“ENYI WANANGU WAWILI,
TANGANYIKA ZANZIBARI”
Kweli
mwanangu Akili, Hebu mwanangu fikiri.
Fiki
mwanangu wa pili,Nawe mwanangu subiri.
Nyie
wanangu wawili,Msifanye ya Bakiri.
ENYI
WANANGU WAWILI,TANGANYIKA ZANZIBARI.
Kawa
mwanangu Wakili, Kawa kiburi Bakiri.
Kawa mwanangu
fedhuli, Kawa utu ufahari.
Hata
muwe Wahadhili, Hakiwafai Kiburi.
ENYI
WANANGU WAWILI, TANGANYIKA ZANZIBARI.
Haya
yenu maadili, Mema kwenu nabashiri.
Japo
hampo kamili,Mko wanangu vizuri.
Wanangu
msikalili,Mkawa ka’ matairi.
ENYI
WANANGU WAWILI, TANGANYIKA ZANZIBARI.
Mzitumie
akili,Msisahau fikiri.
Kukuza
zenu akili,Msome bila kiburi.
Msiwe
mabaladhuli,Msipende ufahari.
ENYI
WANANGU WAWILI, TANGANYIKA ZANZIBARI.
Zisiwazidi
akili,Zikawazidi na shari.
Muwe
na stahamili,Muwe na kujihariri.
Mjenge
na mihimili,Mpate na utajiri.
ENYI
WANANGU WAWILI, TANGANYIKA ZANZIBARI.
Asije
kwenu Wakili,Na Amani ikithiri.
Ugomvi
wenu wawili,Mwenzenu anasubiri.
Udini
kwenu batili,Ukabila iwe shari.
ENYI
WANANGU WAWILI, TANGANYIKA ZANZIBARI.
Kenya hata
kule mbali,Msikilize habari.
Tanzania Swali Sali,Swali Sali Zanzibari.
Dhulumu
iwe batili,Isiwape utajiri.
ENYI
WANANGU WAWILI, TANGANYIKA ZANZIBARI.
Ya moyoni
yawe mbali,Ya akili yakithiri.
Akili
ni muhimili,Akili tungi la shari.
Msijifanye
viburi,Mkatupa ushauri.
ENYI
WANANGU WAWILI, TANGANYIKA ZANZIBARI.
Hakuna
kuwa kamili,Mpaka kwenye Kaburi.
Fikra
nawe Akili,Muda hauwasubiri.
Jioni
kwangu kamili,Maswali sitosubiri.
ENYI
WANANGU WAWILI,TANGANYIKA ZANZIBARI.
0 comments:
Post a Comment