"HAPA NI KENYA NA TANSANIA IPO HAPAHAPA"
Unaweza kuwa na kila kitu, ukikosa fikra bora umekwisha, unaishia kunufaisha wengine.
Mtu kwao bwana, mambo ya kanga, chai,"gahwa" na kadhalika, watu twaonja tu! Ukigundua kanga imeandikwa nini utakubali kuwa watanzania tumelala. |
Siku ya tarehe 26 mwezi wa kwanza, hapa Koln, moja kati miji mikubwa ya Ujerumani kwenye moja ya majumba ya makumbusho kulifanyika maonyesho, ambayo kwa mujibu wa hapa na pale ilikuwa ni siku ya
Africa ndani ya Ujerumani kwa mwaka wa 201, kwenye jumba hilo la makumbusho. Kwa ujumla kuna vitu vingi vwa kujiffunza kutoka kwenye jumba hilo. Kama Mtanzania na Mwafrika ,nilijikongoja na kuhudhuria kuweza kujikumbusha kidogo mambo ya nyumbani. Nyumbani ni Nyumbani.
Kwa kweli nilitegemea nikikosa sana nitakutana na bendera ya taifa. Zaidi nilitegemea kukuta na watz wenye pesa zao za matumizi, ambao watakapoomba muziki,basi tuselebuke wote na vitu vya Msondo,Twanga,Mipasho ya mwambao au Akudo Impact na ikibidi kama ni majanki basi Bongo Flava na kiduku kiana. Lakini vilevile kichwani mwangu nilitarajia watanzania tutafunika sana kwenye mambo mbalimbali ya kitalalii, si unajua tunajiamini kwa maliasili tulizonazo, yaani zilivyo nzuri, nyingi na za kuvutia.
Mambo kwa kweli hayakuwa hivyo kiviile! Sikumbuki kusikia Kiswahili cha mtanzania,japo kiswahili nilikisikia kiduuuuchu.Niliona rangi za bendera yangu kwenye vitabu na vipeperushi, na kwenye vitu vichachevichache. Pia niliona matangazo ya kutosha ya vivutio vyetu kama Mlima Kilimanjaro,ambao mtu alikuwa kautengeneza kwa kutumia "Setilaiti" na kutoa picha moja nzuri anaiuza kati ya Euro 25-30 (Yaani elfu kama Hamsini na zaidi hivi za kibongo). Hapa ilinibidi niulize mahusiano yake na nchi, na jibu nililopata ni kuwa anatumia pesa nyingi sana kuandaa na amesomea,nikakumbuka kuwa pengine sina haki ya kuuliza hilo! Maana "akufukuzaye hakwambii toka".
Kuna mfanyakazi wa kampuni ya kitalii alisema kuna mawakala mbalimbali nchini Tanzania , ambao ndio wanaopiga picha mbalimbali nilizokuwa nikiangalia kisheria kabisa,wengine waliamini huyu Mtanzania kwao mambo safi, vivutio vyote hivi, kumbe wapi. Ikiwa hivyo, hapo naipongeza Serikali kudhibiti mfumo huo mzuri,ila juhudi bado ziendelee kudhibiti hasa kitechnologia kama jamaa wa Kilimanjaro. Labda kama lugha ilikuwa "Gongana",vinginevyo tutaendelea kupoteza faida za kitalii, kwa sababu sikuona mahali panapoonyesha kuwa mlima ni wa Tanzania.
Haya yote hayakuwa kero sana kwangu, na wala sikusikitika sana mpaka pale nilipokuja kugundua kuwa wanaoonyehsa vitu vinavyohusiana na Tanzania sio watanzania ni ndugu zetu Wakenya. Na kwa kweli wanasema, hapa ni Kenya, na ukiuliza Tanzania wapi unaambiwa hapa ni Kenya naTanzania ipo humuhumu, sasa sijui labda ni kutofahamu kiswahili vizuri !
Nikaondoka nikiwa mnyonge kabisa na msemo wangu wa
"HAPA NI KENYA NA TANZANIA IPO HUMUHUMU"
Unaweza kuwa na kila kitu, ukikosa fikra bora umekwisha, unaishia kunufaisha wengine.
Kumbuka wajinga ndio waliwao!
SASA
WATANZANIA TUAMKE NA KUINGIA DUNIANI KUTAFUTA
TUMEWANUFAISHA WENGINE KIASI CHA KUTOSHA.
0 comments:
Post a Comment