Friday, March 29, 2013

KATIBA YETU MPYA TUIPIMEJE UBORA WAKE?



 " IWE NA UWEZO WA KUTUFANYA 
TUUOGOPE UONGOZI , TUPENDE KUFANYA KAZI NA TULIPENDE TAIFA LETU KULIKO KITU KINGINE CHOCHOTE"

Maana yeyote ambayo mtu atatoa kuhusu katiba inaweza kwa namna moja au nyingine ikaangukia kwenye maana ya kuwa KATIBA ni MAKUBALIONA JUU YA MWONGOZO WA JAMII AU TAIFA FULANI. Huwa ni MSINGI wa MUAFAKA katika UTAWALAJI na UENDESHAJI, wa TAIFA au JAMII husika, na hata kikundi katika kufikia Mafaniko Bora. Pengine kutokana na uzito wake ndio
maana huitwa SHERIA MAMA. japo uzito wake ni zaidi ya sheria, labda iitwe DIRA MAMA, hasa kwa nchi masikini kama Tanzania.Katiba inatakiwa kuwa na ubora wa mama bora.


Kama ni makubaliano au muafaka basi maana yake kuna kutokubaliana au kutoafikiana kabla yake. Sasa TANKI linashauri mambo yafuatayo katika kutafakari juu ya uboreshaji na uandaaji wa  KATIBA mpya ya TANZANIA

1.       Tutambue ni YAPI hatuafikiani na YALE tunayoafikiana. Maoni mengi yanayotolewa yanaweza kutusaidia kulitatua hili, kama tutayachuja na kuyatafakari vizuri.

2.       Tatambue TUNAYOYATAKA na YANAYOTUFAA. Hapa ni tatizo kwa sababu kila mtu ana analolitaka. Katiba SI lazima iwe na UNAYOYATAKA, ila ni vema ikawa na TUNAYOYATAKA YANAYOTUFAA. Hapa kuna “kimbembe”, maana ZAMA hizi hata wengi wanaweza kuwa wajinga, kwa sababu PESA ndio INAYOONGEA na KUFIKIRI badala ya VICHWA. Hivyo Maoni yanayokusanywa, yanahitaji WATANZANIA WOTE wayatambue hayo na kuafikiana kuwa ndio hasa wanayoyataka na yanayowafaa. Kwa kuwa hilo ni gumu, WAWAKILISHI wao lazima wawe na sifa SAHIHI za uwakilishi wa WATANZANIA. Hii inatupelekea kuhitaji Mchakato sahihi wa kupata wawakilishi wa kushughulikia KATIBA. KWA nchi ya kidemokrasia mara nyingi KURA ndio muamuzi, basi WAWAKILISHI HAWA wagombee na kupigiwa kura!

3.       Tukubali kuwa hatuwezi KUJIHUKUMU bila kujipendelea, hivyo ni vema mtazamo uwe kuwa sisi wote tuko upande mmoja na MSINGI huu tunauweka ili wa upande wa pili ambao TUNATOFAUTIANA na ndio WATAPATA nafasi ya KUTAWALA NA KUONGOZA JAMII YETU,waweze kuufuata bila matatizo na UTUNUFAISHE SISI. Hivyo KATIBA tunaiandaa ili wasitudhulu na itunufaishe. Mfano: Tufikirie kuwa tumeamua kuwaita Wakoloni waje tena kututawala, kwa kuwa siku za nyuma waliona si vema kujenga nchini kwetu, basi katiba tunaiandaa ili iwaamuru kujenga nchini mwetu. Hili hatuwezi kulipata kama ndani ya UWAKILISHI pia kuna wakoloni au mamluki wa wakoloni au kuna wawakilishi wenye FIKRA MBOVU.

4. Katiba, ni Muhimu ikawa na uwezo wa KUJILINDA na KUJIBORESHA kwa siku za USONI. Kwa kuwa katiba sio kama VITABU vya DINI, tunatarajia siku moja, KUTOKANA na mabadiliko ya DUNIA, mahitaji ya WATANZANIA yatahitaji TARATIBU tofauti. Sasa kama katiba tunayoiandaa haitakuwa na UWEZO wa kuhakikisha MAZURI yake hayakiukwi kwa HATA kipengere kidogo, na kama haitakuwa na UWEZO wa KUJIUNDIA MCHAKATO BORA ZAIDI, inaweza kupelekea KUTOFIKIA manufaa TARAJIWA ya katiba MPYA IANDALIWAYO wakati wowote ule.

KIFUPI: Katiba haipaswi kuwa na UWASTANI bali UJUMLA wa mazuri TUNAYOYATAKA na YANAYOTUFAA. Na ituwezeshe KUJIONGOZA kuyatambua tutayotaka na yanayotufaa siku za usoni. Iweze kutupatia Wawakilishi sahihi wa KUTUWEZESHA KUJIONGOZA katika kuyafikia tunayotaka na yanayotufaa sote.Katiba ITUONGOZE kuyasimamia MAZURI na iweze KUJILINDA na KUJIBORESHA siku za USONI. KATIBA ITUFANYE TUUOGOPE UONGOZI NA KUPENDA KWANZA KAZI NA TAIFA LETU KULIKO KITU KINGINE CHOCHOTE.

0 comments:

Post a Comment