Monday, July 8, 2013

BAJETI YA TANZANIA 2013-14: Kama kupanga ni matumizi,WAKULIMA TUMO!



"Upenyo Sahihi wa kuboresha Bajeti ni kupitia Kuongeza Makusanyo Yetu".

Kila mtanzania ana haki ya kusema moja au kadhaa kuhusu bajeti ya nchi yetu maana kwa namna moja u nyingine itakuwa inamgusa tu! Wengi wameitazama kwa jinsi wainavyo, na kuitathmini kwa jinsi waonavyo kuwa ndio sawa!


Kutoka Tankini, bajeti na mambo mengi yahusuyo hatma ya Taifa letu hutazamwa kwa kujali fikra zenye utamaduni wa ubora. Bajeti hii ni makadirio au mpango wa MUKUSANYO YA PESA na MATUMIZI ya Taifa letu kwa kipindi kifupi kijacho (mwaka mmoja).  Mambo ya kuyaangalia katika hili kwa mujibu wa tanki ni pamoja na haya;

KWANZA , ni kuwa UNAPOPANGA lazima uwe na UWEZO wa kuingalia kesho kwa MAPANA. Hili linahitaji UTAALAMU na uwezo wa kufikiri pia. Kujua nini kinatakiwa kufanyika na kinahusisha nini hasa na mazingira ya kiutendaji yakoje na hivyo basi, hili sio jambo dogo.

PILI, ni kuwa na uwezo wa KUCHAGUA KINACHOSTAHILI (KWA KUZINGATIA TIJA YAKE KATIKA TAIFA NA KWA WATANZANIA WALIO WENGI, KWA MTAZAMO WAO HALISI) kuanza na namna ya KUKITEKELEZA NA KUKISIMIMAMIA. Kujua nini kianze, kwanini, faida na hasara zake ni zipi na zaidi utakitekelezaje na utahakikisha vipi kuwa hakikwami, na kadhalika

TATU, ni KUACHAGUA, KUWEKA NA KUTUMIA na VIGEZO SAHIHI vya KUJIKAGUA, KUJIPIMA na hata KUTHIBITISHA JAMBO ili kuona MAFANIKIO, MATATIZO na UBORA WA MIONO ya Mpango mkubwa na Mipango saidizi.

Kunaweza kuwa na mambo mengine mengi yanayohitaji kukamilisha hili swala Bajeti,lakini haya kwa namna moja au nyingine yamo, na yanatosha katika kuingalia na kuchangia juu ya Bejeti yetu.
Hivyo basi, Kwa kila sentensi tunatakayokutana nayo kwenye bajeti, kikubwa ni kujaribu kuona kama ina sifa hizo tatu za MSINGI. Na hapa cha kuangalia sana ni makusanyo na matumizi. Yaani, kuangalia ni jinsi gani tunaweza kwa kupitia MAKUSANYO NA MATUMIZI BORA, kupata TIJA BORA.

Baada ya kupitia kwa kiwango chake, tanki lina haya:

  1. Bajeti, imeonyesha KUTAZAMA zaidi MUDA mfupi, usiozidiMIAKA 30, nap engine ndio maana madhara ya vitu Kama kuongezeka kwa DENI la Taifa na mengine hayakuwa yakielezewa MAANA zake kwa MAPANA (Mtazamo wake kwenye MKUKUTA na DIRA ya 2025), na kuonyeshwa mikakakati yake kwa marefu stahili. Hapa kunaweza kuwa na sababu kadhaa, ikiwemo pengine MUDA MFUPI wa kuandaa bajeti au MAPUNGUFU ya KIUFANISI katika hili. Ni vizuri, kuwe na TAFSIRI za Bajeti yetu kwa mapana na marefu ya namna hiyo, na kazi hii inaweza kufanywa pembeni japo sambamba na bajeti.
  2. Mtazamo umekuwa ni MKUKUTA na DIRA ya 2025, Watanzania wengi ni WAKULIMA, hivyo tunaitarajia bajeti KUCHAGUA angalau VIPAUMBELE kwa kuwaangalia WAKULIMA. Bajeti imeonyesha MAHUSIANO ya hili Kwa KUELEKEZA PESA ZAIDI kwenye Wizara ya Maji, Nishati na Uchukuzi, wizara ambazo kwa namna moja au nyingine zina uhusiano sana na KILIMO, yaani kama vile kuwekeza kwenye KILIMO CHA UMWAGILIAJI na kuongeza UFANISI kupitia UCHUKUZI na NISHATI.

  1. Juu ya muda Na vigezo vya kujipima, bajeti haijaonyesha, pengine sio sehemu sahihi. Hivyo Muda umebaki kuwa mwaka mmoja. Hii inapelekea ugumu wa kuweza kuona muelekeo wa kufanikisha matarajio haya ya bejeti HII na hata kuweza kuchambua uhusiano wake na ILIYOPITA au na IJAYO.
 
  1. Kwa ujumla bajeti MARA NYINGI haijawa wazi juu ya VIGEZO vya AHADI NA SABABU za juu ya mikakati ya MAKUSANYO NA MATUMIZI. Pia kumejitokeza mapungufu juu ya uhalisia wa VIGEZO kwenye uthibitishaji wa mafanikio, kama vile . Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa MKUKUTA II umeonesha mafanikio katika maeneo mengi ingawa bado kuna changamoto. Mafanikio hayo Ni pamoja Na kuendelea kukua Kwa pato la Taifa, kuongezeka Kwa mapato ya kodi, kukua Kwa sekta ya fedha Na mikopo Kwa sekta binafsi, kuimarika kwa usimamizi wa matumizi ya Serikali na kuimarika kwa utoaji na upatikanaji wa huduma za jamii.Kuona na kuamini Uhalisia wa mafanikio haya kwenye tumbo la mkulima unahitaji MANATI sana, kwa sababu ya matumizi ya maneno ya UJUMLA sana,bila kuhusisha na Mkulima moja kwa moja.

