Vijana
waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.
Fimbo
tangia kitambo, Kwao TFF ni wimbo.
Bora wale
wa kitambo, Waliweza wetu wimbo.
Wa leo
twaona mambo, Na Mengi yao majigambo
Vijana
waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.
Raisi kafanya mambo, Sitomlaumu jambo.
Kawaleta na wa ng’ambo, Mliosema wagambo.
Mapesa Rambo kwa Rambo, Mkamnyima na WIMBO
Vijana
waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.
Tumeganda
na Urimbo, Kandanda laenda kombo.
Nina langu
moja jambo, Sitoongea kimombo.
Tubaki
kwenye urimbo, Vijana wafanye mambo.
Vijana
waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.
Tuache
vyetu vimambo, Kupenda yetu matumbo.
Hata iwe ni
kitambo, Yatafika majigambo.
Pesa nyingi
sio jambo, Tujali yao matumbo.
Vijana
waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.
Taachane na
wa ng’mbo, Watuacha kwa urimbo.
Yanawiriyo
matumbo, Sina hamu na wang’ambo.
Hatuchukui
kitambo, Kwa mafupi majigambo.
Vijana
waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.
Tushike
yetu mitambo, Tusidekeze matumbo.
Tusiwe na
mengi mambo, Tuchague moja jambo.
Turudi kama
kitambo, Tuzidi ya kale mambo.
Vijana
waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.
Kila wimbi lina
chombo, Kiswahili si kimombo.
Vipaji kama
ng’ambo, Hatuyaoni makombo.
Hii mifumo
ya ng’ambo, Kwetu kivuli cha fimbo
Vijana
waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.
Wanawasifu
wa ng’ambo, Nyumbani kwaenda kombo.
Onyesheni
yenu mambo, Mkiimarishe chombo
Ligi yetu ya kitambo, Tumeitupa na Chambo.
Vijana
waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.
0 comments:
Post a Comment