Sayansi ni neno ambalo pengine watanzania tunalitamka sana.
Kati yao wapo ambao tunalitamka na kulitumia vizuri, na pia ambao hatulitumii vizuri ama na hata kutolifahamu kabisa
kama sio hata kulitamka na kulisikia.Ukianza kuzungumzia maana, unaweza kuzua
UBISHI badala ya MJADALA, kitu ambacho ndio JADI yetu WABONGO. Lakini, KIBONGOBONGO,potelea mbali acha tubishane tu
mpaka tufe na NJAA.
Kimsingi,
Sayansi ni utashi,uelewa utokanao na fikra ama elimu
katika nyanja yeyote ile,ili mradi tu upatikanaji huo wa utashi umepitia njia
ama taratibu thabiti na madhubuti ikiwemo uhakiki bayana wa KITAFITI. Lengo likiwa ni kuongeza
“UTASHI JUU JAMBO FULANI”. Hii ina maanisha, kuwa karibia kila kiumbe kinaweza
kuitwa mwanasayansi, ili mradi tu kinakidhi misingi kadhaa katika kutupatia
utashi fulani,yaani nadharia sahihi na uthibitisho madhubuti katika kufikia kiasi
hicho cha utashi huo. Tafiti za kisayansi, nazo zinapitia hapohapo,kwamba kama
ikiwezekana, ili kukamilika kuwa utafiti wa kisayansi, basi uwepo wa nadharia
sahihi na uthibitisho madhubuti wa jambo fulani, ni muhimu kukamilisha sifa ya
utafiti bora. Pengine tofauti ni kuwa tafiti zina lenga kutupatia MAELEZO kuhusu
jambo kwa manufaa yetu.
Mfano: Ukisema MTOTO ASIPOCHEZA SIKU NZIMA, NI DALILI YA KUWA NI MGONJWA, kama kuna
nadharia sahihi na uthibitisho madhubuti, kuwa huo ni UTASHI mpya muhimu
kwetu,basi nawe ni mwanasayansi, na ULE utaratibu na hatua ulizotumia kufikia
UTASHI huo (tangia nadharia mpaka vidhibiti) ndio unabeba sifa za kitafiti kama
ni wa kisayansi au la.Kikubwa ni matumizi ya kifikra kwenye kujengea nadharia/mitazamo na vidhibiti kimtaa na kuweza kufikia hapo. Swala la mwanasayansi bora na kiasi cha sayansi yako kutumika kwenye jamii, litupilie mbali, ama angalia mazingira yako, ili mradi usiifuate nafsi/moyo zaidi ya ukweli na uhalisia sahihi,sio wa wengi wape,bali wa wengi bora wapewe.
Sasa, porojo ni nyingi sana juu ya sayansi hasa
ukitaka kujua kuwa chimbuko hasa ni kwenye imani za kidini, wakati UTASHI ulitegemea
IMANI tu, ikapitia hatua ya utashi kutegemea uwezo wa kifikra na mpaka leo hii wakati imeonekana vema
uthibitisho wa uhalisia usaidie uwezo wa kiakili/fikra kuonyesha kuwa nadharia
ni sahihi na inamaanisha uwepo wa UTASHI sahihi katika maisha yetu. Kuna maubishi
kibao, japo sio kama ya KIBONGO,yasiyolenga KUJENGA, bali kuonekana nani zaidi.
KWA NINI TUNAHITAJI TAFITI ZA KISAYANSI
- SAYANSI SIO UBISHI
Sayansi haiko kutufanya tubishane, bali kutufanya
tufikie muafaka ambao unatufaa wote na hasa tunauamini na kukubaliana kuwa unatufaa,
ili kesho tusipate kutupiana lawama. Bila hili, hatuwezi kuwa tunaenda
mbele,kwa sababu WATU ni wapekee.Kila mtu anajua na kutaka lake kwa sababu zake
- SAYANSI HAIKATAI IMANI
Sayansi na dini bado ni vitu viwili, vinavyoendelea
kuchuana, kama baba na mtoto wa kwanza. Uwepo wa vyote ni muhimu kwetu na kwa
vyenyewe. Huna sayansi, pengine utachelewesha kusambaa kwa imani, kwa sababu
vitendea kazi vya imani nyingi vinatokana na ugunduzi wa kisayansi na imani pia
zinasisitiza kusaka UTASHI kwa udi na uvumba kama sehemu ya kuonyesha kuwa ni
muhimu kuwa mwanasayansi ili uendeleze imani. Na pengine unapoacha kuamini tu
ndipo uanasayansi wako unapoelekea mwishoni,maana unakosa wa kukuongoza, ama
dira.
