MPANGO WA LAZIMA KUPITIA JKT, HAUNA MASLAHI MAKUBWA KWA TAIFA LETU
NUKUU YA 1. KUTOKA KWA DEUDATUS BALILE, 04 March 2013 09:45 “http://modans.go.tz/site/index.php/jeshi-la-kujenga-taifa-laagizwa-kuajiri-vijana-wa-kujitolea-“
“……Kwa Mujibu wa Meja Jenerali Muhuga uwezo wa kifedha uliopo ni mdogo kuhudumia watu katika kambi zote nchini, kinyume na ilivyokuwa JKT ya awali kwamba wahitimu wote wa kidato cha sita wanajiunga na JKT kwa lazima. Hivyo kati ya wahitimu zaidi ya 41,000 waliomaliza kidato hicho mwaka 2013 ni 5000 tu ndio watajiunga kwa lazima na kutoka katika kundi la hiyari la vijana pamoja na wabunge 47 watakaokuwa kambini kwa wiki tatu.
NUKUU YA 2. KUTOKA http://sabahionline.com/sw/articles/hoa/articles/features/2012/06/21/feature-02
Tanzania
inajiandaa kurejesha mpango wa taifa wa jeshi la Kujenga Taifa, ambao
ulisitishwa miaka 20…………….Pamoja na mafunzo ya kijeshi yenye kiwango,
mpango huu pia hutoa mafunzo juu ya haki za binadamu, elimu ya uraia,
na historia ya Tanganyika na zanzibar, na pia unakusudiwa kuamsha hisia
za umoja
na uzalendo kwa wanafunzi.
Waziri
wa Fedha wa Tanzania William Mgimwa
aliliambia bunge wiki iliyopita kuwa kiasi cha shilingi bilioni 7.5 (dola milioni 4.7)
zitatengwa katika bajeti ijayo ili kufufua mpango wa Jeshi la Kujenga Taifa.Kwa
kuanzia, wanafunzi 5,000 tu wahitimu wa elimu ya juu watachaguliwa kushiriki
katika mpango huo.
Waziri
Mkuu wa zamani Edward Lowassa
aliukaribisha uamuzi wa kuanzisha mpango huu, kwa kusema Jeshi la Kujenga Taifa
liliwapa wanafunzi kutoka matabaka tofauti fursa ya kukaa pamoja kabla ya
kujiunga na chuo kikuu na kujifunza kuhusu uzalendo na maadili ya Tanzania.
Alisema
baadhi ya majirani wa Tanzania wameshindwa kufikia makubaliano katika nchi zao,
jambo ambalo limechangiwa na kutokuwa kwao na utulivu. Tanzania imeweza kujitofautisha
katika hilo kutokana na Jeshi la Kijenga Taifa, alisema.“Amani
yetu haiwezi kutenganishwa na Jeshi la Kujenga Taifa,” Lowassa alisema.
Kujenga kujiamini na kuimarisha umoja
Simon Mokiwa,
mwenye umri wa miaka 42 na mkazi wa Dar
es Salaam, ambaye alitumikia Jeshi la Kujenga Taifa katika kambi ya
Bulombola Kigoma mwaka 1991, alisema shughuli hizo zilisaidia kujenga moyo
wa ushindani na mtu kukabiliana na utofauti wa Tanzania. Mokiwa
aliiambia Sabahi kuwa jeshi la Kujenga Taifa liliwasaidia vijana kujiamini
wakati huo huo kujenga hisia za umoja.“Liliwaunganisha Watanzania wa asili
mbali mbali,” alisema. “Wahindi, weupe na weusi walikwenda kambini,
kufunzwa, kulima mashamba pamoja, bila ya kujali asili za familia zao. Nafikiri
ni kitu kizuri kwa kizazi kipya na kwa taifa letu pia.”
Luteni
kanali Hashim Mzava, afisa wa jeshi mstaafu, aliiambia Sabahi kuwa
kufufuliwa kwa mpango wa Jeshi la Kujenga Taifa kutasaidia kuwajenga
vijana na maadili mema ya kazi. “Watafunzwa mambo mengi kuhusu Tanzania na
maslahi ya taifa. Haya hayafunzwi katika mtaala wa kawaida wa shule.”
Ikiwa serikali iko makini kuhusu
kuugharimia mpango huu, lazima itenge pesa zaidi, alisema mwanauchumi Honest
Ngowi.Ngowi, ambaye anafundisha katika Chuo Kikuu cha Maumbe, alisema wanafunzi
5,000 ambao sasa serikali imeshawapangia bajeti, ni sehemu tu ya wanafunzi
700,000 wanahitimu elimu ya juu kila mwaka.Ikiwa Watanzania wote watahitajika
kushiriki katika mpango huu kabla ya kujiunga na chuo kikuu, lazima pesa nyingi
zaidi ziingizwe ili kuuendeleza, alisema.
MWISHO WA KUNUKUU.
