WA-BONGO TUPUNGUZE KUSHABIKIA SHEREHE ZENYE
TIJA NDOGO
KWA TAIFA LETU
"MWANAMKE NA MWANAUME WOTE MUHIMU NA KILA MTU ANA HAKI ZAKE NA WAJIBU WAKE, TUSIDANGANYIKE"
Badi Abu Al-farouq
akijibu kupitia ukurasa wake wa “Facebook” wenye mafunzo mengi sana ya DINI YA
KIISLAMU alisema ,“ Juma
Mpangule
uislamu umemtukuza sana mwanamke Alikuja mtu kwa Mtume wa
Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Ewe Mjumbe wa Allah! Ni
nani mwenye haki zaidi miongoni mwa watu kwa mimi kusuhubiana naye kwa wema?”
Akasema: “Mamako”. Akasema: “Kisha
nani?” Akasema: “Mamako”. Akasema: “Kisha
nani?” Akasema: “Mamako”. Akasema: “Kisha nani?” Akasema (Swalla Allaahu
‘alayhi wa sallam): “Babako” (al-Bukhaariy na Muslim). Hata wazazi wako
unapowapa msaada pesa za mama lazma ziwe nyingi kuliko utakazo mpa baba yako
sasa
waanzilishi wa siku ya wanawake sijui malengo yao yalikuwa ni nini hivyo
sitokuwa na jibu la moja kwa moja na mtume(s.a.w) anasema "acha lenye
kukutia shaka uliendee usilo na shaka nalo"mie nakushauri usisubiri leo tu
kila siku watakiwa umtukuze mama yako,dada zako na watoto wako wa kike........”.
Naamini,hata
katika dini zingine,majibu yanaweza kutofautiana maneno,lakini yakawa na maana
sawa kabisa na hii. Kikubwa hapa sio kwa sababu dini imeongea hivyo, basi TANKI
nalo,limepata cha kuongezea, la hasha! Mtazamo wa TANKI kidogo uko tofauti,ila huwa
ni vizuri kabla hujakubaliana na mawazo yako siku zote kujaribu kuangalia MUNGU
anasema nini! Hiyo itakupa uhakika au nafasi ya kutafakari upya juu ya mtazamo
wako!
SHEREHE
ya wanawake dunia, ina historia ndefu sana, tokea nyakati za ukomunisti
miaka ya 1900. Na walionzisha hasa walikuwa wanalenga madai mbalimbali
ya wanawake kama vile kuruhusiwa kupiga kura. Nchi nyingi kubwa dunia zilikubaliana
na sherehe hii,japo kuna wakati ilichukuliwa kama sikukuu ya wafanyakazi kwa wanawake, au siku ya kimama
duniani na hata kufikia kuchanganywa na siku ya wapendanao dunia kwenye baadhi
ya nchi.Hii ilitokana na kubadilika kwa malengo katika kila nchi na kulingana
na wakati, mpaka kufikia kama leo kuwa zaidi ni kumpatia mwanamke zawadi na
kumuonyesha kuwa unampenda japo kwa kutamka! Ni jambo zuri kumpenda na kumjali
mwanadamu mwenzio hasa mwanamke! (http://en.wikipedia.org/wiki/International_Women%27s_Day)
Kuna mambo
kadhaa ambayo ni vema watanzania kama nchi yenye lundo la
umasikini,tukayaangalia kulingana na sherehe za namna hii!
- Sherehe ni kwa ajili ya nini hasa? Wakati sherehe hizi zikiendelea kuboreshwa ilichukuliwa kuwa ni kumpongeza mwanamke kwa hatua yake katika maendeleo kwa ujumla. Sasa kwa ujumla imebaki kupongezana kwa kupeana hongera na maneno matamu. Nafikiri kuna umuhimu wa pia kujua uwajibikaji na maendeleo yaliyofikiwa na wanawake. Kwa kwetu Tanzania, wengi tunaambatanisha sherehe hii na kukumbushana juu ya kupunguza mfumo DUME juu ya wanawake. Hatuongelei sana juu ya uwajibika wa wanawake, na hatuongelei kabisa mafao ya taifa juu ya sherehe hii ya wanawake.Watanzania tuna tabia ya kupenda sana starehe kuliko kazi (Profesa J). Leo birthdays zimeshika hatamu mpaka kadi kama harusi, mara kidogo mwanamke duniani , siku si nyingi tutasikia siku ya mama duniani , tayari tumemaliza valentine, nayo ilianza kama utani,watu wawili, watatu mpaka karibia inakuwa ya kitaifa.Hapo kutakuwa na sherehe ya MKULIMA kweli?
- Haki gani zinazozungumziwa? Haki za mwanamke, lazima ziheshimiwe. Hilo halina ubishi,lakini ikumbukwe kuwa lengo la kuheshimu na kulinda haki ni kuongeza uwajibikaji na maendeleo ya mtu au kundi husika na Taifa kwa ujumla. Na hizo haki, sio maana yake kila kitu kiwe sawa! Yaani kuna nchi duniani leo Wazazi wanawaogopa watoto zao, sasa hii ni haki ya mtoto au kuwaonea Wazazi? Mambo yanayopaswa kuboreshwa yaboreshwe,kama kuzuia baadhi ya mila ambazo kwa wakati huu tunaweza kabisa kukubaliana kuwa zina madhara zaidi kwa Taifa kuliko faida, mfano ni zile za kutupa watoto mapacha. Lakini, na pale ambapo mwanamke hapaswi kuwa sawa na mwanaume tumwambie mwanamke na aelewe. Ifike hatua sasa tuongee kama wamoja,kuwa WANAUME NA WANAWAKE tumeumbwa tofauti,hivyo mwanaume abaki kuwa mwanaume na atimize wajibu wake,na mwanamke abaki kuwa mwanamke na atimize wajibu wake. Hakuna aliye muhimu zaidi ya mwenzie,ila ni mgawanyo tu wa asili wa uwajibikaji. Kuwa na viti sawa bungeni,sidhani kama ndio haki tunayoihitaji hapa!
- MWISHO NA RAI JUU YA HILI! Watanzania tuache kudumisha sherehe ambazo hazina tija kubwa kwa taifa, badala yake tuzipe kipaumbele zile zenye maslahi ya kitaifa, kama vile sikukuu ya WAKULIMA. Mwanamke apewe heshima na upendo kila siku, na haki ambazo zinaendana na UANAMKE WAKE,sio kumpa USAWA NA MWANAUME ndio kumkomboa,na zaidi hii inaligharimu taifa kwa kulazimisha wanawake kuingia hata sehemu ambazo ufanisi wao hauwi mkubwa na kuzuia nafasi ambayo mwanaume angefanya vizuri zaidi. Hii haina TIJA kwa taifa letu ambalo bado ni changa,hivyo linahitaji kila mtu kuwajibika hata kwa viboko katika eneo lake. Inapotokea mwanaume anafanya mambo ya wanawake,huo ni UPUNGUFU/KILEMA tu, na tusigeuze kuwa ni HAKI ya wanaume, na wanawake pia hivyo hivyo. Hata hivyo, Kwa kutambua umuhimu wa kukumbushana juu ya mwanamke kitaifa, basi zote hizi sherehe zinazohusiana na upendo,tuzitumbukize kwenye FAMILY DAY. NGUMU KUISEMA HII,UNAWEZA KUPEWA TALAKA NA LAANA KWA MPIGO! hahahahahahahahahaha........!
0 comments:
Post a Comment