona kuwa tayari mtoto ana shida kama vile
Njaa,baridi
ama joto na kadhalika! Haya ni yale ya kawaida, lakini yako pia ya Muumba ya kibaiolojia Zaidi.
ama joto na kadhalika! Haya ni yale ya kawaida, lakini yako pia ya Muumba ya kibaiolojia Zaidi.
Kwangu mimi, Tatizo, ni hali ama
jambo, mtu anahitaji kuishughulikia ili asonge mbele kimaisha kwa namna aonavyo
atapata ubora Zaidi wa kimaisha, kwa kutumia rasimali asizoweza kuzipata
kirahisi.Tatizo mara nyingi ni hali
tunayoiambatanisha na ugumu wa kutatua kinachotutatiza ama shida. Kwa
msingi huo, mtoto pia ana shida za msingi, ambazo ndio ubinadamu wake, na mara
nyingi huwa kuna suluhu kadhaa rahisi zisizotatiza, ama kutoka kwa mwenyezi
mungu ama kutokana na asili, ukiongeza na utashi kiasi wa binadamu, hakuna
tatizo kuzimudu shida/matatizo hayo.
Sasa kwa nini tunayatafuta
matatizo? Kwanza, ili kuweza kusonga mbele kama nilivyogusia kwenye maana. Pili
huwa ni kwa ajili ya udhaifu tu wa kibanadamu, pengine kutojua kama shida aliyonayo
ni ya msingi na muhimu kwake,matokeo yake anaboronga kuishughulikia na kuifanya
ni tatizo, na nafikiri hapa ndio kwenye tatizo letu. Lakini, pia hulka, kama
vile ubinafsi na ulafi. Hivi pia hupelekea mtu
kutaka apate kupindukia, pengine mpaka akaiba na kadhalika. Kwa hii
sababu ya kwanza, kila mtu inabidi ama anaifanya kwa kukamilisha ubinadamu,
maana nafikiri ni agizo la muumba.
Yaani, unapaswa kuyasaka matatizo
yako, kuyatatua, hata kama ni kwa kuomba msaada wa muumba, huko ndio kuishi.
Inasemekana tulikwisha muuzi Muumba, hivyo akatoa kama adhabu, hivyo kama hatuna
hizo shida hatupo duniani, na kuzilalamikia si sahihi, bali tunapaswa
kuzifurahia, kwa sababmu Mungu anatupenda hawezi kutupatia sumu hata kama ni
adhabu, ina lengo zuri. Shida ama Matatizo ya msingi ni Rasilimali kwa mtu makini.
Sasa, utakuta, hatushughuliki na matatizo
ya msingi (hayo ya sababu ya kwanza), ambayo rasilimali kwa kiasi kikubwa
tunazo, na tunaweza kuyatatua,na kwa kufanya hivyo tunakuwa tunasonga mbele,
bila kupata tatizo. Badala yake huwa tunajikita kutaka mambo yawe makubwa
kuliko rasilimali tulizonazo (hayo mengine, na yale ujuayo wewe). Hapo ndio
kuyatafuta matatizo sasa niongeleako.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Itaendelea,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
0 comments:
Post a Comment