Wednesday, September 11, 2013

MADAWA YA KULEVYA-KULIKONI TANZANIA?

Madawa yenye kulevya, Nahisi Yametulevya.
Juma Sala na Kaluvya, Hakuna yasomlevya.
Tulilamba tukachovya, Tunajidunga  kilevya.


Akili yamezilevya, Fikira yamezilevya.
Mipango yameilevya, Juhudi yamezilevya.
Wajibu yameulevya, Hakize yamezilevya

Kilimo yamekilevya, Sayansi yameilevya
Afya yameilevya, Elimu yameilevya
Majenzi yameyalevya, Safiri yamezilevya
Kweli madawa yalevya, Na Jumla Yametulevya.

Tamaduni yamelevya, Katiba yameilevya.
Bunge yamelilevya, Siasa yameilevya.
Uongozi yamelevya, Madaraka yamelevya

Mahakama yamelevya, majeshi yameyalevya
Wizara yamezilevya, Balozi yamezilevya.
Habari yamezilevya, Mitandao yamelevya

Mipira yameilevya,Riadha yameilevya.
Masumbwi Yameyalevya, Mdako yameulevya.
Muziki yameulevya, Sinema yamezilevya
Kweli madawa yalevya, Na Jumla Yametulevya.

Vijana yanawalevya, Wazee yaliwalevya
Watoto yatawalevya, Wakubwa yamawalevya
Masikini yalevya, Tajiri anayalevya

Hata wewe yakulevya,Hata mimi yanilevya
Jirani yamemlevya, Fulani yamemlevya
Zanzibar yawalevya, Tanganyika yatulevya

Zamani tuliyalevya, Si leo yanatulevya
Dunia imetulevya, Tayari yametulevya
Ukweli yanauvivya, Moja tano yatulevya
Kweli madawa yalevya, Na Jumla Yametulevya.

2 comments:

  1. Kwa mashahiri hakika uko mahiri, toka lile shahiri,
    hakika ya zamani mahiri, hakika wewe siyo bahiri,
    Mungu akujaze umahiri, ufaulu wako uwe mzuri,
    KILA LA HERI MUNGU AKUPE HERI.

    ReplyDelete
  2. Nashukuru kwa comment, kwa Shairi u mecomment
    kwa vina umecement, kuihakiki comment
    Na kesho ukicomment, mizani mia cement
    comment jina cement, comment jenga comment

    ReplyDelete