- UTATUZI WA MATATIZO
Utatuzi wa matatizo unahitaji FIKRA na pia UTHIBITISHO
wa UHALISIA kimaisha. Hili moja kwa moja linatupelekea kuhitaji sayansi, ili
kuwa na uhakika kuwa TATIZO ni nini hasa Na UTATUZI WAKE ni upi hasa. Maana
bila ya hivyo, tutakuwa tunabahatisha kila wakati,kitu ambacho ni sawa na KULA
SUMU. Mfano, ni pale tunapojua kuwa RUSHWA ni TATIZO,lakinihatuwezi kuijua
rushwa kisayansi. Matokeo yake, tunaanza kukubaliana na wazo la KIONGOZI bila
utafiti wa kisayansi, matokeo yake tunakuja kugundua kuwa hatukutibu UGONJWA
bali tuliongeza,tayari tumeumia. Kama haitoshi, maendeleo yanahitaji UVUMBUZI
NA UBUNIFU KADHAA WA KADHAA, ambao unahitaji utashi utokanao na UTAFITI wa
KISAYANSI. Ndio hivyo wenzetu wanavyoendelea jamani.
- UBORA WA KIFIKRA
Kama haitoshi, dunia tulionayo ni ya KISAYANSI, hivyo
kama hatuwezi KUFIKIRI kisayansi, maana yake hatuongei lugha moja na
wenzetu,hivyo hatuwezi kuwaelewa. Na matokeo yake watatudanganya usiku na
mchana. Huwezi kujua kama utafiti uliofanyika kuhusu DAWA ya MALARIA
unayoitumia ulikuwa sahihi, na hivyo kuthibitisha MATUMIZI ya DAWA hiyo kwa
binadamu,kama MWENYEWE HUNA misingi ya tafiti za kisayansi. Vile vile unaweza
hata KUOGOPA kivuli chako, kwa sababu UTASHI wa kisayansi UKO mbali, na hivyo
kujichelewesha kimaendeleo. Mbaya kabisa, utaendelea KUJILISHA sumu za UTASHI
kwa kudhani unatibu matatizo yako kumbe la hasha,hakuna kitu,unaahirisha
maumivu tu.
HITIMISHO
Tunahitaji kufahamu matumizi ya neno sayansi na
kuelewa hasa sayansi ina umuhimu gani katika KARNE hii bila kujali itikadi zetu
ama imani zetu ama asili zetu. Mwanasayansi anaweza kuwa mtoto,mtu mzima,
mwanamke ama mwanaume na hata pengine wanyama na mimea ituzungukayo kama sio
MUNGU. Imani za kuwa kuwa mwanasayansi lazima uwe na hesabu kibao ama fizikia
na sio siasa, si za msingi kwa maisha haya, ama kuwa lazima uwe umefikia chuo
kikuu, hazitusaidii kwa sababu matatizo mengi sana yako majumbani mwetu ambayo
kwa kujua misingi hii ya sayansi,mtu anaweza kutatua matatizo yake kisayansi
kwenye kiwango chake.
Mbongo lazima ubishe, kwa sababu sio
mwanasayansi,hivyo hutaanza kuangalia ANDIKO kama ni la KISAYANSI, bali utaanza
kubisha.Lakini jiulize “mtoto akichezea wembe mpe”, ni msemo wenye maana gani? Kama
sio kuwa NADHARIA ya msingi kabisa kuwa mtoto anaweza kuwa NI KING’NG’ANIZI, na
huku hajaelewa mambo mengi kwa sababu bado angali na umri mdogo hivyo anajifunza,hajaona
mengi na anapaswa kuwasikiliza sana wakubwa na kupima kabla ya kubisha na
kuendelea, na uthibitisho kuwa wembe si rahisi UKAMUUA,bali utampa fundisho
ambalo litamfanya ASICHEZEE BOMU siku nyingine akiambiwa linaua, ni kweli na ni
UTASHI sahihi kwa jamii yetu!
Kudharau haya kumetupelekea sasa, si ajabu, mtaalamu
wa UJENZI anataka aulizwe kuhusu ujenzi tu, na pengine katika eneo lake tu, kwa
sababu mengine hayamuhusu, hivyo ripoti ya gazetini kuhusu siasa ataimeza na kuitema
popote kwa UHAKIKA kabisa,ama atasema hili sio tatizo langu,japo ni mkazi wa
eneo husika. Mcheza mpira haamini kama kuna misingi ya mpira, zaidi ya kipaji, wala
mwanasiasa anaamini uongo ndio msingi mkuu wa siasa, na mwanahisabati kajitoa kwenye maboresho ya
katiba. Mkubwa hataki kuulizwa na mdogo, na mdogo anaamini tamthilia na blogu
kama hii, kuliko wakubwa zake.
“Mankind has tried the
other two roads to peace - the road of political jealousy and the road of
religious bigotry - and found them both equally misleading. Perhaps it will now
try the third, the road of scientific truth, the only road on which the
passenger is not deceived. Science does not, ostrich-like, bury its head amidst
perils and difficulties. It tries to see everything exactly as everything is.
(Professor Garrett P. Serviss)”.
............ITAENDELEA......
0 comments:
Post a Comment