Ni Nelson Mandela, Muhimu kuliko Hela.
Alipendwa na Masela,Fukara na wenye Hela.
Wasomi wafunga
tela, Kawafunza bila hela.
Lala Peponi Madiba, Upumzike Wetu baba.
Nelson Mandela (18 Julai 1918 - 05 Disemba 2013)-Na KEVIN BLOOM |
"Fifty years ago Martin Luther King called out in hope, “Let freedom ring”. “Freedom” answered his call by walking out of Victor Verster Prison 27 years later - and the world embraced the human embodiment of that elusive concept in Nelson Mandela. The body that nurtured the concept is no more, and now the world again
cries out, “Let freedom ring”, this time in tribute. Hamba kahle, Tata Madiba, your long walk is done. By KEVIN BLOOM.(http://www.dailymaverick.co.za/article/2013-12-05-rest-in-peace-madiba-thank-you-for-everything/#.UqER5VNqySo)"
Kila mtu atamkumbuka mzee Madiba kwa namna yake, ikiwa ni pamoja na TANKI,kutoka tankini kuna MAWILI yakuchangia.
1- Tumuenzi kwa kufanya mazuri aliyosisitiza,na sio kama ilivyoada ya nchi zetu kusimulia zaidi ya kutenda.
2- Kila mtu aichukie ari ya MZEE Madiba, na kuitumia katika eneo lake,sio lazima uwe kiongozi wa nchi kuweza kuyatumia mwawazo yake. Kifupi huyu pengine ndiye mtu aliyeweza kuifanya DUNIA ione UTU wa mtu mweusi, kuwa PAMOJA NA kuwabagua kwa RANGI, bado aliposhika UONGOZI alisahau kabisa KISASI na kuanza upya,kitu ambacho mimi na wewe sidhani kama tungeweza. MTAZAMO TU.
Ndugu zetu wa South Afrika, TUKO pamoja
Ni Nelson Mandela, Muhimu kuliko Hela.
Alipendwa na Masela,Fukara na wenye Hela.
Wasomi wafunga
tela, Kawafunza bila hela.
Lala Peponi Madiba, Upumzike Wetu baba.
Chozi latutiririka,Upweke
umetufika.
Madiba umetutoka,
Bondeni Kumepasuka
Mababa mwapukutika,
Afrika twaweweseka
Lala Peponi Madiba, Pumzika Wetu baba.
Mengi uliyo tufunza,
Vichwani tumeyatunza.
Dunia Uliifunza, Ubaguzi
sio kwanza.
Shani walizo kutunza,Iringa
tumezitunza.
Lala Peponi Madiba, Pumzika Wetu baba.
Kimwili
umetutoka, Fikirani hutotoka.
Matendoni ninashaka,
Ya baba nimefutika.
Ukweli ulo
andika, Katu hautofutika.
Lala Peponi Madiba, Pumzika Wetu baba.
Salamu
ukikumbuka, Wapashe Ukiwakuta.
Mlibya patashika,
Mbongo nguo chanika.
Umoja tumeuzika,
Tanzania na Afrika.
Lala Peponi Madiba, Pumzika Wetu baba.
Busara hata
kucheka, Yalikukwepa Majoka.
Kisasi ulikizika,
Dunia ikageuka.
Akili wakafunguka,Weusi
utu funika.
Lala
Peponi Madiba, Pumzika Wetu baba.
Hatushangai Mauti,Mioyo yetu si miti.
Upendo wako wa dhati, Umetushika thabiti.
Rufaa si kwa Mauti,Tukashinde kwa manati.
Lala Peponi Madiba, Pumzika Wetu baba.
Hatushangai Mauti,Mioyo yetu si miti.
Upendo wako wa dhati, Umetushika thabiti.
Rufaa si kwa Mauti,Tukashinde kwa manati.
Lala Peponi Madiba, Pumzika Wetu baba.
Daima tushukuruni,
Muumba akisaini.
Michozi tuitoeni,
Tujiombee amani.
Madiba awe rohoni,
Mafunzo mema tendeni.
Lala Peponi Madiba, Pumzika Wetu baba.
Ulale pema peponi,
Sisi wote tu njiani.
Ameamua manani,Sisi
tubishe tu nani.
Tuwemo pia
manyani, Ubora wa duniani.
Lala Peponi Madiba, Pumzika Wetu baba.
0 comments:
Post a Comment