"Kuogopa Ukweli
Kunatugharimu Sana Kimaisha"
Mara nyingi tunapoongelea Utumwa tunamaanisha ile hali ya Umiliki wa Binadamu na kumfanya kama bidhaa. Inawezekana kukawa na
kufanana kwa baadhi ya vitu, lakini pia hali ya kuwa huwezi kufanya maamuzi fulani sahihi kwa
sababu tu unaogopa kuwa utakuwa unapingana na ukweli au uhalisia, na hivyo unalazimika
kuendelea kufanya yasiyo sahihi kuyafanya tunaweza kuiita utumwa wa kifikra.
Watu, Familia
mpaka Mataifa hasa kutoka nchi zetu zinazoendelea bado utumwa huu wa kifikra unatutafuna
sana. Msingi wa Biashara ya Utumwa ilikuwa ni Mtumwa Mwenyewe na hapa pia kwa kiasi kikubwa msingi wa utumwa wa kifikra ni mtu/mtumwa mwenyewe.Umefika wakati tuukatae utumwa wa kifikra kuanzia majumbani mpaka kitaifa! Taifa na fikra za wananchi ni vitu vinavyotegemeana sana.
Mfano 1:
Una
mpenzi wako, unampenda sana, umemsaliti, halafu jamaa mmoja akakuona ukifanya
huo usaliti, naye akaona ni vema afanye kitega uchumi, akakulazimisha umpatie
kiasi cha pesa ili,asitoe siri. Ukimpatia hicho kiasi cha pesa tayari umekuwa
mtumwa wake, siku nyingine,itabidi umfanyie kikubwa zaidi kwa sababu sasa utakuwa
na makosa mawili,lile la usaliti na la pili ni kumpatia pesa! Hii tunakutana
nayo katika mazingira mengi kwa sehemu au nyadhifa tofauti. Mfikirie, kiongozi
anayeogopa usimtolee siri ya kuwa anajihusisha na uovu Fulani, baba/mama
anayemuogopa mwanae kwa kuwa anafahamu udhaifu wake fulani, au Mabosi na
wafanyakazi (Makazini na Majumbani) na Pengine Mashuleni na vyuoni! Na hii
imekuwa ikiathiri sana utendaji sehemu nyingi,mtu anatenda chini ya uwezo tu
kwa sababu ya baadhi ya mambo ambayo yanahusiana na madeni ya fadhila!
Mfano 2:
Wewe
hukubahatika kuwa na kitu Fulani kama uzuri,akili kali,pesa nyingi, kupendwa na
watu, na mambo mengine kama haya! Hivi ni vitu ambavyo vingine huwa ni
majaaliwa ya mwenyezi mungu na vingine huwa ni jitihada mbalimbali ambazo
zinaweza kuwa na sababu za wazi kabisa kama vile kufanya kazi kwa nidhamu ya
hali ya juu. Sasa inapotokea, hauna kimojawapo au vyote, badala ya kukubali
kuwa huna kwanza, unaona ni bora kulazimisha. Hii hutokana na Ukweli kuwa
binadamu tunapenda kushinda siku zote na tumeumbwa na TAMAA na WIVU, lakini kumbuka
KUWA NA KIASI KWENYE KILA JAMBO NI MUHIMU SANA. Hivyo ni lazima uchague kiasi
sahihi! Bila kuwa na kiasi utajikuta unakuwa mtumwa wa kifikra, mwenzio
kapendeza kuliko wewe, tatizo, mwenzio kasifiwa,tatizo, mwenzio anafaulu
mitihani zaidi yako,tatizo, mwenzio anapesa zaidi yako,tatizo kubwa, na
mwishowe mwenzio anawapenzi wengi pia inakuwa tatizo na unataka kuhakikisha
unakuwa wewe. Tumeona katika jamii zetu watu wanapenda kuwa wao mpaka wanaingia
kwenye mikumbo ya ajabuajabu.
Mafno 3:
Pia kuna
wakati mtu anatawaliwa kifikra sio kutokana KUPEWA MAWAZO “SUMU’ NA WATU WENGINE, mawazo hayo yanakufanya fikra zako kutumikia aina ya maisha ambayo haina uhalisia kabisa kwako,lakini unafanya hivyo kwa sababu ya kutaka ama kumfurahisha mwingine au kulazimisha jambo au kwa kuwa unaamini ndio suluhisho pekee kwako na mbaya kabisa ikawa ni kwa sababu ya kutaka kumkomesha fulani au kinafulani.
Binadamu ni wapekee sana na hivyo jamii imeundwa na watu wenye fikra tofauti. Hivyo ni kazi yako
wewe au ya mzazi kutambua ubora wa fikra hizo mbalimbali zinazotokana na jamii.