3. KUTOKA
TANKINI
Naipongeza serikali na wabunge wetu
kwa kutambua kuwa kuna umuhimu wa kuwa tunathamini ZAMANI yetu Hili ni jambo
jema na hasa pale tunapotambua kuwa uzalendo wan chi umeshuka, umoja unapotea
na mambo mengi kama hayo ambayo yalikuwa nguzo kubwa sana katika kufikia hapa
tulipo. Kwa kweli kuna mengi ya kujifunza na kuyaenzi kutokana na ZAMANI yetu. Lakini
tunaisoma historia yetu ili iweze kutusaidia kuboresha leo na kesho,kulingana
namazingira tuliyonayo. Ndio hasa tutapata faida ya HISTORIA na ZAMANI yetu.
Kwa kulitambua hilo, TANKI lina
mchango TOFAUTI kwenye Maamuzi ya Kurudisha Utaratibu Wa Lazima kujiunga na
Jeshi la Kujenga Taifa. JKT SIO MUHIMU KWA WATANZANIA WA LEO NA KESHO.
Wengi wa wachangiaji katika nukuu
za hapo juu wameonekana kuamini kuwa Mpango huu utaturudishia Uzalendo
Maadili, Umoja,Ukakamavu,Uvumilivu na kujenga msingi wa Amani. Japo
bado hatukupewa ushahidi wa kitaalamu juu ya hili, naheshimu uzoefu wa watu
walionukuliwa.
ANGALIZO 1 : MABADILIKO TUTAENDANA
NAYO?
Wakati umebadilika sana, mtoto wa
miaka ya sitini, si sawa kabisa na
mtoto wa miaka ya tisini, na si sawa kabisa na mtoto wa miaka ya 2000. Sio tu
kitabia, kimitazamo na kimahitaji bali hata kiafya. Ni watu wenye mazingira tofauti hata
aina yao ya vyakula. Sijui kama uzoefu wetu unaweza kututhibitishia kuwa
mafunzo ya jeshi yataliona hili. Au tutaombana tu msamaha pale mtoto tena wa dawa
wa mtu akifariki kwa sababu ya mchakamchaka,
ambao hajawahi kukimbia tokea akiwa darasa la kwanza. Na Zamani, wengi walikuwa
wanategemea elimu na kazi kutoka serikalini, na pengine ndio maana wakawa
hawana ujanja juu ya jeshi. Lakini kwa sasa hivi, wakati mtoto kasomeshwa Uganda,
chekechea, msingi Kenya, na Sekondari na chuo kamalizia India, akikataa kwenda
jeshini,adhabu yake ni nini? Sio hivyo tu, miezi sita ambayo lazima apite
jeshini,kama mzazi wake kapata nafasi ya kazi, inakuwaje,maana hatuna tena
waajiri wa kusubiri umalize Jeshi. Kuna mengi pia juu ya Maadili na maana zake,
kitaifa na kijamii. Sijui kama maadili tunayoyaongelewa hapa hapa ni yale ya
kitaifa zaidi au pamoja na kijamii,ambayo kuna baadhi hupatiwa na wazazi wao
kupitia aina Fulani ya mifumo kama ya Dini.
ANGALIZO 2 :
Amani kimsingi huambatana sana na
haki. Sasa kwa kurudisha jeshi la kujenga taifa, tunaboreshaje misingi ya HAKI
na haki zenyewe za mtanzania? Makundi mengi sana yanahitaji kutimiziwa haki
zao,likiwemo kundi la MKULIMA, uwepo wa jeshi unaboreshaje haki yake? Kwa
kuwaingilia vijana kwenye mipango yao ya kimaisha na kuwalazimisha kuwa lazima wapitie
Jeshini, tunaboresha vipi haki hapo? Tusinywe dawa bila kujua ugonjwa, tunaweza
kuongeza sumu mwilini. Amani ya Tanzania inahatarishwa na kasi ya kujitokeza
kwa matabaka ya walio nacho na wasionacho. Amani ya Tanzania inahatarishwa na
FIKRA MBOVU kwenye maeneo ya UWAJIBIKAJI, IMANI ZA DINI NA UZALENDO. Na
wanaohatarisha amani ya Tanzania sio vijana kutoka matabaka ya WATANZANIA WA
KAWAIDA, bali baadhi ya viongozi wa nchi na uwepo wa kundi kubwa la wanasiasa feki
ambao kutwa ni kuhubiri juu ya mambo ya kichochezi na uongo kwa ajili ya
maslahi yao. Jeshi litaweza kuyaondoa hayo kichwani mwa kijana kwa muda wa miezi sita, au
litamuongezea ujasiri wa kutetea fikra zake potofu kufa nakupona. Ama nalo
jeshi litazidi kujenga matabaka kwa kuwafanya wasiopita jeshini kuwa raia feki.
ANGALIZO 3.