  1. Na pia bajeti, imeonyesha kuwa kiasi cha mapato tunachokusanya WENYEWE ni kama 63% wakati tunachotumia (MISHAHARA NA MATUMIZI SAIDIZI) ni kama 51%. Ulipaji wa Deni na Maendeleo yote, IKIWEMO pesa ya kundi kubwa la WAKULIMA vinategemea 49%. Ulipaji wa deni ni kama 18%, hivyo MAENDELEO YOTE NA MKULIMA NI 31%. Hapa ni rahisi kuona kuwa, UFANISI UNAOTAKIWA KWENYE hii 31% ni mkubwa kiasi gani. Na hata tukisema maendeleo yote yana mlenga MKULIMA, bado ukweli unabaki kuwa WENGI ndio wanakula kidogo.
 
  1. Ukichukua 63% ya bajeti, pesa tunayokula,ukagawa kwa idadi ya watanzania wote (40,000,000) pengine ni kama 240,000 kwa mwaka kila mmoja. Huyu mtu anatakiwa kutmia kiasi hicho cha fedha na kulipa deni la 6% (14400) kwa kutumia kama 31% (75,000) kama kitega uchumi.

 
HITIMISHO

Wachache kupewa kingi si TATIZO sana, kama tu ni kweli, tija waileteayo taifa ni kubwa kiasi cha kilikwamua taifa zima. Kifupi bajeti inatuambia kuwa Maendeleo ya MKULIMA na TAIFA letu, kupitia Nishati, Maji na Uchukuzi kwa pamoja kwa kadri ya jinsi wizara hizi zilivyopewa kipaumbele kwenye bajeti hii zinahitaji kama 22%, na hivyo wizara zingine kuhitaji 9% tu, kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Pengine kunaweza kuwa na ukweli ama uwezekano, au hata kuwa ni makosa ya kuelewa BAJETI yenyewe, lakini mambo MAKUU mawili yaliyo wazi juu ya bajeti yetu hii ni:
  1. Umuhimu wa Kuongeza Ukusanyaji wa kodi na Vyanzo wa Kodi. Hili linawezekana zaidi Kama tutawafanya watoa kodi ndio wawe wakusanya, wapangaji Na watumiaji wakuu wa kodi hizo. Ni vema sasa Halamshauri zikaongezewa madaraka juu ya Maamuzi ya maendeleo ya sehemu husika.
  2. Umuhimu wa JUHUDI za MAKUSUDI za kuongeza UFANISI na uelewa juu ya UFANISI WA Kitaifa, ILI KUHAKIKISHA KILA PESA INAPOPELEKWA INAZAIRSHA FAIDA ZAIDI. Hili linawezekana, Kama TAIFA litafanya kazi kama TIMU moja, na wananchi kuwajibika KWA taifa lao na sio SERIKALI. Hii itawezekana pia endapo, MPANGAJI, MSIMAMIZI, NA MLAJI wanonana ANA KWA ANA. Hivyo Umuhimu wa kupunguza madaraka kwenda MAWILAYANI bado haukwepeki.
  3. Umuhimu wa kuwa na MIPANGO YA MUDA MREFU (Miaka kama 100 na zaidi) na kuiheshimu, kwa kuihakiki kwenye kila mipango midogo unaoelezwa kama BAJETI. Hili litawezekana kama TUTATOA kipaumbele kwa UHAKIKI na MATUMIZI ya UTAALAMU kwenye kila JAMBO, ikiwemo kurekebisha mfumo wa Elimu ili kuhusisha UTAALAMU NA UMAALUMU wa UTAALAMU.


Kunaweza kuwa na mengi zaidi, ni haki yako kueleza, ila kwa sababu najua wabongo, utasikia jamaa hakusoma kabisa alafu anasema sema tu, hii hapa chini rafu yangu, ipitie na wewe. KIBONGOBONGO IKO POA kiana!

HAMKAWII KUSEMA;HATA BAJETI YENYEWE HAKUISOMA. HIKI KIPANDE CHA RAFU YANGU

Mapato ya Ndani
                                11,154,071
(i) Mapato ya Kodi (TRA)
10,412,937
(ii) Mapato yasiyo ya Kodi
741,134
B. Mapato ya Halmashauri

383,452
C. Mikopo na Misaada ya Kibajeti

1,163,131
D. Maendeleo ikijumuisha MCA (T)

2,692,069
E. Mikopo ya Ndani

1,699,860
F. Mikopo yenye Masharti ya Kibiashara

1,156,400
JUMLA YA MAPATO YOTE                                                                  
                                    18,248,983
Matumizi
G. Matumizi ya Kawaida
                                        
12,574,949
(i) Deni la Taifa
3,319,156
(ii) Mishahara
4,763,196
(iii) Matumizi Mengineyo
4,492,566
Wizara                                                3,738,316
Mikoa                                                     49,701
Halmashauri                                           04,549
H. Matumizi ya Maendeleo

5,674,034
(i) Fedha za Ndani
2,981,965
(ii) Fedha za Nje
2,692,069
JUMLA YA MATUMIZI YOTE
                                     18,248,983












































0 comments:

Post a Comment