Si ajabu mtoto kufanya jambo lisilo sawa na akasifiwa, na mzazi ukafurahia au
pengine ikawa ni kicheko kwenye sura tu lakini usilikemee, au vijana kupeana
ushauri ambao unawazulu wote au mmojawao na wakandelea nao au wakaachwa tu. Pia hata watu wazima
kushauriana mambo ambayo pengine vichwani mwao hawayakubali kabisa,ila kwa sababu ya
kudumisha urafiki, hawana budi kutekeleza! Wakati mwingine watu hutoa ushauri ambao
kwa mazingira fulani, ulikuwa ni mzuri
na unafaa lakini kwa pupa mchukua ushauri akawa hujaelewa bali kaamua KUKOPI NA
KUPESTI, matokeo yake ushauri unakwenda kutumika sehemu isiyo sahihi kutokana
na upekee wa kibinadamu na kuwa sumu kwake! Kitu huwa ni DAWA KINAPOTIBU na pia huweza kuwa SUMU
na KUUA kinapotumiwa tofauti. Kuielewa vizuri hii,fikiria kuwa wewe ni mwanasheria halafu, mtu anakushauri kuwa unaweza kuwa daktari bingwa,mbona yeye alisoma masomo ya sanaa lakini kwa sasa ni mhasibu mzuri tu. Wakati unatekeleza kuwa daktari bingwa,unaweza kuwa mtumwa wa kifikra kwa kiasi kikubwa.Na pia anaweza kuwa anakukataza kuwa sio rahisi kuwa daktari bingwa wewe kutokea eneo la uanasheria, unakasirika na kumuona hafai,hivyo kutaka sasa kumuonyesha kuwa unaweza,pia unaweza kuwa kwenye utumwa wa kifikra!
Ukiambiwa:
Kama hunywi pombe huwezi kupata dili mjini, au mumeo asikubabaishe bwana haki
sawa siku hizi, au kusomesha kitu gani, mbona mimi sikusoma na mambo yangu
safi, au mimi mambo ya wazazi na ndugu sitaki kusikia kabisaaa kwa sababu sio
wajibu wangu kuwaangalia, wajibu wangu ni wanangu tu; na mengine mengi kama
haya, na ukimsikiliza mtu huyo anatoa hoja ambazo pengine zinaendana na maisha
yake, hivyo kwake zinaweza kuwa ni fikra bora kabisa, kwa kuwa zinayafaa
mazingira yake ya kimaisha! USIKOPI NA KUPESTI kwako wewe,sikiliza,elewa sababu za yote
yaliyosemwa,fananisha mazingira yako,fikra zako na mazingira simuliwa ndio uone ushauri huo
utakufaa vipi! KUMBUKA KUWA PAMOJA SI KILA WAKATI INAMAANISHA KUWA NA UMOJA.
HATA UNDUGU UPO WA KUFANANA NA WA KUFAANA, na kumbuka pia kuwa DUNIANI WAWILIWAWILI, hivyo
ni lazima ujue kuangalia ni wakati gani wewe na rafiki yako mko pamoja na wakati
mna umoja, au ni lipi wazo linalokufaa kati ya yale yanayofanana kufaa, na ni ndugu yako au kafanana na ndugu yako na kama ni ndugu yako ni wa kufanana au
wa kufaana!
Suluhisho!
Binadamu ni
wapekee kama tunavyoamini. Suluhisho la haya litatakiwa usikopi na kupesti kama
wanavyotukataza (Orijino Komedi-Tanzania (TBC)).Na ieleweke kuwa binadamu wa
leo 50% ndio 100%, kwa sababu makosa na mazuri yakilingana, unashukuru! Hivyo tunachpigania hapa ni kujitahidi
kuboresha fikra zetu kuelekea kwenye hiyo hamsini . Waswahili husema dawa ya
deni kulipa,ukiangalia kwa undani hasa utaona kuna aina Fulani ya deni ambalo
mtu anakuwa anaogopa kulilipa, ukweli hudumu daima hivyo kuukimbia UKWELI ni
kujidanganya. Kwa hiyo UKILIKOROGA WE LINYWE HARAKA HARAKA utakuwa umemalizana
nalo, na ndio maana kuna hata swala la
kutubu, na kukubali huyafanya yaishe! HAKUNA ALIYE MSAFI na BORA KWA KILA KITU ,
hivyo huna haja ya kuogopa UKWELI JUU YAKO na kuishi katika uongo unajidhulu
zaidi mpendwa,UYAFANYAYO NDIO WEWE,hivyo ukifanya ya uongo uongo UJUE na wewe unakuwa
WA UONGO UONGO, na furaha ya UONGO huwa ni ya muda mfupi na zaidi huwa ni RAHA TU ambayo
huendelea kukugharimu kila inapoitwa leo na pengine mwishoni kukubwaga pabaya sana.
FURAHA YA KWELI hudumu kama ukweli na huanzia kwenye UKWELI NA
UHALISIA, hii NI YA WATU WA UKWELI, jaribu uone FURAHA ya KUWA WA UKWELI! Ni ya wachache kwa sababu ni kawaida kwetu wengi kutopenda ukweli, "What is right is always not Popular", hivyo watajaribu wachache wapenda UKWELI, na tunaamini we ni mmoja wa wachache hao wa UKWELI.
KILA LA KHERI,
TOA MAONI YAKO YA DHATI NA UKWELI
0 comments:
Post a Comment