Moja kati ya masomo, ambayo wanafunzi
siku kadhaa hapo nyuma tulikuwa tukifeli kwenye KIDATO cha SITA, ni UCHUMI.
Ukisoma maswali yake, unaona kama tayari umefaulu, lakini majibu yakitoka
unashangaa, alama kubwa ni “C”,pengine hata kitaifa. Sijui mambo yakoje kwa
sasa. Lakini, badala ya
kuwalaumu wanafunzi, wengine walijiuliza na kupata
majibu kuwa, wengi wa walimu waliokuwa wakifundisha uchumi, walikuwa ni walimu
ambao hawakuchukua somo hilo kama la MSINGI wakiwa vyuoni,ila kwa sababu ya
uhaba wa walimu wa uchumi mashuleni, ikawa inawalazimu kufundisha hivyohivyo kwa KUJISOMEA kwanza.
Kwa kweli ilisaidia lakini, tatizo likawa ni wanafunzi kuelewa visivyo na
kuona rahisi kupindukia. Mfano, mzuri ulikuwa matumizi ya nadharia ya “MARGINAL”,
yaani marginal productivity,marginal utility,marginal value na
kadhalika.Na baraza la taifa a mitihani,wao waliuliza maswali kwa kuamini mmefafanuliwa hadi matumizi ya kimtaa,japo walikuwepo wakali walioweza kuelewa zaidi ikiwa ni uwezo wao wa kuzaliwa. Jamani elimu ni ya taifa sio ya wachache.
Kifupi wanauchumi hutumia hii nadharia
kusoma matokeo baada ya kuongeza rasilimali kwa kiwango Fulani,hasa kimoja.
Yaani, mfano ukiongeza mtu mmoja shambani, nini ongezeko la magunia ya mazao,
kama yameongezeka kumi, basi ndio unasema huyo mtu kaongeza kumi, kama
yamepungua matatu, basi pengine kaleta hadithi za LIVERPOOL NA MAN
U, AMA SIMBA NA YANGA, kama sio majungu,na kupelekea hilo. Ulichokijua ndio
MARGINAL, “ONGEZEKO ZIADA litokanalo na kiwango kimoja cha ongezeko la
rasilimali”. Hii inatumika kwenye mambo kibao,ikiwemo hata kuridhika kutoka na
unachokula au kutumia, na zaidi hadi, hufikia hadi kufananishwa na nia ya watu
kulipa pesa kwa ajili ya huduma Fulani. Inaaminika kiuchumi kuwa mtu analipa
kulingana na kiasi cha kurudhika anachotegemea ama kiasi cha msukumo cha kutaka kulipa akilinganisha na
kiasi cha pesa anachoweza kutoa. Hapo ndio hasa tanki linalenga, yaani,uthamani
ambao mtu anawiwa kuulipia. Kwa kweli kuelewa sana uchumi,inabidi tutafute
wanauchumi. Japo kuelewa kidogo, kunaweza kutusaidi sana kwenye maisha yetu ya
kawaida. Lakini kujadili hakuanzushwi na wanaoelewa sana,bali wanaotaka
kuelewa.
Kama mtu analipa kulingana na
anachotarajia, maana yake,mtu akipewa mshahara mkubwa anategemewa kutoa
ongezeko la thamani kubwa Zaidi ya anayelipwa kidogo. Hii inajionyesha sehemu
nyingi,hasa kwenye SOKA LA BONGO,japo sijui makazini,hasa Tanzania. Lakini bado
ukweli,unajidhihirisha kuwa meneja akipiga simu moja,inaweza kuingizia ama
kuindalia,ama kuiokoa kampuni kwa kiasi kikubwa kuliko mfagizi, hata kama
anachafuka sana.
Tukiachana na porojo hizi, tukajikita kwenye UJENZI, eneo mlengwa, maana WABONGO, hawakawii kusema mpaju blogu imekuwa ya kisiasa sasa, imeingilia madai ya kutangazwa mishahara maraisi, kama itasaidi kifikra kulifikiria hilo basi vema. Katika Ujenzi kuna taaluma kama UBUNIFU, UHANDISI, UKADIRIAJI NA KADHALIKA ambazo hasa huwa ziko
katika muundo wa huduma, na zina taratibu madhubuti, kutokana na unyeti wake
kiutendaji na kijamii. Mteja hapa, wakati mwingine hutoa pesa kisheria, na sio
kiupimaji wa thamani yake yeye mwenyewe. Na hata kama kwa namna moja au
nyingine akiwa anapima, bado kuna maswali,yanayojitokeza,kutokana na kuwa na
washiriki kibao,katika kukamilisha huduma na mjengo wenyewe. Kwa kweli,kuna
wakati mteja eneo hili hubaki kama MBONGO akiwa hoi mbele ya daktari, lolote
litakuwa ndio. Bora ujamaa unatuokoa na bei za madaktari. Japo kuna vigezo
vingi vya uthamani katika uwanja huu wa ujenzi, lakini sijui kama wateja
huzingatia vyote kwenye kuamua, na sijui hasa kama sheria zilizopo zilizingatia
vigezo vyote kwa kumtazama mteja mwenyewe au kutazama duniani, na Zaidi sijui
kama upimaji wa thamani iendayo kwa mteja hauathiriwi na mabadiliko ya
kiteknolojia ama la!
