Monday, December 28, 2020

Mpaju Week 2020-YAWA CHACHU KWA SOKA LA WANAWAKE MBEYA

Mpaju Week 2020 yaleta matumaini ya SOKA LA WANAWAKE MBEYA: Tamasha hili lenye KAULI MBIU YA JAMII YETU NDIO KIOO CHETU, lilifikia tamati siku ya Jumanne tarehe 22 Disemba 2020 pale Uwanja wa Chuo cha Magereza Mbeya, kuwakaribisha wenyeji kutoka Mkoa wa Momba-Tunduma

timu ya ijana wa miaka 17 na 15 ya Super Power. Timu Hii yenye vijana wengi wenye uwezo, ilipewa nafasi ya kucheza na timu za Super Eagle,Mpaju Fc na Magereza kama sehemu ya Kufunga Tamasha hili. Hiyo ni TISA, kumi ni burudani na ushindani ulijitokeza baina ya timu za Wasichana kutoka Tukuyu,Garijembe na Mbeya Mjini. Pamoja na Timu za ICON na TUKUYU QUEENS kuonekana kuwa majabali katika mitanange ya timu za wasichana, bado Mbeya Soccer, Zunya Queens, Super Eagle na Mpaju FC a.k.a ATINISU hawakuwa nyuma kimapambano. Tamasha hili linakuwa Kati ya matamasha Bora yaliyowahi kufanyika kwa timu za wasichana hapa Mbeya Mjini kwa kuhusisha timu kutoka maeneo zaidi ya Mbeya Mjini. Ni matumaini ya wadau wa SOKA mbeya kuwa matokeo chanya ya Tamasha hili yataendelezwa kwa kuwepo ligi ya Mpira wa Miguu kwa timu za wasichana mkoa wa Mbeya. Matukio zaidi ni kama picha zinvyoonyesha.


Mpaju FC (W) a.k.a ATINISU

Tukuyu Queens

Mbeya Soccer (W)

Zunya Queens (Garijembe)

ICON FC (W)


Ilemi Youth U-12 wakishangilia baada ya kushinda moja ya Mechi zao 

Ilemi Youth U-12

Magereza U-15

Mpaju FC U-12

Mtoni Junior U-12 and U-15

Super Eagle U-15

Mpaju Fc U-15

Kocha Ali Mkumbukwa wa Mpaju FC akiongea na Mpaju FC (W) a.k.a ATINISU

Kocha Juma Ahmed Mpangule akiongea na wachezaji wa Mpaju U-12
MPAJU FC na ICON FC
Mpaju U-12 na Mtoni Junior U-12
Mpaju U-15 na Super Eagle U-15
Waalimu wakifurahi baada ya Michezo kwa kujikumbusha mambo kadhaa wakati wa Kozi yao ya INTERMEDIATE
Kucha Mubeshi (Kushoto) na Andrew (Kulia) wakimzawadia Kiongozi wa Mpaju SC kwa kuandaa
tamasha la Mpaju Week 2020

0 comments:

Post a Comment