Friday, December 13, 2013

WAJENZI WA "BONGO" NA MASLAHI YAO


NANI ALIPWE NINI? KWA NINI?
BWANA MIHELA UNAJUA UNACHOKILIPIA?

 ",,,,,,,,,,KIBONGOBONGO,unaweza kujibu unavyoona, lakini ni vema sana kujua hasa Uthamani ama VALUE, yenyewe ndio nini kwa huyu MNUNUZI au CLIENT? Ili
tukichanganya na uchumi wetu kidogo, tunaweza kuona kuwa anayestahili kupewa kipaumbele kimalipo, ni nani kati ya kundi tajwa hapo juu, yaani yule ambaye MCHANGO wake unapelekea ONGEZEKO kubwa la UTHAMANI huo,,,,,,,,"
"(http://mpaju.blogspot.de/2013/12/mshahara-nani-apewe-zaidi-meneja-au.html#more)"
 Interest“, ni neno lenye maana nyingi kwenye kiingereza na masikioni mwa watu, lakini ni MASLAHI, na sio riba ama kitu kingine chochote katika lugha ya kiswahili. Hakuna sehemu muhimu kwa Mtanzania kama mahali penye maslahi yake. Kuanzia kwenye KATIBA YA NCHI, VYAMA, VILABU, FAMILIA na hata MAKAZINI, ogopa sana kugusa maslahi ya mtu. Hatari ya MASLAHI, ni zaidi ya madhara baina ya watu. Inaweza kupelekea hatua ya mtu kupoteza UZALENDO na hata KULITUMBUKIZA taifa kwenye matatizo. Swala la kugombea maslahi sio baya, kama mtu anachogombea ni HAKI YAKE KIMSINGI. Na hilo hasa, likipewa UWAZI mzuri linaweza kubadili taswira nzima ya UBAYA wa MASLAHI na kuleta UBORA wa MASLAHI.

Kwenye Ujenzi, wataalamu hufanya kazi kama timu, japo pia hupambana kugombea kazi hiyo kabla ya kuifanya. Kwa hiyo, kiundani sana, mtaalamu wa ujenzi anatakaiwa kuwa mtu ambaye, UKWELI kwa maana ya UTAALAMU uko mbele, ili asijikute katika wimbi la kuchukia anapokosolewa ama kupokonywa mradi katika harakati mbalimbali za KIUTENDAJI. MASLAHI BINAFSI YASIMTAWALE. Hii haimaanishi kuwa mtaalamu huyu asifuatilie haki zake. Mijadala juu ya uhalali wa malipo inajitokeza sehemu kadhaa, kuanzia kwenye ubishi wa nani anafaa kuwa MKUU wa timu za ujenzi mpaka nani apate kiasi gani katika MIRADI. Muhimu, haiwezi kuwa ubishi bali hoja za kwa nini wataalamu hawa wanalipwa. Ambayo kimsingi, kama mfano wa kichumi unawahusu, basi, wanalipwa kwa sababu wanampatia MTEJA/MSHITIRI/CLIENT uthamani fulani kwa kila jambo ama kipande cha huduma zao.

Maeneo makuu matatu ya UJENZI, mteja/mshitiri, mkandarasi na wataalamu, lazima uyape kipaumbele. Mteja, ndio mtoa pesa na anategemea uthamani fulani, yaani kama vile kupata jengo la kuridhisha na kuanza kutumika wakati sahihi na kwa muda mrefu bila kuleta matatizo yeyote ikiwemo kutoongeza gharama za ukarabati ama matumizi ya nishati na kadhalika.Yaani „SUSTAINABLE FACILITY“. Mkandarasi, ndio mjenzi mwenyewe,anaebadili taswira kuwa kitu halisi. Wataalamu, wenye jukumu la kutoa taswira ya kitu kinachotakiwa na kumfaa mteja kwa mujibu wa taratibu za kitaalamu na sheria za nchi na kusimamia zoezi zima kwa manufaa ya mteja kwa kushirikiana na mkandarasi.

Vigezo vya kujua UFANISI viko vingi, lakini maarufu ni UBORA,MUDA,GHARAMA NA USALAMA. Kwa hiyo hivi vitu vikikamilishwa kulingana na mahitaji ya mteja,ndio kumpa uthamani mteja huo. Na kwa upande mwingine, washiriki hawa wote wanategemewa kutoa mchango kuelekea kwenye vitu hivyo,ili mteja apate anachostahili, na hivyo basi, kama MSANIFU, MHANDISI, MKADIRIAJI NA MKANDARASI, tunamtegemea awe na mchango mkubwa sana katika maeneo ya namna hiyo, ikibidi hata KUMBADILI MAWAZO MTEJA, maana mteja sio mtaalamu na hana dhamana ya UTAALAMU kwa taifa. Na hiyo thamani ya mchango ndio mteja anatakiwa kuilipia, kama unachangia kidogo,basi upate kidogo. Sijui kama hali iko hivi hasa kwa nchi yetu.

Dunia ya leo, sio ya jana. Ubora, leo ni Zaidi ya kukidhi mahitaji ya msingi. Ubora unahusisha mambo mengi ikiwemo kuridhika kwa mteja, ili upate mradi mwingine. Kujenga jengo zuri, likamalizika baada ya miaka miwili badala ya miezi sita, kunaweza kupunguza ubora wa mradi. Hivyo hivyo, muda wa mradi umekuwa pesa kwelikweli, hivyo ukichelewesha mradi umechelewesha kumuingizia pesa mteja. Usalama, katika ujenzi, ni muhimu sana, maana maisha ya watu ni bora kuliko kitu chochote. Na Zaidi Gharama, za ujenzi ni jambo la kulitazama kwa jicho kubwa Zaidi, na pengine ndio chanzo cha Makala hii mbovu.Ukweli maamuzi mengi mara nyingi hupimwa ubora wake kwa kuangalia gharama.

Ukizungumzia gharama kwenye ujenzi, hasa Bongo, utasikia mtu kaguna “BIOKYU hiyo”. Hiyo ndio dhana namba moja, kuwa mkadiriaji wa ujenzi ni muhimu kwa sababu ataandaa mchanganuo wa gharama na kazi za ujenzi, ili zisaidie kuchagua mkandarasi na kufuatilia malipo baadae kama ikiamliwa hivyo. Na wakati mwingine baadhi ya wasomi hufikiria kuwa pengine ukiondoa BOQ, maana yake mkadiriaji ajipange kushuka thamani tenakatika timu ya ujenzi. Mfano ni kwenye ujio wa BUILDING INFORMATION MODELLING (BIM),teknolojia inayoonyesha uweza kuharakisha hesabu za gharama. Sidhani kama kuna ukweli katika hili,lakini kuamini kuwa MUNGU yupo ni bora kuliko kukataa na kutenda dhambi. Teknolojia hii BUILDING INFORMATION MODELLING, inakuja kumboresha mkadiriaji na kumdhihilishia nafasi yake  katika ujenzi,ni mtazamo tu toka tankini.

 Ukweli ni kwamba wataalamu wachache sana wanakubali kuwa mkadiriaji ujenzi anamchango mkubwa kwa mshitiri, na kibaya Zaidi washitiri wenyewe ndio hawana habari kabisa na wakadiriaji ujenzi. Wakiwa makini Makala hii inaweza kuwa uponyo mzuri tu kifikra, kama si kulitupa tanki kwenye kundi la blogu feki.Pengine kuiweka sawa hii ni kusema, mkadiriaji ni mhasibu Fulani wa ujenzi, sasa, kwa mfanyabiashara ama mwajiri makini sidhani kama anaweza kusema mhasibu hana mchango mkubwa kwenye uzalishaji Zaidi. Kimsingi mameneja makini huwa hawachezi mbali na wahasibu,yaani kiutendaji. Vile vile mshitiri makini,anapaswa awe karibu na mkadiriaji pengine kuliko mtaalamu mwingine, hasa anapokuwa na uhitaji sana wa kuhakikisha rasilimali fedha inatumika vizuri, na kumrudishia thamani tarajiwa.

Uzoefu mdogo, unaonyesha kuwa wakadiriaji bongo wanafanya kazi Zaidi na wabunifu, na wakandarasi makini. Wakati huo huo wateja wengi akiwemo TAIFA wanalalamika kuwa gharama za ujenzi ziko juu sana, lakini wanajitahidi sana kuwa karibu na wabunifu,wahansisi ama wakandarasi badala ya wakadiriaji ambao wanaijui siri ya hizo gharama zao. Pengine, malalamiko ni geresha toto. Kujua umuhimu wa mkadiriaji mtu hahitaji kwenda kwenye ukweli wa ndani kama vile umuhimu wa makadirio ya mwanzo ama madhara ya mabadiliko ya maamuzi kadha wa kadha katika mradi. Fikiria kuwa kazi ya msingi ya mkadiriaji ni hiyo ya kuandaa Bills of Quantities (BOQ) tu, kitu ambacho hufanyika hatua Fulani tu wakati mradi umekwishaanza. Bado,pamoja na ugumu wa lugha ya kiufundi, mteja makini unaweza kumbana mkadiririaji, akakusaidia kuvumbua undani wa pesa yako, badala ya kumuacha awe chini ya maamuzi ya wabunifu.

Duniani, gharama kubwa ya majengo, imegundulika kuwa Zaidi wakati wa uendeshaji. Ukarabati, matumizi ya nishati na kadhalika ni vitu ambavyo mbali ya kuwasumbua watumiaji na washitiri, vinaonekana kuwaongezea mzigo mkubwa sana kigharama, na kibaya ni kuwa asilimia kadhaa ya mzigo huo inaweza kupungua kama washiriki hawa wa ujenzi watakuwa makini kwenye eneo lao. Yaani, inawezekana kabisa ikawa mapungufu yao, wanamtupia mshitiri. Unawezaje kupiga picha ya gharama zote hizo bila kumhusisha mkadiriaji ni swali ambalo, tanki linakuachia wewe. Kama haitoshi, Imani ya kuwa KAMA PESA IPO YA NINI KUSHUGHULIKIA GHARAMA? Pia inaweza kuwa na madhara kwenye utendaji wa shughuli za ujenzi, na sio kumpunguzia mkadiriaji umuhimu kama ambavyo wengi wetu tunafikiria. Na pengine ikawa inaongeza maumivu kwa mteja, hasa anapoonyesha kuwa hela sio tatizo. Kivipi?

Fikiria mbunifu, na mkandarasi, wanamjengea mteja ambaye gharama sio swala la kuzungumzia kabisa.Yaani, ni mteja wa ajabu, ambaye hajali leo wala kesho jengo litamgharimu kiasi gani. Bado kuna kiasi ambacho ,wataalamu na mkandarasi watatakiwa kulipwa, kitahitaji makubaliano ni kasi gani, na kama haitoshi kuna maswala ya kodi. Hivyo kama  mkadiriaji hamtetei mteja basi, atalitetea taifa. Zaidi, fikiria kazi atakayofanya mbunifu na mhandisi, kwa kutazama mchango wao wa UBORA, itakuwa yenye umakini mdogo na pengine maumivu kidogo kwa sababu, vigezo vya kuzingatia vimepunguzwa. Na kama hela yake itabaki palepale ama kuongezeka, maana yake anachangia kidogo, na kupata kikubwa. Lakini kwa sababu pesa sio shida, hiyo haina shaka. Na hivyo hivyo kwa mkandarasi, anaweza kutupia upungufu wake kwa mteja, hivyo swala la usimamizi wa gharama huenda lisikwepeke, lakini kama ni mwaminifu,atakuwa na nafasi ndogo tu ya kuvuna pesa isiyo na sababu. Bado kwa kuwa gharama siyo shida,haina shaka. Lakini mwelekeo huu, kwa kiasi kikubwa ndio unatumika. Yaani, mkadiririaji ni mtaalamu msaidizi sana, na huja baada ya kukamilika kwa ubunifu, kitu ambacho kinamuumiza sana mteja ,kwa kutonufaika na hudumu muhimu ya mkadiriaji,katika maamuzi mbalimbali.