Sasa, uthamani wa mteja wa namna hii
chimbuko lake liko wapi? Na je huwa chimbuko hilo ni la kudumu,
ama hubadilika? Nini kipo ndani ya ujenzi na thamani ya malipo kwa wataalamu
wake au hata pamoja na wajenzi? Tanki limeona kuna kitu cha kukichambua japo
kwa upeo kidogo uliopo kwa sababu, ujenzi unaligharimu taifa pesa nyingi
sana,hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha thamani sahihi inapatikana na inaenda
kwa mhusika sahihi. Bila hivyo, hata utaalamu hautakuwa na changamoto za
kimaendeleo.
Ujenzi kama
ununuzi wa simu mtaani, tunaweza kusema, mtu anaita wamachinga anawaambia
nataka simu aina fulani. Wamachinga wanakimbia madukani a kuleta simu kama kumi
hivi,na yeye anachagua moja na kuinunua. Tofauti ni kuwa kwenye ujenzi, mnunuzi
husika huwatumia wataalamu wa simu kumshauri aina na kuwaita wamachinga na
kuhakikisha kama simu waliyoleta ndio yenyewe,na ikibidi kusimamia malipo ya
simu hiyo. Mchakato huo ukiufafanua kwenye mazingira halisi,unaweza kuchanganyikiwa,kiasi
cha kuona ni vema wataalamu hao waongezewe miaka ya kusomea hizo taaluma. Sasa,
nani hasa anayepelekea kumpatia MNUNUZI thamani ya simu yake kati ya wale
mafundi, labda (Architect-Msanifu, anayesema simu iwe hivi, na nivema mkononi
ijae hivi), (Engineers-Wahandisi,wanaosema lazima ihusishe chombo hiki,waya huu
na kadhalika iwe madhubuti), (Quantity Surveyor-Mkadiriaji, anawafafanulia kuwa
simu hii itacheza kati ya bei hizi, na hata kama kaleta kwa mtindo huu, bei haizidi
hii) ama (Contractor-Mkandarasi, anayesema usijali, pesa yako kaa nayo kwanza, utanipa
nikileta simu na baadae anaomba nyongeza kidogo kwa ajili ya taksi ama ndege,akidai
kazunguka kote ili kuleta kitu bora kwa bei nzuri,kama simu yake ndio
iliyochaguliwa).
KIBONGOBONGO,unaweza
kujibu unavyoona, lakini ni vema sana kujua hasa Uthamani ama VALUE, yenyewe ndio nini kwa huyu
MNUNUZI au CLIENT? Ili tukichanganya na uchumi wetu kidogo, tunaweza kuona kuwa
anayestahili kupewa kipaumbele kimalipo, ni nani kati ya kundi tajwa hapo juu,
yaani yule ambaye MCHANGO wake unapelekea ONGEZEKO kubwa la UTHAMANI huo. Ama,
tukitaka kufanya maisha magumu zaidi, tunaweza kuanza kuona UMUHIMU wa kuwepo,
kitu AMBACHO sheria imeturahisishia kwa kusema wote wanatakiwa kuwepo kwenye
UJENZI. Kama ilivyo ada, japo mada haijaisha, wengine watahoji,mbona mwandishi hakugusia, aina zote za ujezi, na mambo kibao yaneye uzito mdogo, kuliko HOJA yenyewe. huo ndio utanzania,wenyewe tunajuana, kikubwa ni kuwa iwe civil works,building works,or any other special works of construction, what exactly is the value the clients get? And are we real proportionally reflecting the value contribution by participants to fees earned, or this economic concept has place in construction. Nimejaribu ung'eng'e,pengine nimeharibu maana kabisa,badala ya kuweka msisitizo. Tutafika ila cha mot tutakiona.
...................................................................Itaendelea..................................................................................
0 comments:
Post a Comment