Bilioni 7.5, (yaani Kama vile
Matreka safi 170) zimetengwa kwa ajili ya wanafunzi 5000 wa mwanzo, wakati
wanaotakiwa ni (41,000). Na uzoefu mdogo niliona ni kuwa hizi pesa hazitatosha
kwa hao 5000. Je, hizi pesa hasa zilitolewa kwa nani? Kodi ya Watanzania, ndio
jibu sahihi. Je, kama tatizo lilisababisha kusitishwa kwa jeshi hili lilitokana
na UKAPA, tayari kuna mahali sasa ambapo tutakuwa na uhakika wa kupata pesa
bila kuyumba? Au ndio hidithi zile zile baada ya miaka miwili. Au uchumi sasa
unakuwa kwa kasi kiasi cha kutuhakikishia kuwa na pesa hiyo bila wasiwasi. Na hakuna ubishi kuwa jeshi lazima liwe la
kiwango, maana vijana wa sasa ni wa kiwango na ukizingatia kutakuwa na
mchanganyiko wa jinsia. La sivyo, ule ubovu wa maadili ndio utazidi na ununda
utakuwa mara dufu. Mwanauchumi Ngowi hakutaka kuweka chumvi yeyote zaidi ya
kusema kama Serikali inataka kufanya hilo lazima iandae pesa nyingi. Hii
haiwezi kuwa ni sababu tosha kuona pengine serikali imeamua hili kisiasa zaidi?
Maamuzi ya kisisasa kwenye mambo yanayogusa utaalamu mara nyingi huwa na
madhara baada ya muda mrefu,tujiandae.
HITIMISHO LA TANKINI
Ni vema kila mtanzania anapokuwa na
jambo la kuzungumzia kitaifa ajitahidi na kuweka hata kawazo kidogo. Uhuru wa
kutoa mawazo ni mkubwa nchini mwetu na ndio wengine tunaishia kutukana viongozi
wengi kitu ambacho sio sawa kabisa.
1.
TUBORESHE ELIMU YETU.
Yote tunayoyahitaji kwa dunia ya
leo yanapatikana katika ELIMU BORA. Elimu bora huboresha fikra za mwananchi na
kumpa upeo wa kuchanganua mambo kulingana na uhalisia wa mazingira aliyonayo.
Serikali ianzishe KODI maalumu kwa ajili ya elimu na idhamilie kuweka misingi
ya elimu bora. (Soma Makala ya Kuoberesha Elimu).
2.
IMARISHA MAJESHI
Majeshi yako kibao Tanzania.
JKT,TWTZ,POLISI,MAGEREZA,UHAMIAJI NA ZIMAMOTO. Haya yote yakipewa kipaumbele,
yanatosha kuwa njia za kuwapatia wale WANAOTAKA kupitia majeshini, hizo nidhamu
za jeshi kwa manufaa yao na ya kitaifa. Mpaka sasa hakuna Jeshi ambalo lina
Askari wa kutosha. Hata uwiano wa askari na idadi ya wananchi pengine hautoshi,
kitu ambacho maana yake haki ya ulinzi kwa watanzania na mali zao bado ina mapungufu
sana. Kuboresha majeshi ni nguzo muhimu sana kwa maendeleo ya taifa. Kwa sasa
jeshi kama la magereza nafikiri linaelekea kuwa linatia hasara taifa kuliko
faida, wakati lilikuwa kati ya majeshi yanayoweza kujihudumia kwa kiasi kikubwa
tu. Wape kipaumbele wanajeshi kwenye maeneo mbalimbali na kuwapa haki zao za
kimaisha.
3.
BORESHA HAKI NA WAJIBU KWA WATANZANIA WA KAWAIDA.
Kitu cha muhimu kuwatanguliza
watanzania kwenye kila jambo la kitaifa, na HII NDIO DHAMBI KUBWA INAYOWATAFUNA
viongozi,serikali,wanasiasa wetu mlio wengi. Na itatafuna kizazi chetu chote,
hata tukiwa kaburini. Tunachohubiri sio tulichonacho vichwani mwetu. Hatuwezi
kukaa meza moja tukatafakari yahusuyo taifa, kisa hatuko CHAMA kimoja. Marufuku
kumsifia mwenzio au kuchukua ushauri wake kisa, utachekwa umetumia sera za
CHAMA kingine. Hatuwezi kusifiana pale tunafanya vizuri kwa sababu tu tuko
vyama tofauti. Je huo ndio wajibu wetu kwa jamii yetu? Tokea tumetangaza MBIU
ya Kilimo kwanza, mkulima wa jembe la mkono ameonja utamu wa kauli mbiu hii, na
je wote tunaiunga mkono? Tunakumbusha ipasavyo na kushiriki kwa vitendo? Kata matumizi
ya serikali yasiyo na umuhimu, tembea na wanyonge na lala nao majalalani uone
kama uzalendo umekufa Tanzania.
NAAMINI NA WEWE MZALENDO WA KWELI UNAYO YAKO, ONGEZA ILA;
“WENGI WAPE
NA
MBISHA
WENGI MCHAWI”
“Tusiwe wajinga kama jamaa aliyekubali kufa aking'ng'nia kuwa dunia ni mviringo”
0 comments:
Post a Comment