Kuna umuhimu wa kuwatumia wakadiriaji mapema kadri iwezkanavo,ili kutoa mchango wao kuhusu gharama. Sababu za kusema tunachelewa,mara nyingi zinapelekea kumuumiza mteja. Hili lieleweke vizuri kuwa, tanki linaamini wabunifu/wahandisi hawawezi kulikubali kirahisi kwa sababu,litawasumbua sana, na pengine kuwapunguzia MASLAHI, yaani kiasi ambacho hawakichangii, lakini pengine wanalipwa kutokana na upungufu wa uelewa wa mteja. Ukitaka mbunifu afikiri sana na kutumia utaalamu wake, lazima afikirie juu ya gharama, maana yake abuni kuelekea kwenye kiasi cha pesa kilichopo, na sio pesa ifuate alicho buni, muundo ambao tunautumia sana na kumuumiza mteja. Mteja analipa na mapungufu ya wataalamu. Kuna mengi ya kuongea na kujadili, lakini kwa kumalizia ni vema kufikiria muunganiko wa ubora na gharama anayobeba mteja. 

Fikiria. Wewe kama mteja. Kimsingi, mtaalamu atakuchaji gharama/pesa yake ya utaalamu, ambayo itakuwa ni jumla ya gharama zote za kukamilisha kazi yako, na faida yake kidogo. Mkandarasi pia hivyo hivyo, atachaji gharama ya kukamilisha ujenzi pamoja na faida yake. Yaani wewe utatakiwa kuweka BAJETI yako kiasi cha pesa sawa na hizo pesa zote. Kimsingi kwenye zile gharama kuna vitu ambavyo, ndio mchango wa uthamani kwa mteja,mfano kutafuta bei mbalimbali za vifaa vya ujenzi kwa mkadiriaji, kubuni na kuprint michoro mingi kadri inavyohitajika kupata mchoro bora na kuwahusisha watu wadau mbalimbali ili kupata kitu bora. Na mkandarasi, pia ana mambo kama hayo likiwemo kutoa ushirikiano mzuri na kujituma ili kurahisisha kumaliza kazi kwa hata kupunguza mapungufu yasiyokwepeka kutoka upande mwingine.   

BAJETI YA MRADI= (Gharama za ujenzi + Faida yake mkandarasi) + (Gharama ya thamani utaalamu + faida ya Wataalamu) + nakadhalika
Sasa kutokana na mtzamao wa mlinganyo huo, unaweza kuona ni jinsi gani wataalamu hawa wana dhamani ya kumuokoa mteja, ikiwa ni ukweli kuwa wao wanahusika kushauri juu ya gharama zingine zote.  Na huu mlinganyo unatupatia msingi wa UTHAMANI UNAOCHANGIWA KWENYE MRADI.

Yaani kifupi UTHAMANI WA MRADI= UTHAMANI WA UJENZI + UTHAMANI WA UTAALAMU. Kwa hiyo, kama wataalamu watakuwa na mapungufu yanayoshusha Uthamani, basi mteja anapata thamani ndogo kuliko pesa anayowalipa. Mteja anatakiwa kujiuliza, ni nani mchango wake unampunguzia maumivu hayo, na kumuongezea UTHAMANI KUPITIA VIGEZO VOTE HIVYO, na hasa ndio mtu wa kuwa NAYE BENETI. Hii inatupeleka kwenye kujiuliza kama, WATEJA wetu wanajua hili, JE MALIPO YANALIFUATA HILI, AMA HALIWAHUSU wajenzi? Je likoje? Ni la kudumu, ama linabadilika kulingana na mazingira ya mradi?
Ni matumaini ya tanki kuwa hizi ni changamoto muhimu kuongelewa.

………AMANI IWE MBELE KAMA MASLAHI YA MTU YAMEGUSWA……………

"UZALENDO KAZI KAMA MAPINDUZI TU, WENGI WANAUKIMBIA"



0 comments:

Post a Comment