Saturday, April 30, 2022

MPAJU FC (ATINISU) WAWAFUNGA ICON FC GOLI MBILI BILA MAJIBU (2-0)

WAMALIZA LIGI YA MKOA - MBEYA KWA KISHINDO

(Magoli yalifungwa na Zainabu Mwambole kwa Penati na Grace Saanane Kutokana na Kona)

Mpaju FC Atinisu wakisalimiana na Icon Fc kabla ya kuanza Mchezo

Walimu wa Mpaju FC Atinisu (David Saimoni-Aliyesimama) na (Ali Mkumbukwa-Aliyeinama) wakitoa uchambuzi wa kipindi cha Kwanza na kuelekeza nini kifanyike Kipindi Cha Pili ili kuhakikisha wanapata ushindi

Juma Mpangule-Meneja wa Mpaju FC akifuatilia kwa makini Maelekezo ya Kocha David Saimoni

USHIRIKI WA MPAJU KWA KIFUPI

Mpaju FC wamefanikiwa kumaliza mashindano wakiwa wamepoteza Michezo Miwili. Wa Kwanza Kupoteza ni ule mchezo Dhidi ya ICON FC pale Iyunga, na wa pili ni dhidi ya Kyela Queens Pale uwanja Mwakangale-Kyela. 

Mpaju FC a.k.a ATINISU wamedhihirsha kuwa kati ya Timu za kuogopwa hivi sasa hapa Mbeya Baada ya kupata ushindi wa goli 2-1, kwa mechi ya Kwanza dhidi ya Kyela na ushindi wa 2-0 leo dhidi ya ICON FC. Ukilinganisha na Miaka ya nyuma, Mpaju FC wamefanikiwa Kuongeza Vitu vingi sana kiushindi na uchezaji. Ubora wa Timu umeonekana kuwa wa hali ya juu, kiasi cha mashabiki wengi wa soka kutoamini kama ni Mpaju FC na wengi pia kusikitishwa sana pale timu hii ilipopoteza. Mashabiki waliohudhuria Mwakangale na Iyunga wanaweza kuthibitisha hili. Kwa ujumla ubora huu unatokana na Ukweli kuwa Wachezaji wa Mpaju FC Msimu huu wengi waliwahi kucheza ICON, na hivyo ni wenye ujuzi na uzoefu wa hali ya juu. Usajili huu wa Mpaju FC umeongeza chachu katika Mpira wa Wanawake Mbeya kwa kufanya mchezo baina ya timu hizi kutoa Hali halisi ya DERBY ya Mbeya kwa mpira wa  miguu kwa Wanawake.

Kimsingi ICON FC wanastahili Pongezi kwa Kuchangia kwa kiwango hiki katika Mpira wa wanawake Mbeya. Pongezi nyingi pia ni kwa Mwalimu David Saimoni kwa kuweza kuhakikisha vijana wanaungana na kuonyesha mpira mzuri na nidhamu ya hali ya juu. Mpaju FC imekuwa Gumzo kila Uwanja kwa kusakata Soka safi na Nidhamu kubwa kabisa.

Uongozi wa Mpira Mkoa wa Mbeya unastahili pongezi kwa jitahada kubwa na uvumilivu wao katika kuhakikisha timu hizi ambazo ni changa zinafanikiwa kushiriki mashindano haya. Kila kheri kwa timu itakayofanikiwa kupata nafasi ya kuwakilisha Mkoa wa Mbeya katika ngazi ya Taifa.

HONGERA MPAJU FC HONGERA ATINISU

Hakika 

Huu ni Mwanzo Mpya

Hakika

BURUHANI INA MAMLAKA



2 comments: